Fahamu mambo mbalimbali kuhusu Kilimo cha Korosho

Hili wazo nalikubali na nimelifanyia kazi, shamba limeanza kuonesha matumaini japo changamoto ni nyingi
HABARI,
"fungafunga,

Amen,Usirudi nyuma hata kama ukikutana na shauri nyingine mamuzi yako ni yako ni heri kufeli kwa maamuzi yako kwa kuwa utajifunza ila sio ya mwingine songa mbele. Samahani sikukuuliza shamba lako liko wapi.

LUMUMBA
 
UTANGULIZI
Korosho ni zao la biashara ambalo chimbuko lake ni Ureno na baadae mnamo karne ya 16 ndipo lilipofika Afrika, katika nchi ya mozamboque na baadae likafika Kenya na Tanzania.

Tanzania zao la korosho ulimwa na kustawi vizuri katika pwani yote ya bahari ya Hindi kuanzia Mtwara mpaka Tanga, pia ipo mikoa mipya kamaTabora, Singida, Dodoma, Songwe, Rukwa huko kote zao la korosho linastawi vizuri
mvua na Udongo.

Korosho hustawi vizuri kwenye maeneo yenye mvua 840mm - 1250 mm wastani wa mvua kwa mwaka, na pia hukua vizuri kwenye maeneo 0- 500 m kutoka usawa wa bahari.

Kutokana na kwamba samadi sehemu nyingi ni adimu, mbolea za viwandani zinafaa kutumika katika kupandia, husaidia kukuza haraka japo ukipanda bila mbolea miti inaota na utavuna kama kawaida ila tofauti ya kutumia mbolea husaidia kukua kwa haraka.

Mikorosho haihitaji maji kilasiku ukuaji hautakuwa mzuri ,kwa kipindi cha kiangazi umwagiliaji mzuri ni ndoo ya lita kumi kwa kila shimo kwa wiki moja inatosha sana,ila kama utakuwa una miche iliyofikia upana wa peni na ukapanda kipindi cha mvua na mche ukapata mvua kwa miezi 4-5 inatosha sana kuendelea kukua wenyewe.

Pia kama ni kipindi cha kiangazi unaweza kuzungushia mche na majani makavu kwa kuhifadhi unyevu. Korosho hukua vizuri kwenye maeneo yenye PH 5.6 udongo wa kichanga (sandy) na pia udongo mfinyazi kichanga.

MAANDALIZI YA SHAMBA
Korosho kama mazao mengine shamba linatakiwa kusafishwa, kusawazishwa nakutifuliwa vizuri kwaajili ya kupanda korosho.

Katika mashimo utakayo chimba unaweza kuweka mbolea ya ngombe ukachanganya na udongo mapema ili kuongeza rutuba.

2242735_IMG-20191201-WA0082.jpeg

JINSI YA KUPANDA
Ni muhimu sana kuchagua mbegu bora kwakua mbegu utakayoipanda ndio itakuonyesha kiasi gani utavuna,
Baada ya kununua mbegu unachukua maji na chumvi 100g ya chumvi unaweka katika maji kiasi cha lita 5 unakoroga vizuri na unachukua mbegu zako unaweka kwenye maji hayo zile zitakazo zama ndio mbegu zenye uwezekano mkubwa wa kiota.

Kitaalamu hekari moja inatakiwa ichukue miche 25-27 ambapo ni space ya mita 12 urefu na 12 upana kwa mbegu za kienyeji. Kwa kilimo cha kisasa nikimaanisha mbegu bora za kisasa na kwa mpango wa upandaji bila kuchanganya na mazao mengine hekari moja inakaa mpaka miti 100 na mkorosho uliostawi vizuri unatoa kuanzia kilo 10-20.

Kwa hiyo unauhakika wa kuvuna kuanzia tani moja ya korosho kila heka ambayao tani moja sio chini ya milioni 3
Mikorosho ile ya kubebesha ya muda mfupi inaanza kutoa Korosho kuanzia miaka mitatu, Huwa wanasema miaka miwili au mmoja ni kweli ila unakuwa hauna nguvu, unashauriwa kutoa mau yote ili uweze kutengeneza matawi na kuwa na nguvu.

AINA ZA UPANDAJI MBEGU
Kupanda moja kwa moja. Hii ni njia mambayo ni hatarishi sana na inaitaji umakini kwa sababu kuna uwezekano mkubwa wa mbegu kufa. ukitumia njia hii unatakiwa kupanda mbegu tatu 3 katika shimo moja na baada ya miezi mi 3 - 4 ng’oa mimea na bakiza mmoja wenye afya na muonekano mzuri.

Njia ya kitaru
Hii ni njia ya pili na ni nzuri kwa sababu unakua huru kuchagua mche ambao umestawi na ulio na muonekano mzuri , unatakiwa kuamishia miche shambani ikiwa na umri wa wiki 6 na zingatia kuchagua mche wenye afya na baadae unatakiwa kupunguza majani urefu wa sm60- 90 kutoka kwenye ardhi na pia ondoa majani yote ambayo yanaonekana kuadhiliwa na magonjwa au wadudu.

