Natafuta wasambazaji wa kijarida cha bure! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Natafuta wasambazaji wa kijarida cha bure!

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Mzee Mwanakijiji, Aug 10, 2008.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Aug 10, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Natafuta wasambazaji wa kijarida cha bure walioko Tanzania TU!! Mpango uliopo sasa ni kuwa kijarida hicho cha kutoka kwenye mtandao kitakuwa katika PDF file. Unachotakiwa kufanya (mchango wako) ni hivi:

  Ya kujua:

  - Kijarida kitakuwa na kurasa nne kama ukichapisha upande mmoja na kurasa mbili kama unachapisha mbele na nyuma.
  - Kijarida kitakuwa na maoni/hoja nzito, habari, mambo ya mtandaoni (kama kutoka JF) na burudani, pamoja na habari za kiingiereza in brief.
  - Kijarida ni cha bure kabisa kwa msomaji. Nitaingia gharama zote za kutengeneza.
  - Hakuna matangazo yoyote ya biashara na hakifungamani na itikadi, siasa, au mtazamo wowote wa kisiasa au dini.
  - Kina lengo la kuwafanya Watanzania wabadili fikra zao na kuweza kuona kuwa na wao wanastahili vilivyo vyema, wanaweza makuu, na wanawajibika kuyaleta wale wanayoyatamania.


  Unachotakiwa kufanya:

  1. Tuma email yako kwa mhariri@klhnews.com
  2. Katika email yako weka simu yako na nitazungumza nawe ili kuondoa namna yoyote ile ya kuvamiwa na mafisadi. Hutaki kuweka simu yako, usitume email.
  Maelekezo mengine ya marketing utayapata kwenye email.

  Kama huna lengo/nia/Uwezo wa kusambaza usitume email.


  Our Motto: "Moto mkubwa huanzishwa kwa Cheche".....
   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Bravo mmkjj
  B blessed
   
 3. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #3
  Aug 10, 2008
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,815
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Mzalendo Mwanakijiji;

  Asante sana, hili ni jambo la maana sana, kubadilisha mitazamo "Attitude Change".

  Tunashukuru sana kwa kuunga mkono jitihada za kubadili ziwe za mtazamo wa kimaendeleo zaidi. Tukiwa na anuani za barua pepe zaidi ya 1000, hakika TPN inakuunga mkono.

  Hongera sana Village Man!
   
 4. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #4
  Aug 11, 2008
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mwana Kijiji,
  Nakubaliana na wee kwa hili kwa asilimia nyingi sana. Nilishaandika hata mie huko nyuma kuwa Tanzania tunahitaji kiongozi mwenye sifa moja kati ya hizi chini ingawa akipatikana mwenye zote mbili na anajua jinsi ya kuzibalance hizi zote mbili itakuwa poa sana sana :-
  1. Awe dictator
  2. Abadili MAWAZO ya watu (Bob Marley alisema Jikwamueni kutoka utumwa wa akili).
  Naona wewe umeanza kusaidia watu moja kwa moja kwa hili la pili. Nafikiri hiyo ndiyo inaitwa kuwapa watu NDOANO badaya ya SAMAKI. Hii ni SILAHA kali kuzidi hata Atomic bomb. Hii ndiyo WANASIASA wote huwa wanaiogopa zaidi ya upinzani wowote.
  BRAVOOOOO!! Na kweli UBARIKIWE.
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Aug 11, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Natafuta wasambazaji!! au ndio maneno matupu ya mabadiliko na kupinga ufisadi tu lakini kwenye vitendo ni watupu? nawashukuru mnaotoa pongezi, lakini kwa kweli ninachotafuta ni watu hizi pongezi zije baada ya kufanikiwa. Hadi hivi sasa ni mtu mmoja tu yuko tayari toka Bukoba!!
   
