Natafuta kazi, maji yamenifika shingoni

Natafuta kazi, maji yamenifika shingoni

Upo kwenye hatua ya kukua na kuvuka daraja mkuu. Haya mawazo ni dalili za kukomaa na kuingia hatua nyingine. Suluhu utakayoipata hapa itakua ya kudumu na utaisimamia ipasavyo.

Nimependa ulivyomuwazi na kuweka waka bayana kwamba msaada unaohitaji sio ajira pekee bali hata mawazo.

1. Tafuta kitabu kidogo sana kinaitwa The Richest Man in Babylon. Kisome, wana toleo la kiswahili pia.

2. Kuanzia mwezi ujao, watafute wadeni wako wote. Waambie hautaweza kuwalipa kiwango chote wanachokudai na utawalipa kidogo kidogo. Najua watacharuka na kukukatisha tamaa wengine watakudhalilusha lakini simamia hapo hapo ilimradi umaanishe kuwalipa kila mwezi.

3. Mshahara wako ukiupata, weka 10% kama akiba, najua utanitukana kimoyo moyo kwamba hapo tu hautoshi itakuaje ubakishe ziada ya kuweka akiba? Mshahara siku zote hautoshi. Hata ulipwe kiasi gani. Dhamiria kujilipa kwanza wewe hiyo asilimia kumi.

4. Baada ya kupunguza madeni na kuanza kuhifadhi hiyo akiba, tafuta mradi wife afanye mtaji ukiwa asilimia kumi uliyohifadhi.

Hii itakujengea msingi imara na nidhamu ya pesa.

Baadhi ya kauli za wanachama zisikukatishe tamaa. Tunatofauriana tabia, malezi, elimu n.k

Kikubwa usikate tamaa. Hii ni hatua ya kukuimarisha tu.
Hebu toa summary kidogo ya hicho kitabu just in briefly richest man in Babylon
 
Hebu toa summary kidogo ya hicho kitabu just in briefly richest man in Babylon

Kinasisitiza kanuni za pesa. Zipo rahisi sana. Msingi mkubwa ni kujiwekea akiba kwa kujilipa kwanza asilimia kumi ya kila unachokipata.

Ni mafunzo yaliyotolewa kwa mfumo wa hadithi lakini msingi upo kwenye tabia za kuikuza na kuilea pesa.
 
Mwenzako ana familia wewe una familia ya kuitunza, msilinganishe mnachopokea, linganisha majukumu
Sikuungi mkono familia imemfata sikaitengeneza mwenyewe hata uyo unayesema hana familia anaweza kuwa na familia ila muulize kwaninj hana mpaka sasahi hata mimi sina familia ila tukizungumza mambo ya maisha au pesa usiingize hoja za wewe unafamilia mimi sina.

Familia jukumu analoliingia mtu mwenyewe kabla ya kuliingia angalia hali yako.
 
Mshirikishe mkeo msaidiane, wewe utafute naye atafute sio akae tu kusubiri wewe ufanye kila kitu. Mfungulie hata mradi wa kutengeneza vitafunio, au genge, au chochote utakachoona kinafaa.
Kweli kabisa, hata juice tena kama upo Dar matunda bei rahisi tu
 
Back
Top Bottom