Nataka nifumue ukweli kuhusu 666

Nataka nifumue ukweli kuhusu 666

Leo nawiwa kufumua ukweli wote kuhusu chapa ya 666 ili watu waache kudanganyana.

Nalipika somo nakuja.
Ila kwa kifupi tu, hii 666 chimbuko ni Israeli kwa mfalme Suleiman.

Why 666 and not other digits? Nakuja!
NB: ukweli huu ulijulikana na wachache mno mimi nikiwa mmoja wao
Hamna kitu hapa, poyoyo tu kama poyoyo wengine
 
Huo ni uongo. Ufunuo umeandikwa ili kumfunua Yesu.
Siyo mambo yajayo. Ni yale yaliyopita


UFUNUO WA YOHANA 1: 1 Ufunuo wa Yesu Kristo, aliopewa na Mungu awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi; naye akatuma kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumwa wake Yohana;


MAMBO AMBAYO HAYANA BUDI KUWAKO UPESI BAADA YA YESU KUONDOKA.

NASISTIZA VIJANA MUWE MNASOMA, SOMENI

ELIMU.
ELIMU.
 
Zishike amri, mengine hayana maana

Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia.

Ayubu 22:21


Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.

Yoshua 1:8



UNAMJUA MUNGU KWA KULISOMA NENO LAKE TAKATIFU NA KULISHIKA
 
Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia.

Ayubu 22:21


Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.

Yoshua 1:8



UNAMJUA MUNGU KWA KULISOMA NENO LAKE TAKATIFU NA KULISHIKA
Yeye amekuambia zishike AMRI. Kumjua Mungu pia kunahusiana na kulishika amri. Hatupo kwenye torati TENA.
 
UFUNUO WA YOHANA 1: 1 Ufunuo wa Yesu Kristo, aliopewa na Mungu awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi; naye akatuma kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumwa wake Yohana;


MAMBO AMBAYO HAYANA BUDI KUWAKO UPESI BAADA YA YESU KUONDOKA.

NASISTIZA VIJANA MUWE MNASOMA, SOMENI

ELIMU.
ELIMU.
Wewe ndio bado hauna hiyo elimu.
Hayana budi 'kutokea upesi' kwahiyo hiyo upesi unaiairisha na kusema haijafika bado.

Soma, Soma.
 
Katika mfumo wa shetani upo mpangilio wa namba 6 ambao kila mmoja unasimamia kitengo fulani.
Pana 111,333,555,666,777,na 999.
666 inashughulika na uchumi, hizo namba zingine ni kitengo cha mambo ya siasa, technology, dini,afya,, nk,sio mada yake kuhusu uchambuzi huu wa namba.
Papa ni mfumo wa dini tena kwa wakatoliki,papa ni kiongozi wa wakatoliki na sio kiongozi wa Wakristo hana amri juu ya Wakristo bali Wakatoliki,na sio mfumo wa uchumi.
666 ni mfumo wa kiuchumi na sio mfumo wa kidini,asiye na chapa yaani asiyefata mfumo huo wa kiuchumi hawezi uza au nunua. Mfano huwezi panda ndege bila kuchanjwa huu ni mfumo Ili upate huduma ni lazima ufate walichoweka.
Ujio wa corona ilikuwa ni test ya 666 walikuwa wanapima matokeo.
So 666 ni mfumo na sio Mtu. Papa hana influence kwa dunia bali kwa wakatoliki Papa mwenyewe yupo under control ya system ya dunia, ambayo akienda kinyume nayo wanamuua, atakuaje 666 sasa? 666 ni mfumo wa wakuu wa Dunia Pope ni mkuu wa dunia, wapo group ambao wao ndio uamua dunia iende vipi.
Hao ndio uamua wimbo gani uchezwe duniani ugaidi, corona, ushoga,

Ukipata wasaaa uje na ufafanuzi wa hizo namba
 
UFUNUO WA YOHANA 1: 1 Ufunuo wa Yesu Kristo, aliopewa na Mungu awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi; naye akatuma kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumwa wake Yohana;


MAMBO AMBAYO HAYANA BUDI KUWAKO UPESI BAADA YA YESU KUONDOKA.