 6. W

  WembeMkali JF-Expert Member

  #6
  Aug 11, 2008
  Joined: Jun 16, 2007
  Messages: 282
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ewaaa...nasikia harufu ya mapinduzi! malalamishi,maneno matupu tu hayatoshi,inabidi tuanze vitendo..Tusisubiri Chadema au TLP au another socialist party! Tuanze mara moja vita dhidi ya mafisadi na ukombozi wa nchi yetu.

  Tuko ukurasa mmoja kwa hili mkuu...good idea.!!

  Sasa mkuu mimi nipo Ukraine kitovu cha mapinduzi! nitakutumia mchango wangu.


  Wembe.
   
 7. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #7
  Aug 11, 2008
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,815
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Mkuu, umecheck PM yako?
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Aug 11, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Sanctus nimekupata vizuri mzee nitakujibu.

  Thanks
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Aug 11, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hadi sasa tumepata watu 10 walio tayari kushiriki katika usambazaji. Lakini wengi bado wako Dar, nahitaji maeneo ya mikoani vile vile. Kitu ambacho mtu anahitaji ni vitu viwili.

  a. Uwe na email na access ya internet angalau mara moja kwa wiki hapo Tanzania.
  b. Uwe tayari kutoa nakala angalau 10 kwa wiki na kuzisambaza bure.

  Nimepata ofa ya mmoja wa wasambazaji wakubwa Dar hivyo kwa jiji la Dar, ukiondoa wasambazaji wadogo wadogo hivyo, tunahitaji mtu ambaye ana uwezo wa kutoa nakala nyingine (zinachapwa katika letter size paper) ambaye yuko tayari kutoa nakala na kumpatia msambazaji.
   
 10. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #10
  Aug 11, 2008
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Bravoo!
  Movement for "Attitude Change" Lakini kusiwe na Element za kisiasa, unajua watu tayari wamelishwa sumu mbaya kuhusiana na Siasa, kwa hiyo hii movement iwe ya kijamii (social) zaidi. hata wakitoa Photocopy ya kawaida inatosha.
   
 11. W

  WembeMkali JF-Expert Member

  #11
  Aug 11, 2008
  Joined: Jun 16, 2007
  Messages: 282
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Suala hapa ni education kwanza.Inabidi kuwaelimisha wananchi kuwa umasikini wao haujaletwa na mungu na kuwa Tanzania ni nchi tajiri kwa maliasili na kama tutazitumia vizuri basi tunaweza kabisa kuondokana na umasikini wetu.
  Na kwamba ufisadi,uongozi mbovu,kulindana, rushwa,uzembe,kuogopa kufanya maamuzi mazito na ya busara kwa taifa letu etc ndiyo hasa misingi mikuu ya umasikini wetu.
  Kwa hiyo baada ya hapo wananchi watakuwa hold accountable kwa kura zao watakazozipiga kwa viongozi wabovu na mafisadi.

  Wembe.
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Aug 11, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  nakupata vizuri kabisa; tatizo moja la siasa ni kuwa ni sehemu ya maisha ya jamii nzima. Ni vigumu kuangalia masuala mengine ya jumuiya pasipo kuingiza siasa. Uzuri wa kijarida hicho (nikisema hivyo mwenyewe) ni kuwa kina lengo la kumfanya mtu afiikiri na kuuliza maswali; na zaidi hayo yeye mwenyewe kutafuta majibu.

  Siyo mahali pa indocrination..
   
 13. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #13
  Aug 12, 2008
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Ni kweli labda tuseme tunavyoanza tusionyeshe tupo biased, kwanza anayemtawala Mtanzania sasa hivi ni Mwanasiasa Fisadi. Nilianzisha Movement huko wilayani Makete ya kupambana na mafisadi wa Hlamshauri na Pesa za UKIMWI tulifanikiwa sana. Na nimekuwa na wazo kama hili la kuanzisha kijalida kwa miaka 3 sasa nilishindwa kwa kukosa resources. Bahati mbaya nimesafiri lakini nitawasiliana na wapiganaji wenzangu huko wagawe hicho kijalida.

