Yegomasika
JF-Expert Member
- Mar 21, 2009
- 13,164
- 61,277
Huyo jamaa anakosa Financial Intelligence. Na hilo siyo tatizo lake bali linatokana na ukweli kuwa shule zetu hazifundishi watu kutengeneza pesa. Watu wanafundishwa kutafuta ajira.
Milioni 1 ni hela nyingi sana kwa mtu anayeziona fursa kutumia jicho la ndani. Vilevile anaweza kwenda Australia na akalipwa hayo mahela lakini akaishia kukatwa kodi na kulipa house rent.
Lazima tujue kufanikiwa siyo kulipwa mshahara mkubwa ila kuwa na kipato kinachozidi expenses zako na kuwa na muda wa kutosha wa kupumzika. Mtu unaenda kuajiriwa ulaya halafu unafanyishwa kazi masaa 20 kwa siku halafu unajiona uko salama.
Tatizo sisi wabongo wavivu sana, halafu hili suala la rent za apartment tunalikuza sana, kwa mfano Marekani, State nyingi za Midwest mbona unaweza kupata a one room apartment kwa $400 ambayo kama unafanya kazi ni hela ya kawaida tu. Na hiyo ndio itakuwa Bill yako pekee ambayo ni kubwa, umeme hata $100 haifiki kwa mwezi, maji apartment nyingi hulipiii. Au labda watu mnachanganya rent ya apartment na mortgage ya nyumba. Suala la kufanyishwa kazi 20hrs mi sijawahi kuliona, hakuna mwajiri atakayekulazimisha kufanya kazi 20hrs, ukiona mtu amefanya 10-12hrs a day huyo lazima ametaka mwenyewe ili kuongezea kipato, ameombwa na akakubali!. Na analipwa Kama overtime, Kama mtu amekwenda kutafuta hayo masaa 10 mbona kawaida tu. Tatizo letu sisi ni uvivu!.