Nataka kujenga, nina laki 5 mkononi

Nataka kujenga, nina laki 5 mkononi

Muite fundi njaa akupimie msingi wa room moja. Then chimba mwenyewe. Baada ya hapo patana naye ujenzi wewe uwe saidia fundi. Lenta weka usawa wa madirisha na milango tu. Tafuta mirunda iliyonyooka ufanye mbao za kupaulia na mabati nunua reject. Unganisha mbao zilizotumika wakati wa kufunga lenta upate mlango au nunua mlango uliokwishatumika. Dirishani ziba kwa tofali huku ukiacha nafasi kati ya tofali na tofali kwa ajili ya kuingiza hewa. Mpaka hapo utakuwa baba/ mama mwenye nyumba.
 
Ndugu inaitaji moyo sana sana sana na ikikupendeza husijenge, hiyo pesa kaizungushe ndani ya miaka 3 tu! Utajenga kwa raha zako kwa sasa ukthubutu hhhhhaaaaaa Dunia utakuja kiujua vizuri na kuikumbuka laki tano yako
NB. kama ni zaidi ya 40years mkuu fanya kujenga unavyojua.

bugs
 
tafuta fundi njaa mwenye kuweza ujenzi mmoja tu nawe unakua msaidizi wake chimba nae msingi wa chumba kimoja na sebule au kuuchimba hata peke ako unaweza kupunguza gharma, kama eneo ni la mfinyazi itapunguza gharma ya msingi bado kokoto bado nondo kadhaa isikupe tabu unaenda hardwea ya karibu unannunua zile za kupima ktk viroba siwezi wwka bei kwa maana sina uzoefu wa bei mpka msingi unaisha na layer ya zege na coz moja pande kadhaa a utakua umebaki na nauli tu na tofali kumi pembeni kajivute tena
ukirudiii njoo na tofali walau mia sita njoo na katipa ka mchanga kama visiment vilibaki aya Kumbuka usiangaikie choo kama msela ukitoka zako baa ukakunyaz uko uko unaoga utakapo pajua wewe tofaut na hapo unachimba ka shimo wewe peke ako u akazungushia mabati usid cha tempo

Sent using Jamii Forums mobile app
mwamba umetisha sana kweli penye nia pana njia
 
Mkuu, hongera sana!
Usiwasikilize hawa MABEBERU wanaokukatisha tamaa.
Hiyo ni hatua kubwa sana kwenye ujenzi. Anza kujenga msingi wa nyumba ya vyumba vitatu. Hata kama ni kozi mbili mbili, utakuwa unaziongeza taratibu. Then ukipata hela unaanza kupandisha chumba kimoja kimoja. Mpaka kufika Dec mwaka huu, utakuwa umepiga hatua kubwa.
 
Nimenunua tofali 400 nimebakiwa na laki 5 natafuta mtu mwenye akili nyingi aniambie jinsi ntakavyokamilisha hata chumba kimoja na kuhamia ikibidi kabaki kachenchi hata elfu 5.
Pia nina mifuko 10 ya cement na mchanga wakutosha Karibuni
Kama hii avatar ni yako kweli, minifundi ujenzi ntajenga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimenunua tofali 400 nimebakiwa na laki 5 natafuta mtu mwenye akili nyingi aniambie jinsi ntakavyokamilisha hata chumba kimoja na kuhamia ikibidi kabaki kachenchi hata elfu 5.
Pia nina mifuko 10 ya cement na mchanga wakutosha Karibuni
Mkuu nimebaki najiuliza unamaanisha 5M au ni laki 5?hautoboi hata ukienda kwa mbana matumizi mzuri, mbao, bati, mifuko hiyo ya cement haitoshi kabisa, nondo, gharama za fundi, mawe, kokoto we jamaa hivi upo serious kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo laki tano unaweza kujenga Mbezi beach mkuu. Nyumba kubwa yenye mpaka Swiming pool na change ukanunua boat la kuvulia samaki nadhani limefika laki na nusu.
Hhahahaha, hii ni hatari sanaaa na sweeming pool pia?
 
