Nataka Rais Magufuli ashindwe

Nataka Rais Magufuli ashindwe

Status
Not open for further replies.
Chadema walivyoogopa kuandamana, ndio imetoa kicwa kwa viongozi wetu kuona kwamba sie bado ni waoga tuu. Watatufanya wanavyotaka, period!
 
Kwa jinsi navyoona itafikia hatua mitandao itaanza kublokiwa kama china.chamsingi hapa hawa wandugu wahamishe tu location waanze kuoparate kutoka nje wakiwafungia tunaanza kutumia VPN tu.china hadi gugo waliifingui lakini bado inatumika tu.hili li inchi lishaanza kuwaka moto bora kujilipua tu bichi
 
  • Thanks
Reactions: ibn
Miezi michache iliyopita rais Magufuli alisema anatamani malaika ashuke [sijui ashuke toka wapi] aje kuizima mitandao ya kijamii ambayo tumekuwa tukiitumia kupashana habari na kubadilishana maoni na mawazo kuhusu mambo mbalimbali.

Baadhi yetu tuliyachukulia maneno hayo kama ishara ya mambo yajayo kuhusu uminywaji wa hii mitandao na haki ya watu kuitumia kwa kujieleza, kutoa maoni, na kuikosoa serikali.

Sasa kitendo kilichotokea jana cha kukamatwa kwa Max kimethibitisha kuwa huu utawala wa Magufuli umeazimia kutuziba midomo kwa kutumia mabavu ya dola.

Kwa hilo mimi nataka huyo Magufuli ashindwe na alegee kabisa. Sitaki kabisa afanikiwe hata kidogo na watu wote wenye akili zao timamu hawana budi kumpinga na kuifanya hizo azma yake iwe muhali.

Kupinga udhalimu ni jambo la adhama. Na huyu mtu tayari keshaonyesha dalili zote za udikteta. Hivyo tumpinge kwa pumzi na nguvu zetu zote. Kwanza ni mtumishi wetu na si vinginevyo.

Hizi siyo zama za kupelekeshana kwa vitisho. Haogopwi mtu zama hizi.

Akichemka tutamkosoa tu. Akichapia Kiingereza tutamcheka tu. Kama hana ngozi nene ya kuweza kumudu na kuvumilia kuongelewa kwa namna yoyote ile basi aondoke. Aachie ngazi.

Mtu mwenyewe kwanza hafai kuwa rais. Hana haiba ya urais, hana hekima wala busara zinazotakiwa mtu wa kiwango cha rais kuwa nazo. Kila akifungua mdomo wake mtu unaanza kuombea asiongee maneno ya kuaibisha.

Sikuwahi hata siku moja kudhani kuna mtu angekuja kumpiku JK kwenye ubomu lakini ndani ya mwaka tu huyu jamaa keshamuacha mbali mno JK. Pata picha hiyo miaka minne iliyobaki hali itakuwaje.

Huyu mtu tumdindie. Tukinywea atavimba kichwa na kujiona ana nguvu nyingi ilhali hana. Hana nguvu za kuweza kuzidi nguvu ya umma.

Kwa hiyo mimi nataka ashindwe. Tena ashindwe vibaya. Je wewe mdau wasemaje?
'IF WISHES WERE HORSES BEGGARS WOULD FLY'
 
Yeyote anayetaka kuzuia na kuzima taa inayowaka kwa vijana kupitia jamiiforum kwa vijana kupata habari alaniniwe na kila mtu.

Ni vema nchi ikaongozwa kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi na si mawazo na mtizamo wa mtu mmoja.

Jambo l a muhimu ni watu wote kufahamu kuwa uongozi ni dhamana na una mwisho wake na hakuna hata mtu mmoja atakayeongoza wengine maisha yake yote.

Hujuma yeyote dhidi ya jamiiforum na mitandao yote ya mawsiliano ishindwe na kulegea katika jina la Yesu.

Max Melo aachwe huru mara moja aendelee na shughuli zake na si kumtengenezea mazingira ya kumtisha kama inavyoonekana sasa.

