Nataka kupenda kama mjinga, nizame nipotee!

Nataka kupenda kama mjinga, nizame nipotee!

Hayo yote ulioyataja Ngoja yakupate Tu!! Utarudi hapa hapa Jf ukimwaga chozi kuomba msaada.

Ndugu yangu Mkenya, inatakiwa kwenye maisha uhesabu your wins and losses, not the times you failed to try. Let me try I my fail or succeed!
 
pole sana tafuta pesa kwanza ndio upende achana na papuchi bhana japo sijajua kama wewe ni me au ke.

Ni Me if it matters, pesa hazina mwisho wa kutafuta, lazima na maisha mengine yaendelee mkuu.
 
nisije sema mimi yani naweza omba game

ahahahaa, yalaah, mpaka akupe hati ya nyumba ya babu yake, akiyanani wanawake wa mujini, ni wamujini tu, unapewa game mpaka unasahau jina lako la kuzaliwa memory ime shift ukimuuliza unaitwa nan baba anabaki aaaa mm naitwa nan vile, mara anataja jina lako badala ya lake, hahaahaha lol
 
Mapenzi ya hivo matamu mpotee wote kwnye msito wa mapenzi, mzame kina kirefu kwnye dimbwi la mahabba, akuite baba umuite mama, mcheke wote mlie wote, upo nae karibu na bado unam miss, ukimpa busu shavuni hamu haiishi, ukimuaga asubuhi unaenda kazini unampa hugs ukifika getini unarudi tena unam hug tena na tena, ukifika kazini unampigia ushamkumbuka, nae analia nimeku mc rudi haraka, ndani nyumbani unambeba mwanamke hatakiwi kutembea chini, akienda jikoni unambeba, akishamaliza kupika anataka kwenda sebuleni unaenda unambeba unampeleka.

usijali wako wanawake wengi wa hivo, ukimpata we zamia tu, hisia hizo ni tamu sana, halafu ukishampata nimpe mdogo wake tuzamie wote wa 4 mzee.

Mapenzi ya kweli duniani yapo. mm naamini Mungu akiumba roho anaumba ya wawili, mmoja anmtupa mashariki mwingine magharibi, ukivumilia anawakutanisha mnapendana mnazikana, ukiona umeumizwa ujue huyo hakupangiwa kuwa wako, mtafute mwenye roho yako.

This is lovely mkuu! shida tu machozi sipatagi, ningeyatiririsha kabisa mkuu
 
  • Thanks
Reactions: HMS
ahahahaa, yalaah, mpaka akupe hati ya nyumba ya babu yake, akiyanani wanawake wa mujini, ni wamujini tu, unapewa game mpaka unasahau jina lako la kuzaliwa memory ime shift ukimuuliza unaitwa nan baba anabaki aaaa mm naitwa nan vile, mara anataja jina lako badala ya lake, hahaahaha lol

Mmmh nipe hela sitaki nyumba
 
This is lovely mkuu! shida tu machozi sipatagi, ningeyatiririsha kabisa mkuu

Watu hawajui kitu kimoja mkuu, mwanamke ana mapenzi ya kweli kabisa, ni wanaume ndo matatizo, hamna mwanamke asiekua na story yake ya penzi la dhati, hata kahaba aliekubuu lazima kuna siku alimpenda mwanaume kwa dhati kabla ya kuwa vile, wanawake wanasaliti kutokana na kuchoshwa na wanaume, unakuta kaumizwa yaani kalia sn mpaka machozi hayatoki tena anabaki kutoa sauti tu, sasa akishaamua kusonga mbele humpati tena, na wanasaliti maana wanajua wanaume ni waongo, hata akikupenda utamuumiza tu, lakini mwanamke akipata mwanaume akampa penzi la kweli kama la kwako, kamwe hakuachi, anabadilika kabisa anatulia kama sio yeye. Boss ukipata wa kukupoteza, we potea nae tu mbele ya safari, ya mbeleni anaejua ni Mungu tu, tena ukimpa penzi hilo nakwambia atapotea zaidi yako.
 
Mmmh nipe hela sitaki nyumba

Unauza nyumba unapata hela. akikupa hela sana sana itakua laki, milioni, moja mbili 3. Lakini nyumba imekaa masaki mkuu, kitu million 900, unasubiri nn? lol
 
Samahani mkuu, sikujua kuna marufuku kutafuta mpenzi hapa. I am truly sorry kwa kukukwaza

[MENTION]Boliver[/MENTION] ni kwamba, unafunguka tu. Jamani natafuta mtu. Hujanikwaza mkuu :A S wink: . Mimi ndio nimekukwaza
 
Boliver ni kwamba, unafunguka tu. Jamani natafuta mtu. Hujanikwaza mkuu :A S wink: . Mimi ndio nimekukwaza

That would be too straight for me, one has to be a bit tricky. I understand though kama hukubaliani na style yangu.
 
dahh namtamani huyo...ila anahelaa? Ntampenda na mimi hadi achanganyikiwe zaidi ya anavyowish
 
dahh namtamani huyo...ila anahelaa? Ntampenda na mimi hadi achanganyikiwe zaidi ya anavyowish

Sasa hapo ndio mnakosea, hata kama lengo lako la kuingia kwenye mahusiano ni maslahi ya kipesa, usiseme wazi wazi. Nidanganye danganye bhanaaa kuwa unanipenda kiukweli na hupendi pesa zangu,
 
Sasa hapo ndio mnakosea, hata kama lengo lako la kuingia kwenye mahusiano ni maslahi ya kipesa, usiseme wazi wazi. Nidanganye danganye bhanaaa kuwa unanipenda kiukweli na hupendi pesa zangu,

Ahhh kuwa fake sitaki...Bora na wewe nikuambie kweli ili tupendane hadi tuchanganyikiwe sote....Me kuwa ktk ......huku nawaza sijala, oohh nadaiwa, oohh sina Lotion Stress nakuwa sijisikii, sipati hisia.....

Km upo tayari kunitimizia mahitaji yangu utachanganyikiwa...Na pesa tambua si kuwa mtu angiongelea pesa ni Za kuweza kununua Hummer ....Zakukidhi mahitaji ya mwanamke...(Nguo, mapambo, kula, Basic needs)

Kuna mwanaume anakuambia anakupenda ila kutunza mwanamke hawezi wala hajui...Hapo inapelekea wewe kumsaliti kwani atatunziwa na wenziwe
 
Kuna Bibi mmoja aliniambia: Unapokuwa unaanza mahusiano na mwanaume Usiwe fake: Wanawake walio wengi utakuta wanapokuwa wachumba atajidae ye anajua kupika, yeye ni mtu wa Mungu, yeye ni mkarimu, hata mawifi kwake ni mkarimu..kumbe si tabia yake....

Siku akiolewa kama ilivyo tabia ambayo hujaizoea haidumu...Tabia zinakuja badilika ugomvi unaanza... Ni bora kuwa mkweli from the beginning uzoeleke mwanaume akujue we ni mtu wa aina gani km mkewe mtaraji hapendi kufua au kupika nk.

Me napenda kutunzwa
 
Interesting! sio shida kumtunza mwanamke, niliogopa nikadhani pesa ya kununua private jet!
Going back, hujawahi kutamani kujitunza mwenyewe? Kujisimamia? Kuweza kukidhi mahitaji yako mwenyewe? You know that independence has some form of attraction!
 
kama uko serious unataka ufurahie mapenzi,mpende kwanza MUNGU kwa style hiyo unayosema.Yani wewe ukisikia mambo ya MUNGU akili yako inaruka kabisaaa.

Then utakae mpata atakupenda na wewe utampenda na mtafurahiana.
Tafuteni kwanza ufalme wa MUNGU na hayo mengine yote mtazidishiwa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom