Kigwangalla: Rafiki yangu aliyempinga sana hayati Magufuli sasa amkubali, aelekea Chato kuomba radhi kaburini na kuweka maua!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,992
142,010
Anaandika mbunge wa Nzega Vijijini ukurasani X kwamba rafiki yake amekiri " kwa siku 4 mfululizo umeme haujakatika Dar tena una nguvu sana"

Kigwangala anasema rafiki yake huyo aliyempinga Shujaa Magufuli sasa anaelekea Chato kuomba radhi kaburini na kuweka maua

Mjumbe hauwawi 😂😂🔥

----
Anaandika Dakta Hamisi Kigwangalla…

Rafiki yangu mmoja alikuwa critic mkubwa sana wa Rais Magufuli na sera na style yake ya utendaji, anaandika “leo ni siku ya 4 Dar umeme haujakatika na una nguvu sana! ‘Nisamehe Baba! Nitakuja mpaka Chato kutubu kwenye kaburi lako!’ ‘Kwa mara nyingine tena nakuomba msamaha, sitachoka kuomba msamaha!’” Yeye huandika hivi kwa mzaha lakini mimi huiona mantiki kubwa sana iliyojificha ndani ya maneno yake.

Siku za hivi karibuni tumearifiwa kukamilika kwa mradi mkubwa sana wa kuzalisha umeme nchini, na kwamba wameanza kuingiza kwenye grid ya Taifa turbine namba 9 yenye megawatts 235, na siku 18 zijazo wataingiza turbine namba 8 yenye megawatts nyingine 235!

Sidhani kama kumetokea habari kubwa na njema zaidi ya hii katika siku za hivi karibuni, sidhani.

Kabla sijafika mbali, nianze kwa kuwapongeza watu wote walioshiriki kufanikisha mradi huu mkubwa na wa kihistoria. Nitaanza na Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere, aliyeubuni mradi huu miaka ya mwisho ya 60, Rais Kikwete aliyeandika mpango wa pili wa Taifa wa Maendeleo wa miaka mitano uliotupelekea kutekeleza miradi mikubwa ya kielekezo na ya kimkakati kama huu, SGR etc, Rais Magufuli aliyeamua kuivamia miradi mikubwa kama huu na mingineyo kwa nguvu, ari na jeuri kubwa ya kutisha, na Rais Samia kwa ujasiri wa kufunga mkanda na kuziba masikio hadi hii miradi ikamilike! Hayawi hayawi, leo yamekuwa.

Unapowashukuru na kuwapongeza viongozi hawa wakuu, huwezi kujifanya hutambui mchango wa ‘foot soldiers’ na ‘paratroopers’ (washauri na Wasaidizi wao). Iingie kwenye rekodi ninautambua mchango wa kila mtu kwa maana hiyo.

Ndugu zetu wa upinzani walipinga sana utekelezaji wa miradi hii mikubwa wakitoa hoja za kiuchumi zenye mantiki kubwa sana ndani yake. Pengine tungewasikiliza na kufuata ushauri wao tusingefika hapa. Kuna wakati walitoa hoja zilizokuwa zikiletwa kwetu na ‘mabeberu’ kwa njia rasmi, tukawa tunajua tu kuwa baada ya mabeberu kukwama lobbying upande wetu wa serikali, wameamua kupenyeza vitisho kwa wapinzani wetu.

Mbali na hoja za kiuchumi, issues za balance of payment, madhara ya kutumia fedha za ndani kufanya miradi mikubwa kama hii, madhara ya kwenda na mambo mengi makubwa kwa wakati mmoja, madhara ya kununua vitu kama ndege kwa cash n.k. kulikuwa na kikwazo cha kimazingira! Kwamba mradi unaenda kutekelezwa kwenye Selous game reserve, hifadhi ambayo ni ya hadhi ya ‘world heritage site’ (eneo la urithi wa dunia) kwenye orodha ya UNESCO!

