Nataka niende Chato nikaiombe msamaha familia ya Hayati Magufuli

Mwizukulu mgikuru

JF-Expert Member
Oct 21, 2021
4,730
11,085
Wakuu mimi ni miongoni mwa vijana wa kitanzania ambao tulijitahidi kuipata elimu huku tukiamini kupata ajira aidha sekta binafsi au serikalini, lakini mambo yakawa tofauti ni miaka saba sasa imepita na wengine tumeshaanza kusahau hata tulichokisomea kwa sababu tuliamua kufanya mambo mengine nje na elimu zetu ili maisha yaende.

Kiukweli alipokufa magufuli mimi nilikuwa ni miongoni mwa vijana waliofurahi sana, nakumbuka siku hiyo walipotangaza kifo cha magufuli mida ya saa sita usiku.

Mimi nilibubujikwa machozi ya furaha nikiamini kuwa sasa na mimi nakwenda kulamba asali, kwa sababu yule aliekuwa anazibana sector binafsi na kubana kutoa ajira serikalini ametangulia kwa hiyo mambo yatakuwa mtelezo.

Sio siri kwa sasa mambo ndio yamekuwa magumu zaidi huwezi kupata kitu mpaka utoe chochote sio tamisemi wala wizarani sio utumishi wala sector binafsi mambo ni magumu zaidi ya jana.
 
Wakuu mimi ni miongoni mwa vijana wa kitanzania ambao tulijitahidi kuipata elimu huku tukiamini kupata ajira aidha sekta binafsi au serikalini, lakini mambo yakawa tofauti...ni miaka saba sasa imepita na wengine tumeshaanza kusahau hata tulichokisomea kwa sababu tuliamua kufanya mambo mengine nje na elimu zetu ili maisha yaende..

Kiukweli alipokufa magufuli mimi nilikuwa ni miongoni mwa vijana waliofurahi sana,,nakumbuka siku hiyo walipotangaza kifo cha magufuli mida ya saa sita usiku. Mimi nilibubujikwa machozi ya furaha nikiamini kuwa sasa na mimi nakwenda kulamba asali, kwa sababu yule aliekuwa anazibana sector binafsi na kubana kutoa ajira serikalini ametangulia kwa hiyo mambo yatakuwa mtelezo....

Sio siri kwa sasa mambo ndio yamekuwa magumu zaidi huwezi kupata kitu mpaka utoe chochote sio tamisemi wala wizarani sio utumishi wala sector binafsi mambo ni magumu zaidi ya jana.
I feel your pain, ajira ni ngumu kwa kweli na hata kujiajiri kwenye mfumo usio rasmi sio rahisi hasa kama huna mtaji....

Endelea kuomba Sana na kutafuta na kutumia vizuri fursa popote inapojitokeza, kuna wakati tu utapata hitaji lakk
 
Man I feel your pain, Tangu JPM atoke hali imekua mbaya sana, niliwai enda mkoani huko Musoma kufatilia maswala flani, enzi za JPM, nilipokelewa kama mgeni rasmi huduma ilikua fasta sana na ndani ya mida mfupi umeondoka na haja zako kutimizwa.

Juzi tu hapa nilikua Musoma, hali ni tofauti tulikaa kumsubiri katibu tawala, akaja ndani ya daka 10 kaenda kwenye kikao baada ya hapo tuka ambiwa tuje kesho, imagine mtu umetoka mbali mfano mimi Mwanza, inabidi niongeze gharama za ziada wakati sikuzipanga.

Bugando tulikua na Mgonjwa pasipo kulipia, mgonjwa asingeli ongezewa damu.

Kipindi kile hatukuwa na haja ya kuwa na matenki, leo maji unayaona ziwani hayo hapo ila nyumbani maji mpaka siku tatu hayapo.

Nimengi sana ila mwisho, vizuri havidumu na mwisho wa siku lazima maisha yanaendelee.

R.I.P JPM.
 
Wakuu mimi ni miongoni mwa vijana wa kitanzania ambao tulijitahidi kuipata elimu huku tukiamini kupata ajira aidha sekta binafsi au serikalini, lakini mambo yakawa tofauti...ni miaka saba sasa imepita na wengine tumeshaanza kusahau h
Ngedere walipojua mwenyeshamba la mahindi waliyokuwa wanaenda kuiba na kula alafu anakuja kuwakimbiza ya kwamba kwasasa kafariki, Ngedere walifurahi saaana na kushangilia kuwa sasa tutakula na kusaza kwasababu aliyekuwa anatukimbiza kafa.

Msimu wa mahindi ulipofika wakaenda kuiba lakini wakashangaa hakuna mahindi limejaa vichaka ndipo walipotambua mwenyeshamba ndo alikuwa mkulima angalau walikuwa wanaambulia kidogo sasa hata hicho kidogo hamna! MTANIKUMBUKA KWA MAZURI@ RIP Magufuli
 
Mwamba yupo wapi
R.I.P Magufuli...

Tulio kiroho tulijua kabla hujawa Rais na Sasa tunajua ulipo...

Hata wanaokulilia tuliwaona...

Hata ungekuwepo tuliona namna ungeiboresha Tanzania...
Mwamba yupo wapi?
Anachomeka au anakula bata?but most possibly like anachomeka but am not surely kama yupo Mbinguni bcoz of mambo fulani fulani ya kiroho zaidi,
Ila marais wote wengine waliobaki ukimtoa magu they are fire wood no matter the name😔😭
Magu am not surely enough but most possibly he is fire wood also🥺
 
Back
Top Bottom