Ukweli kuhusu alama ya mnyama inayosemwa kwenye biblia na namba 666

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,907
6,700
Je alama ya mnyama ni nini? Kuna maelezo mengi yaliyotolewa na baadhi ya watu juu ya alama ya mnyama, wengine hudhani kuwa alama ya mnyama ni “chip” ya computa, au kadi, au kitu halisi kinachoweza kubebeka! Lakini Je Biblia inaelezea vipi kuhusu alama ya mnyama? Ngoja tuangalie Mungu anachokisema juu ya alama ya mnyama.

(NB: maneno “alama”, “muhuri”, “ishara” au “dalili” ni visawe).

Ufunuo 13:16-17 “Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa masikini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao; tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.”

Kwanini alama hii ni ya muhimu kuelewa? Kama ukitaka kuthibitisha kwamba kitu flani ni chako, au ukitaka kuonyesha kuwa wewe ni mmiliki wa kitu flani, au ukitaka kutia alama kitu flani kuwa chako, siku zote kutakuwa na vitu vitatu tofauti.

*. Jina lako.

*. Cheo chako.

*. Mahali unapomiliki.

Hivyo, kama mtu akitaka kuthibitisha kwamba kitu flani kimetoka kwake lazima athibitishe kama hivi:

*. Jina = John S Samweli

*. Cheo = Raisi

*. Anapomiliki = Tanzania

Kuna serikali mbinguni (Isa. 9:6), na alama au muhuri wa Mungu ni sheria yake. Angalia katikati ya amri kumi na utaona muhuri wa Mungu, “Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba;…” Kut. 20:11

JINA LAKE = BWANA (“Mimi ni BWANA; ndilo jina langu…” Isa. 42:8).CHEO CHAKE = MUUMBA (…BWANA…yeye aliyeziumba mbingu, na…nchi…” Isa. 42:5).ANAPOMILIKI = MBINGU NA NCHI (“Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya BWANA…” Zab. 24:1).

Hivyo, BWANA alipoziumba mbingu na nchi kwa siku sita, siku ya saba alipumzika ili kuweka alama au muhuri kwamba yeye ndiye aliyeziumba mbingu na nchi, kwa hiyo Sabato ni muhuri unaothibitisha kwamba BWANA:

Aliziumba mbingu na nchi.Alituumba sisi pamoja na vitu vingine vyote.Anamiliki mbingu na nchi, pamoja na vitu vyote vilivyomo.

Kwanini shetani anafanya bidii sana kuwaongoza watu wasiitambue Sabato? Ni kwa sababu shetani anataka kujifanya yeye kuwa kama muumba wa mbingu na nchi, hivyo anainaingiza alama yake ambayo ni kinyume na alama ya kweli ya Mungu. Sabato ni alama au muhuri wa Mungu, kwa hakika Mungu mwenye anathibitisha ukweli huu kwa kusema, “…Hakika mtazishika Sabato zangu, kwa kuwa ni ishara kati ya mimi na ninyi katika vizazi vyenu vyote;…” Kut. 31:13. (Kumbuka! maneno ishara, muhuri, alama ni visawe, na yanaweza kutumika kwa kuyachanganya-changanya).

Njia rahisi na nyepesi ya kugundua alama ya mnyama, ni kutafuta kujua kwanza alama ya Mungu., harafu utaona kwamba alama ya mnyama ni kinyume na alama ya Mungu.

Ufunuo 7:2-3 “Nikaona malaika mwingine, akipanda kutoka mawio ya jua, mwenye mhuri wa Mungu aliye hai; akawapigia kelele kwa sauti kuu wale malaika wanne waliopewa kuidhuru nchi na bahari, akisema, Msiidhuru nchi, wala bahari, wala miti, hata tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu wetu juu ya vipaji vya nyuso zao.”

Kama tulivyoona huko nyuma kwamba muhuri na alama ni visawe! Hivyo watumwa wa Mungu wanawekwa alama katika vipaji vyao vya nyuso, kipaji cha uso hapa humaanisha akili, mawazo, au nia.