NASISTIZA VIJANA MUWE MNASOMA, SOMENI

ELIMU.
ELIMU.
Soma upya ufunuo sura 12 kwa mfano.
Alafu useme yatatokea au yalikwisha tokea?
 
. Mnyama ana jina lenye namba 666.

Ufunuo 13:17 “tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, ispokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.”

Ufunuo 13:18 “Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinaadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita.”

Biblia inatuambia kuwa hesabu au namba ya jina la mnyama ni 666

Kanisa la Romani Katoliki hudai kuwa Papa ni kichwa cha kanisa au mwakilishi wa Yesu.

“Maneno yaliyoandikwa katika kofia (miter) ya Papa ni haya, ‘VICURIUS FILII DEI’. ambayo ni ya kilatini kwa ajili ya ‘KASISI WA MWANA WA MUNGU’. Wakatoliki huchukulia kwamba kanisa, ambalo ni jumuiya ya kuonekana, lazima liwe na kichwa cha kuonekana. Kristo, kabla ya kupaa kwake kwenda mbinguni, alimteua M.t. Petro kuwa kama mwakilishi wake…hata hivyo Askofu wa Roma, kama kichwa cha kanisa, alipewa jina ‘KASISI WA YESU.'” –Our Sunday Visitor, (Catholic Weekly) “Bureau of information,” Huntington, Ind., April 18, 1915.

Kwa hiyo “VICARIUS FILII DEI” ndilo jina linalotumiwa na mamlaka ya Upapa na kumthibitisha Papa kama kichwa cha kanisa.

Helufi za kilatini zinaweza kutumika pia kama namba, na siku hizi hujulikana kama “Namba za Kirumi,” na helufi U inaweza pia kutumika kama V.


VICARIVS FILII DEI”

(Kasisi wa Mwana wa Mungu)

V...............................5
I.................................1
C.......................... 100
A..............................0
R,.............................0
I................................1
V.............................5
S.............................0
F..............................0
I................................1
L.............................50
I...............................1
I................................1
D..........................500
E..............................0
I.................................1
Jumla =666

Vicarius inamaanisha, katika nafasi ya
Filii Mwana
Dei Mungu
Hivyo, kanisa la Romani Katoliki linatimiza unabi huu wa hesabu ya mnyama 666 kwa ukamilifu kabisa.

11. Onyo la Mungu kwa wote walio katika kanisa katoliki.

Mungu anaoya vikali sana juu ya wale wote ambao wanashirikiana na mnyama huyu, kama wewe ni mmojawapo unapaswa kuchukua uamuzi sahihi sasa bila kupoteza muda; kwa maana hukumu itakuja juu ya mnyama na yule kahaba (kanisa Katoliki) aliyekaa juu mnyama. Hili ni onyo la mwisho la upendo na la rehema kutoka kwa Mungu.

Ufunuo 14:9-10. “Na mwingine, malaika watatu, akafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo ya gadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo.”

Ufunuo 19:20 “Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa wangali hai katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti;”

Ufunuo 18:4 “Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake. Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amemkumbuka maovu yake…Kwa sababu hiyo mapigo yake yatakuja katika siku moja, mauti, na huzuni, na njaa, naye atateketezwa kabisa kwa moto. Kwa maana Bwana Mungu aliyemuhukumu ni mwenye nguvu

KARIBU KWA MJADALA.
the mad man seems what he sees

by Ned stark

GOT
 
Uliza ndio maana ya mjadala
Unatumia Bible ipi kuhalalisha madai yako. Orthodox ina vitabu 84
Coptic 86
Catholic 72
Protestant 66 .
We umetumia kipi kati ya hivyo na ni kwasababu gani hivyo vitabu vingine havipo kwenye bible nyingine.
 
Back
Top Bottom