Hatufanyi Printing kama yanavyofanya magazeti kwamba kuna central printing. Printers ni wasambazaji wenyewe.
- Unatarajia kusambaza copy ngapi kwa kipindi?
Kwa sasa sijui kwani kila msambazaji atatoa copy kwa kadiri ya uwezo wake, ila isiwe chini ya 10 kwa kila toleo.
Kwa kweli sitegemei kuungwa mkono na kundi lolote isipokuwa mtu mmoja mmoja.
- Ni makundi yapi unategemea yatakuunga mkono?
- Je, utafanya jitihada kuzishirikisha asasi za kijamii kwa mfano?
Hapana kwa kweli, asasi za kijamii zina majukumu yake na shughuli zake. Ila wao wakitaka kusambaza kijarida wako huru kusambaza kwa kadiri wapendavyo na kama wana habari ambazo wanataka zitoke tuko tayari kuzipokea. Lakini hakutakuwa na formal arrangement ya ushirikiano wa namna hiyo.
Msambazaji anawezaje kupata credit kwa zoezi hili. Ukiacha swala la gharama, ipo risk ya kuswekwa ndani.
'Benjamin. G. Mwalukasa' (and klhnews) will get the most credits obviously and he is likely to use this fame for financial gain in the future, should he wish to do so.
Msambazaji anawezaje kupata walau recognition kwa kazi hii ya kujitolea? (Recognition kutoka kwa msomaji) - Someone is being used here, don't you think?
.
mnazungumzia kama credit gani? hivi wanaosambaza vipeperushi vyote vya bure wanapewa credit gani? jamani, kama mtu hawezi asifanye. Haya mapambano hamna kubembelezana wala kupigiana magoti. Unaona huwezi kusambaza bure kwa kujitolea kama waandishi wanavyoandika bure na kwa kujitolea, DON'T DO IT.
Ni kwa sababu hiyo kwa wakati huu hatuweki wala hatukubali matangazo yoyote ya biashara. Lakini tutakuletea habari za kina, maoni huru kabisa, na kwa wakati muafaka. Unachoweza kufanya ambacho ni kidogo ni kusambaza. Huwezi kaa pembeni. Credits haziendi kwa mtu yeyote isipokuwa timu nzima ya Cheche, masupporters wake, na wasambazaji. Lakini zaidi ni wasomaji ambao wanakingojea kila Jumanne.
Shukrani.