Wabrania 10:16 “Hili ni agano nitakaloagana nao baada ya siku zile, anena Bwana, Nitatia sheria zangu mioyoni mwao, Na katika nia zao nitaziandika…”

Pia Wanafisikolojia hutuambia kuwa ubongo wa mbele wa cerebrum [paji la uso] ndipo shughuri kama uamuzi, hukumu, na uhuru wa kutaka vinapofanyikia. Hivyo, Wakristo wanawekwa alama katika vipaji vya nyuso zao, pale tu wanapomkubali Yesu kuwa Mwokozi wao na kutunza amri kumi zote kwa kuhiari, au kutaka wao wenyewe bila kulazimishwa. Hii ndiyo maana muhuri au alama ya Mungu haiwekwi mkononi, kwa sababu Yesu hatawalazimisha watu kumwabudu na kuzitii amri zake. Mkono humaanisha kulazimishwa kufanya kitu furani kinyume na nia zetu.

Jeremia 38:23 “Na watawatoa wake zako, na watoto wako wote, na kuwachukua kwa Wakaldayo; wala wewe hutapona na mikono yao, bali utakamatwa kwa mkono wa mfalme wa Babeli, nawe utakuwa sababu ya kuteketezwa kwa mji huu.”

Yesu kamwe hatatulazimisha sisi kumwabudu, kwani anapendezwa kama tutamwabudu na kutunza sheria zake zote, kwa hiari yetu bila kulazimishwa.

Ufunuo 13:15-17 “Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe. Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao; tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.”

Alama ya mnyama inawekwa katika kipaji cha uso na kwenye mkono. Hivyo wale wote wanaokubali kwa hiari yao wenyewe kumfuata mnyama na kutii amri zake, hawa wamewekwa alama kwenye paji la uso; maana wamehiari wao wenyewe bila kulazimishwa. Na wale wanaopokea alama kwenye mkono, ni wale watakaotii amri za mnyama kwa kulazimishwa bila ridhaa yao. Kwa hofu ya kifo na kushindwa kununua wala kuuza, wanaamua kumtii mnyama ili wasipoteze vitu walivyovifanyia juhudi nyingi katika maisha yao na hili ni bonge la kosa.

Kwa sababu tumeelewa kwamba kuamua kumkubali Yesu kama Mwokozi wetu na kutunza mafundisho na amri zake zote, ni sawa na kupokea alama au muhuri wa Mungu. Tunatakiwa pia tuelewe kuwa kukubali amri, mafundisho, au mapokeo ya kanisa la Romani Katoliki au kanisa lingine lolote linalofuata imani ile ile na kufundisha mapokeo yake, inamaanisha tumepokea alama ya mnyama. Pia elewa kuwa kutakuwa na wengine ambao sio Wakatoliki lakini wanafanya kila kitu ambacho mnyama anaamru kwa kuogopa kufa, au kupoteza mahitaji ya kawaida kwa kuzuiliwa kuuza wala kununua, kitu ambacho kitapelekea kukubali kufuata matakwa ya mnyama. Hawa watapokea alama ya mnyama kwenye mkono kwa sababu wamelazimishwa kinyume na matakwa yao. Wakatoliki na Wakristo wengine ambao hukubali haya “mafundisho ya wanadamu” watakuwa wamepokea alama ya mnyama kwenye vipaji vya nyuso zao kwa sababu wamekubali kwa hiari kuwa kanisa lao liko sawa kwa kubadili maandiko na kuingiza “mapokeo” au “mafundisho ya wanadamu.” Na hii ilionywa katika unabii.

Wakolosai 2:8 “Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na madanganyo matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo.”

Hivyo, kama ukipokea “alama” kwa kuchagua mwenyewe, hii inamaanisha umewekwa alama kwenye kipaji cha uso. Na kama ukipokea “alama” kwa kulazimisha, hii inamaanisha umewekwa alama kenye mkono wa kulia. Lakini kumbuka.

Mathayo 16:25 “Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona.”