Yaani nimecheka sana comment za wadau humu.. eti uza tofali ujenge nyumba ya tope! Ila kama nimemuelewa vizuri jamaa ni kuwa baada ya kununua baadhi ya vitu alivyotaja amebakiwa na laki tano. Hii haimaanishi kwamba anategemea kujenga nyumba nzima kwa kutumia hiyo laki tano, ila anataka pa kuanzia. Ushauri wangu ni kuwa kwavile tayari ana tofali, mchanga na cement yeye angetafuta fundi waelewane ni kipi kinaweza kufanyika kwa hiyo hela iliyopo mpaka itakapoishia jamaa atajipanga upya. Lakini sio kuacha na kuinywea pombe hiyo kilo tano.
 
tafuta fundi njaa mwenye kuweza ujenzi mmoja tu nawe unakua msaidizi wake chimba nae msingi wa chumba kimoja na sebule au kuuchimba hata peke ako unaweza kupunguza gharma, kama eneo ni la mfinyazi itapunguza gharma ya msingi bado kokoto bado nondo kadhaa isikupe tabu unaenda hardwea ya karibu unannunua zile za kupima ktk viroba siwezi wwka bei kwa maana sina uzoefu wa bei mpka msingi unaisha na layer ya zege na coz moja pande kadhaa a utakua umebaki na nauli tu na tofali kumi pembeni kajivute tena
ukirudiii njoo na tofali walau mia sita njoo na katipa ka mchanga kama visiment vilibaki aya Kumbuka usiangaikie choo kama msela ukitoka zako baa ukakunyaz uko uko unaoga utakapo pajua wewe tofaut na hapo unachimba ka shimo wewe peke ako u akazungushia mabati usid cha tempo

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa kuongezea katika kujisaidia uwe unajisaidia usiku mwingi sana
 
Jenga msingi tu tena wa chumba kimoja ila kama inawezekana tafuta matofali mengine 400 ujenge msingi wa vyumba viwili na subule ili simenti isiaribike maana mvua zinakuja ila kwa laki5 huwezi jenga nyumba yoyote labda chumba cha kujistiri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usivunjike moyo, tafuta fundi atakaekubaliana na wewe japo umlipe nusu nusu. Tofali 400 unaweza kujenga chumba kimoja na kukamilika

"ᵂᵒʳʳʸ ⁱˢ ᵃ ʷᵒʳᵈ ᵗʰᵃᵗ ᴵ ᵈᵒⁿᵗ ᵃˡˡᵒʷ ᵐʸˢᵉˡᶠ ᵗᵒ ᵘˢᵉ"
 
Inawezekana . Mtafute fundi ambae ni rafiki yako kabisa alafu
Mwambie kwa sasa sina pesa ila utampa elfu hamsini 50000
Lakini utamlisha chakula
Kibarua wa kuchanganya udongo na kusogeza tofari utakuwa wewe mwenyewe
Nunua mchanga wa laki moja na nusu
Nunua cement
Na kokoto
Anzeni kazi
Hivi nyie watu huwa mnasoma uzi wote au kichwa cha habari tu then mnatiririka? Amani iwe kwako ndugu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kujenga kila siku hakuhitaji speed kama uwezo wako ni mdogo. Usiwe na haraka ya kutaka kuwa na nyumba pasipo kuzingatia viwango na ubora wa ujenzi. Hiyo pesa unaweza ukafanya jambo moja ktk hatua za ujenzi. Jambo lenyewe kama kuanda msingi bora wa chumba hicho kimoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo pesa nenda ka bet, kutupa hela kwenye udongo inauma zaidi kama utashindwa kumaliza hiyo project
 
Nimenunua tofali 400 nimebakiwa na laki 5 natafuta mtu mwenye akili nyingi aniambie jinsi ntakavyokamilisha hata chumba kimoja na kuhamia ikibidi kabaki kachenchi hata elfu 5.
Pia nina mifuko 10 ya cement na mchanga wakutosha Karibuni
Mafundi wengi wanajenga tofali moja sh.200 kwahiyo 400 x 200 = 80,000
Hivyo fundi waweza kumpa 120,000 akaanza kukujengea kuanzia msingi hadi kukumalizia chumba kimoja. Kuwa na moyo then epuka matumizi yasiyo na msingi ufikie malengo.

"ᵂᵒʳʳʸ ⁱˢ ᵃ ʷᵒʳᵈ ᵗʰᵃᵗ ᴵ ᵈᵒⁿᵗ ᵃˡˡᵒʷ ᵐʸˢᵉˡᶠ ᵗᵒ ᵘˢᵉ"
 
Nimenunua tofali 400 nimebakiwa na laki 5 natafuta mtu mwenye akili nyingi aniambie jinsi ntakavyokamilisha hata chumba kimoja na kuhamia ikibidi kabaki kachenchi hata elfu 5.
Pia nina mifuko 10 ya cement na mchanga wakutosha Karibuni
Jenga
 
Back
Top Bottom