  Naattach design ya Kijalida chetu. (the layout is copy right protected), Tulikuwa tumekidesign katika pdf, Word na Publisher. Mkuu songa mbele! Daima Mbele
   

  Attached Files:

 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Aug 12, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nimependa hiyo sana Mbogela. Ninachohitaji pia ni habari kutoka sehemu mbalimbali.
   
 15. Mongoiwe

  Mongoiwe JF-Expert Member

  #15
  Aug 12, 2008
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 521
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Nimekiona nami pia nakupa Big up lakini ili wa huko Makete pia wakisome nadhani tumia pia Lugha ya Taifa (Kiswahili) ili nao wakisome kwani nimeona kipo katika Lugha moja tu ambayo nadhani wengi hasa ambao ni walengwa wanapaswa kubadilishwa wanaweza kushindwa soma na ujumbe usifike.
   
 16. t

  think BIG JF-Expert Member

  #16
  Aug 12, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 236
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Mkuu Mbogela,

  Kijarida kiko juu! Ila hiyo lugha sijui ni ya wapi (kama ni lugha ya asili), ni vizuri mkachanganya lugha, kuwe na lugha ya asili (kwa ajili ya wenyeji) pamoja na kiswahili (kwa ajili ya wahamiaji), ili kuwaelimisha wakazi wote wa wilaya hiyo ya Makete.
   
 17. t

  think BIG JF-Expert Member

  #17
  Aug 12, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 236
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Mkuu MMKJJ,

  Wazo zuri sana! Huko Wilayani kuna habari nyingi sana (za kimaendeleo na hata zile zinazokwamisha maendeleo yao), lakini wanakosa nafasi ya "kupashana"! Ukifanikiwa katika hilo basi halitaitwa kijarida bali Jarida! I wish you all the best!
   
 18. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #18
  Aug 12, 2008
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Asante sana wakuu. Hiyo lugha ni lugha ya kudesign tu, ni mchanganyiko wa herufi mbali mbali randomly wala haipo duniani popote ni lugha ya kifundi kutengenezea lay out za majarida. Mawasiliano ni kuwa katika Lugha rahisi sana, ambayo kila mwanchi ataielewa. Titles niliweka kwa kizungu kwa sababu tulitegemea kuombea pesa za uzalishaji kwa wanotaka plan za miradi kwa kizungu.

  Wananchi wanasupport kubwa sana wakikuelewa. Kesi 12 za watuhumiwa wa ufisadi wa Halmashauri zipo mahakamani, Tulisababisha mabadiliko makubwa ndani ya kanisa Dayosisi ya Makete (KKKT) Askofu alitolewa kabla ya kipindi kuisha, kwa ujumla nilipewa support. Ingawaje nimekamatwa na kuwekwa ndani, nimekatiwa umeme, maji n.k Yawapasa wanaojua kweli kuteseka ili walio wengi waijue hiyo kweli, maana nayo hiyo kweli itawaweka huru!
   
 19. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #19
  Aug 13, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135

  Typo.
  *indoctrination - The indoctrinated person is expected not to question or critically examine the doctrine they have learned.  Signature ya Mtu wa Pwani inasema:
  Our job is not to make up anybody's mind, but to open minds and to make the agony of the decision-making so intense you can escape only by thinking. ~Author Unknown
  Kutengeneza ni pamoja na kufanya printing?


  • Unatarajia kusambaza copy ngapi kwa kipindi?
  • Ni makundi yapi unategemea yatakuunga mkono?
  • Je, utafanya jitihada kuzishirikisha asasi za kijamii kwa mfano?


  Mwelekeo uliouchagua naaunga mkono sana, binafsi nitajishirikisha na usambazaji wa majarida na vitu kama CD, DVD bure, mfano open source software n.k. Hili nitafanya baadae kidogo, sio sasa.  .
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  Aug 13, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
   
Loading...