Mathayo 10:39 “Wala mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata, hanistahili. Mwenye kuiona nafsi yake ataipoteza; naye mwenye kuipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona.”

Yohana 12:25 “Yeye aipendaye nafsi yake ataiangamiza; naye aichukiaye nafsi yake katika ulimwengu huu ataisalimisha hata uzima wa milele.”

Tukirudi kwenye alama ya mnyama kanisa la Romani Katoliki bila ya kutambua linatimiza unabii huu kwa maelezo yafuatayo.

“Bila shaka kanisa la katoliki hudai kuwa badiliko, (la Sabato Jumamosi kwenda Jumapili) ilikuwa ni kitendo chake…na kitendo hicho ni ALAMA ya mamlaka yake katika mambo ya kidini.” –-H.F. Thomas, Chancellor of Cardinal Gibbons

“Jumapili ni ALAMA yetu ya mamlaka…kanisa liko juu ya Biblia, na uhamishaji huu wa utunzaji wa Sabato ni ushahidi wa jambo hilo la ukweli.” -–Catholic Record of London, Ontario Sept 1, 1923.

Kama unabii uko sawa unaposema jumapili ni alama ya mnyama, na Mungu anasema wazi wazi.

Kutoka 31:13 “…Hakika mtazishika Sabato zangu, kwa kuwa ni ishara kati ya mimi na ninyi katika vizazi vyenu vyote; ili mpate kujua mimi ndimi BWANA niwatakasaye ninyi.”

Ezekieli 20:12, 20 “Tena naliwapa sabato zangu, ziwe ishara kati ya mimi na wao, wapate kujua yakuwa mimi, BWANA, ndimi niwatakasaye…zitakaseni sabato zangu; zitakuwa ishara kati ya mimi na ninyi, mpate kujua yakuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.”
 
Achana na usabato (Dhehebu)
Then, njoo uandike uzi mzuri.

Agano jipya kila siku iendayo kwa Mungu, kwetu ni Sabato.
Tuache unafiki.
Ety usifanye kazi siku ya jumamosi.
Wakati watu ( wa SDA ) wanafanya kazi na kwenda makazini kama kawaida siku ya jumamosi
 
sijaona ukija na hitimisho zuri badala yake umekuja na kejeli za imani za watu tu
 
Achana na usabato (Dhehebu)
Then, njoo uandike uzi mzuri.

Agano jipya kila siku iendayo kwa Mungu, kwetu ni Sabato.
Tuache unafiki.
Ety usifanye kazi siku ya jumamosi.
Wakati watu ( wa SDA ) wanafanya kazi na kwenda makazini kama kawaida siku ya jumamosi
Wadwanzi tu unafiki mwngn wala hauna maana
 
Hii kitu tuliwahi kuijadili hapa jukwaani naona imerudi tena.
 
All in all hivyo vitabu vya iman za kidin ni hadith na stor zilzotungwa na wajanja wachache il wawatawale wajinga wenye kuamin upuuz wao bila kuhoj.

Hizo tabir haztowai kutimia wala kutokea kwakuwa zmebase kwenye uongo..Haya yote tushayazungumzia humu
 
Unapaswa utambue:
Aina ya uandishi uliotumika: Apocalyptic
Mnyama: Uongozi /Kiongozi (Daniel 7)
Maji: Taifa/Kabila/Jamaa/Lugha/jamii
Upepo: Machafuko/Ghasia/Vita.

Muandishi anaandika akiwa Patmo.

Kesho nitaandika machache juu ya ufunuo wa Yohana
 
Unapaswa utambue:
Aina ya uandishi uliotumika: Apocalyptic
Mnyama: Uongozi /Kiongozi (Daniel 7)
Maji: Taifa/Kabila/Jamaa/Lugha/jamii
Upepo: Machafuko/Ghasia/Vita.

Muandishi anaandika akiwa Patmo.