Tuacheni huru jamani mmetubana mno hadi tunakosa amani duuu!!!
 
Kwa nini usimdindie wewe mmeo na watoto wako nyumbani kwako mpaka utuhusishe sisi. Chuki binafsi ni matapishi tu unayotuletea hapa. Hatuna muda nazo. Kama umeshindwa maisha hapa duniani kwa nini usijaribu ahera !
Unatoa mapovu bure tu...
 
Na ye huwa anaisoma namba akiwa Magogoni..polepoleehhh wana JF jmn ohoo msije mtoa roho mwenzenu, anajua kutumbua tuu,kutumbuliwa kunaumaaa kumbeee hahaaahaaha
 
Naona akisomaga baadhi ya comments itakua hadi anazimia hadi wampepeeee...
 
Kwani mtu ukitoa maoni yako pasipo kutoa matusi au ukianzisha uzi wenye uhalisia na usio wa kichochezi unakuwa na hofu ya nini?

Tatizo lililopo kuna baadhi yetu tumekuwa maarufu kutunga stori za uongo na kuzijengea hoja then tunataka jamii iamini kama ni kweli kumbe ni upotoshaji

Mtu kama umeanzisha mada yako na ushahidi unao kwa nini uogope? Endapo utahitajika polisi si unapeleka ushahidi?

Fikiria mtu anayeanzisha uzi hapa eti Dangote anahamishia kiwanda Kenya na hizo habari zinasambaa dunia nzima kumbe ni uonge pasipo kufikiria negative impacts kwa wawekezeji walioko huko nje. Mtu kama huyu leo hawezi fanywa kitu sababu tu anatumia ID feki sishangai kesho akaibuka na jambo jingine

Watu wa namna hii lazima washughulikiwe hakuna kulea ujinga. Watanzania tumekuwa maarufu sana wa kupika majungu

Ninakubaliana na wewe kabisa uhuru wa kutoa maoni lazima uheshimiwe na watawala kwani ni takwa la kikatiba lakini uhuru huo lazima uzingatie utu na nidhamu.

Leo mtu akimchukia mtu flani sababu za kiitikadi za vyama au jambo lolote, kesho anamtungia tuhuma na kusambaza kwenye mitandao. Vitu vya namna hiyo siyo vya kulea

Kwani mtu akianzisha habari hapa kwamba Dangote anahamishia kiwanda Kenya na wewe ukaamini, unafikiri ni nani anapaswa kuswekwa rumande? Kwa maoni yangu, ni wewe unayeamini vitu hovyo hovyo bila kuhoji. Jinga kabisa. Tena hustahili kuchangamana na jamii. Unapaswa kufungwa. Yaani mtu anakuambia lile likiwanda linahamishiwa Kenya na wewe unakubali tu kama zuzu. Na kwa taarifa yako, investors ni watu makini and very informed. Usifikiri wanayumbishwa kwa taarifa fake unazoweka hapa JF. Umeniuzi sana kwa sababu ni watu wenye mawazo kama yako mnaojenga hoja za kijinga mpaka Max yuko ndani sasa na hatima yake haifahamiki. Eti impacts kwa wawekezaji huko nje! Ndio ulichomwambia JPM na kufanya Max akamatwe? Mijitu mingine sijui kwanini imetokea kuwa sehemu ya jamii yetu. Nalaumu sana elimu yetu. Ndio imetupatia watu wa namna hii. We need to do something guys.
 
Yeyote anayetaka kuzuia na kuzima taa inayowaka kwa vijana kupitia jamiiforum kwa vijana kupata habari alaniniwe na kila mtu.

Ni vema nchi ikaongozwa kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi na si mawazo na mtizamo wa mtu mmoja.

Jambo l a muhimu ni watu wote kufahamu kuwa uongozi ni dhamana na una mwisho wake na hakuna hata mtu mmoja atakayeongoza wengine maisha yake yote.

Hujuma yeyote dhidi ya jamiiforum na mitandao yote ya mawsiliano ishindwe na kulegea katika jina la Yesu.