MAGONJWA NA WADUDU

MAGONJWA

  • Anthracnose
  • Powdery mildew
Hayo ni baadhi ya magonjwa yanayo athiri sana korosho

WADUDU
  • Cashew stem girdler
  • Cashew weevil
  • Coconut bug
  • Heliotropes bug
KUZUIA NA TIBA
  • Ili kuweza kuzuia maagonjwa na wadudu unatakiwa kuzingatia yafuatayo:
  • Palilia mapema
  • Weka shamba katika hali ya usafi
  • Tumia mbinu ya kuchanganya mazao kwa korosho unaweza kuchanya pamba au maharagwe hiyo inasaidia kukimbiza wadudu wengine ambao wanakua hawapatani na mazao hayo
  • Tumia pesticide kutibu magonjwa na insecticide kuuwa wadudu wahalibifu.
Uwekezaji
Wengi wananunua mashamba yenye mikorosho then wanaindeleza kwa kupanda niche mipya,ambapo ikianza kuzaa kwa wingi ndipo hukata ya zamani.Ila kipindi hiki kuuziwa shamba la mikorosho ni shughuli ni sawa na kuuza kitalu cha madini.

images-1.jpeg
 
Asante kwa andiko zuri. Ila ningetamani kufahamu zaidi.. huo mkorosho uliostawi vizuri wenye kutoa kilo 10 hadi 20 unakuwa na umri wa miaka mingapi?
 
Asante kwa andiko zuri. Ila ningetamani kufahamu zaidi.. huo mkorosho uliostawi vizuri wenye kutoa kilo 10 hadi 20 unakuwa na umri wa miaka mingapi?
mkorosho huanza kuzaa vizuri kuanzia miaka 2½ hadi mitatu kupata kilo 10 inategemea na aina ya mbegu lakini hizo kilo 10 ni pale unapochanganya kuzaa vizuri yani miaka 3 hadi 4 na kadri umri unavyo ongezeka basi mapato yanaongezeka.
 
Vipi kuhusu spacing kwa mbegu za kisasa ambazo hutoa miti 100?

Sijui kama ulisoma vizuri hichi kipengele

Kitaalamu hekari moja inatakiwa ichukue miche 25-27 ambapo ni space ya mita 12 urefu na 12 upana kwa mbegu za kienyeji. Kwa kilimo cha kisasa nikimaanisha mbegu bora za kisasa na kwa mpango wa upandaji bila kuchanganya na mazao mengine hekari moja inakaa mpaka miti 100
 
Nimekuelewa vizuri. Ila swali linakuja kwamba niweke space ngapi mti na mti ili nipate miti 100 kwa mbegu za kisasa?

Mbegu za kisasa miti yake haiwi mikubwa na matawi makubwa yaliyochanua kama yakienyeji, unashauliwa kuweka space sawa na ya kienyeji faida zake ni hizi:-

1. Mikorosho itakuwa na nafasi ya kutosha hii itakusaidia kupalilia na kumwaga dawa kirahisi kwa kila mti.
2. Kufwatilia maendeleo ya mti husika bila kujichanganya(mwingiliano)
3. Wakati wa kuvuna pia inakurahisishia jinsi kuhamisha mazao kutakuwa hakuna msongamano.
4. Kwakuwa ipo mbalimbali basi si rahisi kuambukizana magonjwa ikitokea mkorosho mmoja umevamiwa na magonjwa.
 
Kwa uelewa wangu mdogo, suala la nafasi kati ya mti na mti lina mambo mengi sana ya kuangalia kabla hujaamua kufuata ushauri wa wataalamu.

Wataalamu wa chuo cha maendeleo ya korosho pale naliendele mtwara wanasisitiza umbali kati ya mti na mti kuwa mita 12 na mstari na mstari pia kuwa mita 12.

Ukifuata utaratibu huu, utaona katika ekari moja unapa miche 25 mpaka 27.

Ila kiuhalisia, na kwakuzingatia majanga mengine yanayoendelea katika mashamba yetu kati ya kipindi ambacho mkorosho umepandwa mpaka kuanza uzalishaji yaani wadudu, magonjwa, wanyama waharibifu, ukame, mvua zilizozidi kipimo, majanga ya moto n.k, unaweza ukakuta unaishia kuwa na miche michache sana katika ekari moja.

Na kama msemaji mmoja alivyosema hapo juu, mikorosho ya sasa haitanuki saaaana kiasi cha kuanza kugusana katika umri mdogo wa miaka 3 mpaka mi5. Mimi nimepanda miche 45 mpaka 50 kwa ekari moja kwakuwa sipandi mazao mengine shambani kwangu. So far inakwenda vizuri sana na ninaamini ntavuna kwa miaka kadhaa kabla sijaanza kuipunguza ile ntakayoona inaanza kugusana.

Changamoto mashambani ni nyingi ila akili za kujiongeza pia zinaruhusiwa.. siyo kila kitu ni vitabu tu..
 
Back
Top Bottom