Hayati Magufuli alivyoifilisi familia ya Jamal Malinzi

mdukuzi

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
12,970
24,613
Uchaguzi wa mwaka 2015 ni miongoni mwa chaguzi ngumu kuwahi kutokea nchini ukiacha ule wa 1995. EL alimkaba vilivyo JPM mpaka akakosa usingizi.

Bajeti ya kampeni ya CCM ilipwaya kwa mchaka mchaka ule ikabidi itafutwe njia mbadala ili mambo yaende.

Wafanyabiashara mbalimbali na taasisi mbalimbali wakaombwa kuchangia na kuahidiwa kurudishiwa pesa zao baada ya uchaguzi.

Kama muujiza shirikisho la mpira nchini TFF likapokea bilioni kadhaa sio nyingi sana ili kuendeleza program za michezo nchini. Vigogo wa chama kubwa wakazinusa,kesho yake mbio mpaka ilala karume zilipo ofisi za TFF ,wimbo ukiwa uleule tuazimeni pesa tutarudisha after uchaguzi. Jamal akagoma akiogopa ma auditor wa FIFA endapo wangetua nchini ghafla wakakuta akaunti haina pesa itakuwaje.

Vigogo wakaondoka mikono.mitupu.
Tarehe 28 june 2017 Nissan Patrol nyeupe inatinga viwanja vya karume wanashuka wanaume wanne wanawatia pingu Jamal Malinzi na katibu wake Mwesigwa Celestine na maofisa wengine wawili wa TFF.

Hawakuliona jua mpaka tarehe 10 dec 2019 miaka miwili na nusu,walishtakiwa kwa uhujumu uchumi,utakatishaji fedha,forgery,matumizi mabaya ya fedha na kutia hasara kuasi cha dola 375,418 sawa na milioni 847 wakati huo.

Uchunguzi ulipofanyika ikaonekana hizo pesa zipo au zilifanya kazi ya TFF ila kulikuwa tu na makosa kidogo ya kiuhasibu,kuna nyaraka hazikukamilika na zilihitaji maelezo ili zikamilike.

Bwana mkubwa hakuelewa hilo akasisitiza plea bargain ,pesa zilipwe.si mlikataa kuchangia kampeni.

Akaunti ya Jama Malinzi ikakutwa na Milioni zisizozidi 100. Celestine Mwesigwa milioni 19 Wale maofisa wawili Nsiande mwaya mhasibu ,na karani Flora kwa pamoja walikutwa na milioni kama tano tu kwenye akaunti.

Jamal akataka kuvimba kama mbwai mbwai tu acha nifungwe, Damu nzito kuliko maji,ndugu zake Jamal walikuwa wanajiweza wakachangishana wakalipa plea bargain ifisi ya DPP.Milioni 847

Kesho yake wakaenda mahakamani akapigwa faini ya shilingi laki tano tu na kuachiwa huru. Milioni 847 sio pesa ndogo,baadhi ya biashara za zimekufa kwa kukosa mtaji na zilizobaki zinayumba. Jiulize wewe na familia yako mtauza nni kupata milioni 800 kumtoa ndugu yenu jela.
 

jameson567

Member
Mar 14, 2018
23
726
Muwe mnatumia akili kidogo, uchaguzi wa 2015 ulifanyika tarehe 25 October, na akatangazwa mshindi tarehe 30 October 2015, kwahiyo kutoka November 2015 alipoapishwa JPM hadi June 28 2017, walikuwa wanamuogopa Malinzi wasimkamate?

Vitu vingine kama hamna data muwe mnakaa kimya. Malinzi alifanya ufisadi mkubwa sana, kama unabisha waulize ndugu zake, kwanza jiulize ni ndugu gani wa Malinzi mwenye uwezo wa kutoa milioni 847, Ili kumtoa Malinzi ndani huku nyuma akifilisika?,mtaje hapa maana ndugu zake wanafahamika wote.
 

feyzal

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
6,162
10,511
Muwe mnatumia akili kidogo, uchaguzi wa 2015 ulifanyika tarehe 25 October, na akatangazwa mshindi tarehe 30 October 2015, kwahiyo kutoka November 2015 alipoapishwa JPM hadi June 28 2017, walikuwa wanamuogopa Malinzi wasimkamate?,vitu vingine kama hamna data muwe mnakaa kimya. Malinzi alifanya ufisadi mkubwa sana, kama unabisha waulize ndugu zake, kwanza jiulize ni ndugu gani wa Malinzi mwenye uwezo wa kutoa milioni 847, Ili kumtoa Malinzi ndani huku nyuma akifilisika?,mtaje hapa maana ndugu zake wanafahamika wote.
Jiwe 2015 kuanzia lipoingia madarakani November hadi mwaka wote 2016 kila mtu alisema Yes huyu ndio Rais sana ila ilipofika 2017 akaanza ukatili wa ajabu na roho mbaya isiyo na mfano.
 
74 Reactions
Reply
Top Bottom