Max Melo aachwe huru mara moja aendelee na shughuli zake na si kumtengenezea mazingira ya kumtisha kama inavyoonekana sasa.

Tuacheni huru jamani mmetubana mno hadi tunakosa amani duuu!!!
Ndo ushangae yanii...vitu kibaooo wamebanaaa posho,safari nje,semina,hela kwny mzunguko,uchumi,maandamano,n.k wamebanaaaa hatarii walau tupumuliee hapaaa JF,polisi na serikali hebu tuacheniiii tuwe huruu kutoa stress online,tuyaseme yetu ya moyoni wapiiiiii,,,,????
 
Vijana wa Kitanzania mnaongoza kwa UNAFIKI ulimwenguni. Unatumia Fake ID humu JF wakati huo huo unahoji Uhalali na Utendaji wa Rais wa Jamhuri ya Muungano! Ama kweli wapiga Dili mmeshikwa pabaya.
Je na wewe hiyo ID yako siyo feki?
Nyani haoni kundule...
 
Watu wa aina yako ni wengi ktk Africa na Tanzania binafsi sioni shaka inawezekana upo kazini ni sehemu ya maisha yako.
Kwa kizazi cha aina yako Africa na Tanzania inahitaji miaka 10000 kufikia Dunia ya kistaarabu.
mkuu kwa watu ka huyo yangekuwa mahindi au mifugo mbegu yake ingekuwa ilisha telekezwa mda maana haifai
 
Miezi michache iliyopita rais Magufuli alisema anatamani malaika ashuke [sijui ashuke toka wapi] aje kuizima mitandao ya kijamii ambayo tumekuwa tukiitumia kupashana habari na kubadilishana maoni na mawazo kuhusu mambo mbalimbali.

Baadhi yetu tuliyachukulia maneno hayo kama ishara ya mambo yajayo kuhusu uminywaji wa hii mitandao na haki ya watu kuitumia kwa kujieleza, kutoa maoni, na kuikosoa serikali.

Sasa kitendo kilichotokea jana cha kukamatwa kwa Max kimethibitisha kuwa huu utawala wa Magufuli umeazimia kutuziba midomo kwa kutumia mabavu ya dola.

Kwa hilo mimi nataka huyo Magufuli ashindwe na alegee kabisa. Sitaki kabisa afanikiwe hata kidogo na watu wote wenye akili zao timamu hawana budi kumpinga na kuifanya hizo azma yake iwe muhali.

Kupinga udhalimu ni jambo la adhama. Na huyu mtu tayari keshaonyesha dalili zote za udikteta. Hivyo tumpinge kwa pumzi na nguvu zetu zote. Kwanza ni mtumishi wetu na si vinginevyo.

Hizi siyo zama za kupelekeshana kwa vitisho. Haogopwi mtu zama hizi.

Akichemka tutamkosoa tu. Akichapia Kiingereza tutamcheka tu. Kama hana ngozi nene ya kuweza kumudu na kuvumilia kuongelewa kwa namna yoyote ile basi aondoke. Aachie ngazi.

Mtu mwenyewe kwanza hafai kuwa rais. Hana haiba ya urais, hana hekima wala busara zinazotakiwa mtu wa kiwango cha rais kuwa nazo. Kila akifungua mdomo wake mtu unaanza kuombea asiongee maneno ya kuaibisha.

Sikuwahi hata siku moja kudhani kuna mtu angekuja kumpiku JK kwenye ubomu lakini ndani ya mwaka tu huyu jamaa keshamuacha mbali mno JK. Pata picha hiyo miaka minne iliyobaki hali itakuwaje.

Huyu mtu tumdindie. Tukinywea atavimba kichwa na kujiona ana nguvu nyingi ilhali hana. Hana nguvu za kuweza kuzidi nguvu ya umma.

Kwa hiyo mimi nataka ashindwe. Tena ashindwe vibaya. Je wewe mdau wasemaje?
kwa sasa ndo nimegundua uraia wa nchi mbili ni muhimu sana.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom