The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,503
- 2,046
Kama mada inavyojieleza hapo juu na kama waswahili wasemavyo wa kushiba huonekana mezani, awamu hii tofauti sana na hali ilivyokuwa kuelekea uchaguzi wa mwaka 2015, sijaona viashiria vingi muhimu vinavyotoa matumaini ya ccm kuanguka katika uchaguzi unaokuja.
Mwaka 2015 kulikuwa na vuguvugu kubwa sana la kisiasa kiwango cha kushawishi hata baadhi ya waliopata kuwa mawaziri katika serikali ya ccm kuhamia upinzani.
Mbali na hiyo hama hama Toka chama tawala kwenda ccm iliyojulikana kama kimbunga Kila Kona ya nchi kulikuwa na mijadala mingi sana iliyokuwa na mwelekeo wa kuichoka ccm na kuuchoka ufisadi uliokithiri miongoni mwa watawala.
Zaidi ya hayo hata chaguzi ndogo zilizoitishwa kipindi hicho ziliipa wakati mgumu sana ccm hata kama walishinda iliwalazimu kushinda Kwa mbinde sana.
Oparesheni zilizofanywa na wapinzani zilikuwa na mguso na mvuto mkubwa sana Kwa wananchi, hali ni tofauti sana awamu hii, mambo yako baridi sana. Unaweza uliza hata watanzania kumi kati yao asitokee hata mmoja anaejua hali ya vuguvugu la kisiasa nchini.
Zaidi sana mwamko mkubwa wa kisiasa umeibukia kwenye dpw vinginevyo hali kisiasa ingepooza zaidi.