Natafuta kazi, maji yamenifika shingoni

Natafuta kazi, maji yamenifika shingoni

Ndugu yangu nafanya kazi kwenye kampuni ya ulinzi. Mshahara baada ya makato unafikia 230,000/= kweli kidogo cha halali lakini kwa maisha ya dar es salaam huku nina familia inayonitegemea, inanipa mawazo sana. hapo hapo kodi, usafiri wa kunifikisha kazini, bado kazini sijala...na nyumbani hiyo hiyo ndio tunayoitegemea. Nawaza hadi nachanganyikiwa
Nawaza tu kwa akili zangu ndogo. Hivi ukiamua mkeo ukamuanzishia biashara ya kuuza matunda uwe na madeli madogo matatu, meza moja ndogo akawa anachukua mzigo wa ndizi za kuiva, tikit anakata vipande, nanasi ananunua mawili anakata vipande vipande, pembeni anauza sigara, hataweza mkishauriana hivyo?

Hivi vitu ni vidogo na vya kipumbavu ila vinauzika sana. Na mtaji wake wa kianzio kwa mpambanaji anaweza kuumudu.
 
Nawaza tu kwa akili zangu ndogo. Hivi ukiamua mkeo ukamuanzishia biashara ya kuuza matunda uwe na madeli madogo matatu, meza moja ndogo akawa anachukua mzigo wa ndizi za kuiva, tikit anakata vipande, nanasi ananunua mawili anakata vipande vipande, pembeni anauza sigara, hataweza mkishauriana hivyo?

Hivi vitu ni vidogo na vya kipumbavu ila vinauzika sana. Na mtaji wake wa kianzio kwa mpambanaji anaweza kuumudu

Nawaza kufanya hivyo ila kwa kazi ninayo ifanya mshahala huwa unaisha kabla sijaupata, sijui nakosea wapi mimi
 
Kuna rafiki yangu anafanyakazi mbili. Usiku nimlinzi na mchana anafanyakazi kweny maghala kubeba mizigo. Maisha yanaenda vizuri tu

kama kuna connection ndugu yangu naomba unisaidie...walau ata nifanye kazi mbili kwa wakati mmoja...nahisi nitachanganyikiwa
 
Kuna rafiki yangu anafanyakazi mbili. Usiku nimlinzi na mchana anafanyakazi kweny maghala kubeba mizigo. Maisha yanaenda vizuri tu
NAOMBA CONNECTION NAE ANAWEZA AKANISAIDIA....maji yamezidi unga kaka nisaidie
 
Ilikua ni kukupa moyo kwamba tafutacha kufanya cha ziada, kama kariakoo au wapi kuna gari zinapakia na kushusha mizigo unga juhudi. Usitegemee kupata kazi ya pili ya mshahara wa mwezi tena itakutesa hutaweza kufanya sehemu zote mbili

Pia ongea na shemeji yetu, auze hata mihogo tu akiongeza 1000 kama faida ya biashara yake kila siku kweny kipato cha kaya maisha yanasogea sana. Siyo sawa na kukaa tu na hela ingekua inatoka tuu na vitafunwa tena mnanunua.
 
nilikuwa na wazo kama hilo...ila mshahala...ni wa madeni tu...!

Banana nao upate pesa kidogo mkeo aanze hata kupika maandazi ya kilo moja tu! Usiwaze kushindwa, waza kufanikiwa, waza kujikwamua. Issue ya ajira ni ngumu.
 
Usawa huu waajiri wengi naona wamesitisha ajira, cha kufanya ndugu jitahidi kumaliza madeni na kata bajeti yako.
Kama unapoishi kodi ni kubwa sana nenda sehemu nyingine ambapo itakua nafuu.

Kwa kipato chako usiendekeze kula nje... Jitahidi uwe unakula vya kutosha nyumbani. Mzee wangu alikua anafanya hivyo na sio kwa sababu hakua na hela ila alijijengea tu hiyo tabia baada ya kuona hela nyingi inatumika kununua vyakula akiwa kazini. Utazoea tu.

Ukipata mshahara, nunua yale mahitaji muhimu ya ndani... Mf. Unga wa sembe, ngano, mchele, mafuta, dagaa, maharage.

Cha muhimu zaidi, Ongea na mkeo aanze biashara. Apike vitafunio asubuhi (skonzi, maandazi, mihogo etc.) Chochote kile... Hamtakosa vihela vya mboga. Pia afungue genge. Kama mtaji mdogo atembeze vitu vya genge ata kwenye beseni. Afanye chochote ili msaidiane.

Hakikisha unatunza vihela na huvigusi ata kidogo kwa ajili ya dharura kama ugonjwa. Yaani ata ukiweka 50 kila mwezi unaweza shangaa n mshahara huo huo unaanza kujenga.

Kuna mtu kazungumzia tenda za kubeba mizigo n.k jaribu na huko ujiongezee kipato wakati unaendelea kutafuta hiyo kazi ya kuajiriwa nyingine.

Kila la kheri mkuu!
Tusichoke kupambana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom