Nataka kuoa Mpare kutoka Same, msaada kwa wanaojua tabia zao

Nataka kuoa Mpare kutoka Same, msaada kwa wanaojua tabia zao

Status
Not open for further replies.

bid2015

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2011
Posts
306
Reaction score
59
Mimi ni kijana ambaye nataka kuoa, kwetu ni Kigoma.

Nataka kuoa binti wa kipare. Naomba msaada wa kuwajua kiundani zaidi tabia zao.

Naomba kuwasilisha wanabodi wenzangu.

Mchango:
Ndugu yangu mbona mnawahukumu sana hawa watu jamani.......Mimi sio mpare ila naomba nitetee hapa........kuhusu tabia, hizi ni tabia tu ndugu yangu ambazo mtu wa kabila yoyote ulimwengu huu anaweza kuwa nazo. Mimi nimeshawahi kuishi na wapare na kuna ndugu yangu ameoa mwanamke wa kipare na wanaishi vizuri tu.......yani mama wa watu mpole na ni mkarimu kweli.

Jamani hivi ni kabila gani dunia hii ambalo ni 100% perfect kuliko makabila mengine? Tusiwe namna hii jamani........hizi tabia ni hulka tu ya mtu mwenyewe na sio kabila maalum.

Sasa hapo kwenye RED hapo......Aisee!!! watu wa ulimwengu huu bwana.......... yaani bila aibu unasema kabisa wanawake wa kipare ni wahuni, ila wewe kutembea na wake za watu ina maana wewe sio muhuni, si ndivyo.

Dah!!!...Ashakun si matusi........Kweli Wahenga waliposema nyani haoni kundule hawakukosea.
 
Ukioa mpare umeoa ukoo mzima.dada kaka mjomba na nk hawatakosekana nyumbani.wageni kutoka paris(aka pare)hapo ndo patakuwa pa kufikia wakija kutafuta maisha

Lakini tabia hii si ya wapare pekee na hata hivyo hawafanani kwa tabia inakuwaje kama huyo binti kazaliwa mjini na amekulia mjini ndugu zake asilimia kubwa wapo mjini hapa inakuwaje na yeye atahamishia nduguze kwake hizo ni tabia za watu wa makabila tofauti haijalishi mparis (mpare) wala nani.
 
Wamefundwa sana hasa katika sekta ya unyagoni.....si unaelewa kwani we ni mtoto mdogo
 
mimi ni kijana ambaye nataka kuoa kwetu ni kigoma sasa nataka kuoa binti wa kipare naomba msaada wa kuwajua kiundani zaidi tabia zao......! naomba kuwasilisha wana bodi wenzangu.

Heshima zenu wana JF wote, na wadogo marhabaa!!!.

Yaani BID2015 unanichekesha SIFA ZOOOTE ZA MKE ANAZO LAKINI AHH! MPARE? Usinikumbushe maneno ya Mwalimu ( J.K Nyerere).

Muhimu kuangalia sifa na sio kabila, Karne ya 21 hii. Bado mmeng`ang`ania makabilaaa mpaka leo.

Nawasilisha Waungwana.:happy:
 
mimi ni kijana ambaye nataka kuoa kwetu ni kigoma sasa nataka kuoa binti wa kipare naomba msaada wa kuwajua kiundani zaidi tabia zao......! naomba kuwasilisha wana bodi wenzangu.

hebu fanya uchunguzi wako kwanza! Tabia za mabinti wa kitanzani kwa sasa,zinafanana maana wengi wao wamezaliwa vijijini na wanakulia mjini!wanasomea vijijini wanaajiriwa mjini! Kwa hiyo kuhusu tabia yake/zao mi naona ni kazi kwa sasa kuwajua!!
 
we oa tu bana...za kuambiwa changanya na zako
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom