Nataka kujenga, nina laki 5 mkononi

Nataka kujenga, nina laki 5 mkononi

Nimenunua tofali 400 nimebakiwa na laki 5 natafuta mtu mwenye akili nyingi aniambie jinsi ntakavyokamilisha hata chumba kimoja na kuhamia ikibidi kabaki kachenchi hata elfu 5.
Pia nina mifuko 10 ya cement na mchanga wakutosha Karibuni
Hiyo pesa ni nyingi mno, nunua bati kama sita, afu tumia fundi unayemlipa kwa siku elf 10 na kibarua 5, utatumia siku 4. Tengeneza mlango na madrisha ya bati hamia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hivi wabongo tumedanganywa na nani maendeleo ni kujenga tu,mbona wahindi wengi ni matajiri na wana biashara kubwakubwa tu lakini wanaishi nyumba za NHC.kajitu kamepata hela ya kubadilisha mboga kanataka kajenge chuma kama choo ili aonekane nae kajenga mi nilidhani utaomba ushauri wa biashara gani ufanye ili ukuze mtaje baadae utumie profit kujiendeleza hatimae ujenge ukiwa umerelux .akili ya kukremishwa mbaya sana
Mkuu kodi inaumiza aisee asikwambie mtu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nenda jimboni kwa ****** chukua dizaini ya zile nyumba za wapiga kura wa jimbo lile, kisha njoo na ramani yake, Jenga, uzinduzi ****** na lusinde bila kumsahau kubwa nyenye le mobimba!
 
Chumba kimoja tofari 200@ 700 mlango wa bati 7000
 
Jenga hadi utapoishia. Kisha vuta subira ukipata tena pesa hata laki 1.5 mwite fundi aendeleze. Hivyo hivyo utatoboa. Ktk ujenzi hata ukijenga tofali 100 ni hatua kubwa. Na ukiwa waona mjengo (kuta nusu nusu), utapata hamasa ya kuendelea tena na tena. Mwisho tahamaki umemaliza boma.
Shukrani kwa niaba yake... Sio wote wanatumia akili Humu.
 
Nimenunua tofali 400 nimebakiwa na laki 5 natafuta mtu mwenye akili nyingi aniambie jinsi ntakavyokamilisha hata chumba kimoja na kuhamia ikibidi kabaki kachenchi hata elfu 5.
Pia nina mifuko 10 ya cement na mchanga wakutosha Karibuni
Unatukaribisha kujenga au?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nunua tu vitu visivyoharibika kama matofali , musumari na mabati halafu piga tena misele ya hapa na pale mwisho urafanikiwa kama kweli una nia . Kuna mwanamke alijenga nyumba kwa kuuza maandazi , ni nia na juhudi , step by step

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo letu kubwa sana ni kuishi kwa kukariri pamoja na mazoea.

Jirani yangu ninaepakana nae uwanja mwaka ulioisha ilikuwa kila akija kucheck uwanja wake anabaki kunung'unika tu, siku nikamuuliza - jirani kunani unanung'unika tu kila wakati ukicheck eneo lako? Akanijibu anawaza atajengaje na hali ya uchumi ni ngumu.

Nikaingia ndani nikachuku tape measure nikamwambia shika tape tuanze vipimo, tukapima pembeni ya uwanja wake tukaweka alama pamoja na kuchimba mashimo, tulipomaliza nikamwambia hivi nenda kanunue;

-milunda (miti ya kujengea)idadi kadhaa

-misumari

-mabati used + reject

-mbao chache

-polythene sheeting's ( maturubai ya nailon yale kanda ya ziwa wanayaita makavelo

Akaondoka baada wiki akaja navyo, tumejenga boonge moja la banda kubwa hlf zuri la kisasa pale tukaweka na mlango wa bati.

Tulipomaliza nikamwambia acha usharobaro wa kijinga maisha sio lelemama ukitaka kuporomosha mahekelu kama hayo unayoyaona sharti uwe na cash vinginevyo utaishia kukonda tu. Alihamishia vifaa vyake yupo kwenye banda lake anaishi vizuri hadaiwi kodi wala chokochoko za mwenye nyumba.

Hivi sasa ameshamaliza kujenga msingi na kuta za nyumba ya vyumba viwili na jiko na sebule anajipanga kumimina linta.

Hao wanaokukatisha tamaa wana hela zao ukiwasikiliza sana na kufuata ushauri wao unazidi kupotea. Kwako ni kwako tu hata paweje.

Kwa tofali ulizo nazo na mifuko ya saruji na mchanga na kiasi cha kuanzia ulichonacho ukikaa chini ukatafakari kwa kina sana ukaumiza akili ujenga na utahamia kisha utaendeleza kutoka pale utakapoishia.

Tafakari na chukua hatua
 
Saf sana mkuu kwa ushauri na wengine ni kula kulala bure tu ooh wahindi wana ela lakini wamepanga wale hawawezi jenga apa sababu sio kwao wale wageni na wanahofia usalama wao.
 
tafuta fundi njaa mwenye kuweza ujenzi mmoja tu nawe unakua msaidizi wake chimba nae msingi wa chumba kimoja na sebule au kuuchimba hata peke ako unaweza kupunguza gharma, kama eneo ni la mfinyazi itapunguza gharma ya msingi bado kokoto bado nondo kadhaa isikupe tabu unaenda hardwea ya karibu unannunua zile za kupima ktk viroba siwezi wwka bei kwa maana sina uzoefu wa bei mpka msingi unaisha na layer ya zege na coz moja pande kadhaa a utakua umebaki na nauli tu na tofali kumi pembeni kajivute tena
ukirudiii njoo na tofali walau mia sita njoo na katipa ka mchanga kama visiment vilibaki aya Kumbuka usiangaikie choo kama msela ukitoka zako baa ukakunyaz uko uko unaoga utakapo pajua wewe tofaut na hapo unachimba ka shimo wewe peke ako u akazungushia mabati usid cha tempo

Sent using Jamii Forums mobile app
Nmecheka sn
 
Back
Top Bottom