Kesho nitaandika machache juu ya ufunuo wa Yohana
Kwani biblia iliandikwa kwa lugha gani? Wewe uoni unajitafsiria mwenyewe. Weka maneno katika lugha yake ksma ni kiebrania alafu ndio utafsiri. Kama aliyetafsiri kutoka kiebrania alikosea je tafsiri yako itakuwa sahihi?
Kuna doubt nyingi kwenye hiki kitabu by the way
 
Achana na usabato (Dhehebu)
Then, njoo uandike uzi mzuri.

Agano jipya kila siku iendayo kwa Mungu, kwetu ni Sabato.
Tuache unafiki.
Ety usifanye kazi siku ya jumamosi.
Wakati watu ( wa SDA ) wanafanya kazi na kwenda makazini kama kawaida siku ya jumamosi
YESU ALIIZUNGUMZIA SABATO KUWEPO 70 AD NA MWISHO WA DUNIA,

MATHY 24
20 OMBENI, ILI KUKIMBIA KWENU KUSIWE WAKATI WA BARIDI, WALA SIKU YA SABATO.

21 KWA KUWA WAKATI HUO KUTAKUWAPO DHIKI KUBWA, AMBAYO HAIJATOKEA NAMNA YAKE TANGU MWANZO WA ULIMWENGU HATA SASA, WALA HAITAKUWAPO KAMWE.

SASA JE TUKUAMINI WEWE UNAYENUNUA MAFUTA NA MAJI KWA MWAMPOSA AU TUMUAMINI YESU??
1639520455184.png
 
Wadwanzi tu unafiki mwngn wala hauna maana
Wakristo waliokuwa wakiishi Yerusalem, ambako ndipo palikuwa makao makuu ya Kanisa la Kikristo Enzi za Mitume, hadi kufikia katika Mwaka wa 70AD walikuwa wakitunza Sabato kama siku yao ya Ibada.

Katika Kitabu cha Mathayo 24 tunapata unabii wa Yesu juu ya kurudi kwake na dalili za Mwisho wa dunia. Katika aya ya 1-2 Tunapata maelezo haya “Yesu akaenda zake, akatoka hekaluni; wanafunzi wake wakamwendea, ili kumwonyesha majengo ya hekalu. Naye akajibu akawaambia, hamyaoni haya yote? Amin , nawaambieni. Halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa”. Kwa wanafunzi wa Yesu kubomolewa kwa hekalu kungemaanisha mwisho wa dunia, maana kwao kama ilivyokuwa kwa Wayahudi wote, wasingetarajia hekalu hilo kubomolewa. Ndipo wakamuuliza, “tuambie, mambo haya yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya kuja kwako, na ya mwisho wa dunia? Naye Yesu katika kujibu kwake, akawaleza wanafunzi wake mambo ambayo yangejili kuanzia kuangushwa huko kwa hekalu hadi mwisho wa dunia kama walivyohitaji kujua.
 
Achana na usabato (Dhehebu)
Then, njoo uandike uzi mzuri.

Agano jipya kila siku iendayo kwa Mungu, kwetu ni Sabato.
Tuache unafiki.
Ety usifanye kazi siku ya jumamosi.
Wakati watu ( wa SDA ) wanafanya kazi na kwenda makazini kama kawaida siku ya jumamosi
USHAHIDI WA KIHISTORIA KUONYESHA KUWA KANISA LA YERUSALEMU LILIENDELEA KUTUNZA SABATO HATA BAADA YA MWAKA 70AD

Wanahistoria, Eusebius(260-340AD) na Epiphanius(315-403) wanatueleza kuwa hadi kufikia wakati wa uvamizi wa Mfalme Hadrian wa Rumi mwaka 135, (Huu ni uvamizi mwingine tofauti na ule wa Tito katika 70AD) Kanisa la Yerusalemu lilikuwa likiongozwa na Wayahudi walioongoka. Kundi moja la kidini la wayahudi hao walijulikana kama Ebionites, hawa walikuwa washika dini wakisisitiza utunzaji wa amri kumi za Mungu, ikiwemo na Sabato. Wengine ni kundi la Wanazarayo (Nazarenes), ambao nao husisitiza juu ya utunzaji wa amri za Mungu na kuabudu katika siku ya Sabato. Eiphanius anasema “Wanazarayo (Nazarenes) wanawakilisha kanisa la Asili kabisa la Yerusalemu (Tazama ecclesiastic History Vol 3. Pg 23)

Jambo lingine linalotuonyesha kwamba Wakristo wa Yerusalemu waliendelea kutunza Sabato ni “Laana kwa Wakristo” Iliyokuwa ikitolewa na Marabi wa Kiyahudi katika mwaka 80-90AD katika maombi yao ya kila siku. Hii ilikuwa imekusudiwa kuwazuia Wakristo kufaya Ibada zao katika Masinagogi. Hivyo yaonyesha kwamba Wakristo wengi bado Walijihesabu kwamba wao nao ni sehemu ya Wayahudi na hivyokushiriki katika Shughuli na Ibada katika hekalu, ikiwa ni pamoja na kuabudu na Wayahudi hao katika Siku ya Sabato. (Tazama, James Parkers, The Conflict of the Church and the Synagogue uk 78)

Biblia iko wazi kabisa kwamba Wakristo wa zama za Kanisa la Mitume waliabudu pamoja katika Masinagogi katika Siku ya Sabato. (Tanzama Mdo 2:46 na Mdo 13:42-45)

Hadi kufikia hapa tumeonyesha kuwa tokea wakati wa Uumbaji hadi Kanisa la Mitume Sabato haikuwahi kusahaulika kwa watu wa Mungu. Historia inashuhudia kwamba ibada katika Siku ya kwanza haikujulikana kwa Wakristo hadi kufikia katika Karne ya Pili.
 
Wadwanzi tu unafiki mwngn wala hauna maana
mathews 15

7Enyi wanafiki, ni vema alivyotabiri Isaya kwa habari zenu, akisema,
8 Watu hawa huniheshimu kwa midomo;
Ila mioyo yao iko mbali nami.
9Nao waniabudu bure,
Wakifundisha mafundisho
Yaliyo maagizo ya wanadamu

1639523736679.png
 
USABATO ni
Papa
Katoriki
Na
Jumamosi.

Hadi Yesu anarudi atawakuta wanajadiri hayo mambo matatu.

Tubuni dhambi zenu mkabatizwe, ili muurithi ufalme wa mbingu.
 
Ufunuo wa Yohana ni kitabu cha mambo yaliyotokea miaka mingi huko nyuma, kiliandikwa kwa mafumbo ili mwandishi aliogopa kuuwawa na dola la kirumi.

666 ni code name ya mtawala wa dola la kirumi la wakati huo, ukumbuke hata Petro alikatwa kichwa.

Miaka mingi ijayo ijayo watoto wetu hawatajuwa kama Tanzania ilitawaliwa na mtu katili mpaka watu waliogopa kulitaja jina lake na kumuita jiwe.

Hiyo ndio style ya uandishi iliyotumika kuandika kitabu cha Ufunuo.
 
Ni wapi Biblia inasema sabato ni jumamosi? Neno jumamosi liko wapi kwenye Biblia?


Pili sabato ya sasa kila nchi Wana ya kwao kutokana na tofauti Za Masaa. JAPAN SABATO IKIANZA Tanzania inakuwa bado watu wako kazini ! !



Mungu sabato yake ilikuwa time moja dunia nzima


Hawa sabato wa sasa kila mmoja Ana yake
 
Swali Nani aliwapa mamlaka wasabato ya kubadili Muda wa kuanza sabato na kumaliza kuwa tofauti duniani kutokana na time difference.? Japan Wana Muda wao Tanzania wa kwao na marekani wa kwao na uingereza wa kwao nk Mungu Muda wa sabato kaanza na kumaliza ulikuwa ule ule dunia nzima na siku hiyo hiyo moja


Mnashutumu katoliki wakati na nyie mlibadili
Na nyie ni mnyama yule yule 666
 
Back
Top Bottom