UNESCO wakitishia kuiondoa hifadhi hii kwenye hiyo orodha, na suppliers wa hiyo mitambo, wajenzi wasingekubali kufanya kazi na sisi kama mradi wetu ungeleta shida za kimazingira kupelekea kuondolewa hadhi yake ya kwenye orodha ya maeneo ya urithi wa dunia!

Hapa sasa ndiyo zile akili za digrii nne huwa zinahitajika kutumika, siyo kwenye ile mijadala yenu ya hapa twita. Maana hapa watendaji wanatetemeka - huku kuna maslahi ya uhifadhi na matishio ya UNESCO na msimamo mkali dhidi Ya mradi kutoka kwa wabia/wadau wetu, kuwa tusitekeleze mradi wetu, na kule kuna maelekezo yasiyopinda ya Rais wetu chuma kabisa kuwa mradi huu uanze mara moja bila kuangalia makunyanzi! Mimi ndiyo Waziri, kazi yangu kubwa kumshauri Mhe. Rais, natoa ushauri gani?

Nikiwa Waziri, nikaitisha kikao cha Menejimenti ya Wizara, nikawaomba wataalamu wanipitishe kwenye historia ya Selous na hayo mambo ya Maliasili na mashaka ya wabia na wadau wetu wote ni nini haswa?

Kikubwa nilichojifunza pale ni kuwa wabia/wadau wanasema utekelezaji wa mradi utasababisha ikolojia iharibike na hivyo baadhi ya species za flora na fauna ya pale zitapotea. Nikawauliza wasomi: kwani hizo species haziko maeneo mengine humo humo Selous ama hifadhi nyingine? Na je hatuwezi kuchukua sample za species zote za flora na fauna ya pale tukazitunza sehemu nyingine?

Wakaniambia inabidi tukafanye utafiti kwanza

Basi nikamuelekeza KM wangu kwa ushirikiano na wenzake waunde timu ya wataalamu wabobezi kwenye maeneo yote husika wakatafute majibu ya maswali yangu kisayansi. Pili, tuwajibu UNESCO tukiwaomba muda tukamilishe utafiti wetu ndipo tutawapa mrejesho kama watubakishe kwenye orodha yao ama watuondoe tu.

Baada ya utafiti tulikuja kuwajibu wadau/wabia wote kuwa hakutokuwa na upotevu wa species hata moja kwa kuwa miti itakatwa mmoja baada ya mwingine, udongo wa juu (huwa unakuwa na mbegu za viumbe hai) utatolewa kwa layers na kutunzwa pembeni ili baadaye uje urudishwe juu tena na uoto uendelee kama ulivyokuwa kabla ya mradi, mto utabaki kama ulivyo baada ya maji kutumika kuzalisha umeme, mbegu za kila baioanuwai ya pale imechukuliwa na kutunzwa kwenye maabara za mbegu za Taifa, na zaidi ya asilimia 90 ya viumbe vya pale inapatikana kwenye maeneo mengine ya hifadhi hiyo na hifadhi nyingine nk.

Mradi wetu ulipitishwa na wataalamu wa mazingira baada ya kuelezea hatua hizi tulizochukua. Wadau/wabia wetu walipongeza jitihada hizi na kuona kwamba tunatekeleza mradi wetu kwa nia njema kabisa huku tukitanguliza maslahi mapana ya uhifadhi.

Sikuishia hapo tu, nilienda mbele zaidi na kumshauri Mhe. Rais kuwa sasa tubadilishe sehemu ya eneo la Selous kuwa hifadhi ya Taifa ya Nyerere (Nyerere National Park) ili kuimarisha ulinzi na uhifadhi wa baioanuwai, na bwawa tuliite Nyerere na litumike kama kivutio cha utalii. Alikubali.

Kuna zile kenge huwa zinanifuata fuata bado kuhusu sanamu la Baba wa Taifa, ziupate ujumbe kuwa mimi ni mfuasi mahiri na wa kweli wa legacy ya Mwl. Nyerere na nilipokuwa kwenye meza ya maamuzi serikalini sikusita kuutambua mchango na nafasi ya Baba wa Taifa na kulikuza na kulitukuza jina lake kila nilipopata nafasi! Tumebaki wachache wa aina hii.

Kuna tabia ya kusahau haraka sana mchango wa watu kwenye ujenzi wa Taifa hili. Leo tunapofurahia mafanikio ya mradi huu, msitusahau foot soldiers na paratroopers tuliopambana siku za mwanzo. Ujenzi wa Taifa una mchango wa kila mmoja wetu kwa nafasi yake na kwa wakati wake. Kwa Mfano, hata waliotupinga walituamsha akili kujipanga vizuri zaidi. Mfano: tulipendekeza kuanzishwa kwa tozo ya mazingira kwenye kila unit ya umeme unaotokana na maji ili hiyo ikasaidie kuhifadhi mazingira na vyanzo vya maji.

Ukiona vyaelea vimeumbwa! Kuna mengi hapa sikuyasema sababu naamini hayapaswi kusemwa. Lakini, mawaziri vijana wa enzi hizo tulisimama imara kuhakikisha haturudi nyuma bali tunasonga mbele kwa akili kubwa sana. Hatukumuangusha Rais wetu, tulimsaidia kufikia malengo yake. Na tuliweza!

Pamoja na mafanikio haya, bado tuna kazi kubwa ya kufanya kwenye nishati. Umeme wa nyuklia, umeme wa Joto ardhi, umeme wa makaa ya mawe, umeme wa jua, umeme wa upepo na umeme wa gesi bado unahitajika kuendelea kuongezwa kwenye vyanzo vyetu. Tusije tukarudi gizani tena. Lazima tutambue kuwa kuna kazi kubwa zaidi ya kuendelea kuvilinda vyanzo vya mito yetu ili maji yasipungue kama ilivyotokea siku za hivi karibuni.

Maeneo yaliyohifadhiwa yana muunganiko wa kiikolojia mkubwa sana, hivyo athari kwenye eneo moja ni athari kwenye jingine. Kabla ya kuyaachia maeneo ya hifadhi, ama kuyashusha hadhi (kama kwa Kigosi) ifanywe tathmini ya kina sana. #HK #Fighter #NjeYaBox Pic: 75% ya watu wasio na umeme wa uhakika wapo Africa.
 
Hivi ina maana ule mgao wa umeme uliokuwepo usingeisha kama pasingekuwepo na bwawa la Nyerere?

Kwamba umeme wote uliokuwepo kabla ya ule mgao ulienda wapi? Ina maana ule mgao uliokuwepo ulikuwa ni "exceptional" sana zaidi ya migao mingine yote iliyowahi kuwepo miaka ya nyuma?

Kuna clip moja niliona Magufuli amerekediwa akisema; "iko siku wakiamua watachukua umeme wao" naona kwa ule mgao ndio wajanja waliamua kuchukua umeme wao!.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Ungeishaje?

Kwa kuleta tena Richmond?!!
Mbona sasa hawakusema ukweli, wakawa wanatudanganya tu mara upungufu wa maji kwenye mabwawa, mara uchakavu wa mitambo, ajabu mitambo yenyewe si ndio hii hii leo siku ya nne umeme haujakatika?! tunaongozwa na serikali ya kitapeli sana.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Anaandika mbunge wa Nzega Vijijini ukurasani X kwamba rafiki yake amekiri " kwa siku 4 mfululizo umeme haujakatika Dar tena una nguvu sana"

Kigwangala anasema rafiki yake huyo aliyempinga Shujaa Magufuli sasa anaelekea Chato kuomba radhi kaburini na kuweka maua

Mjumbe hauwawi 😂😂🔥
R.I.P CHUMAJPM!watasema tu wote waliokua wanakupinga mwamba!!
 
Back
Top Bottom