Natafuta kazi, maji yamenifika shingoni

Natafuta kazi, maji yamenifika shingoni

Usawa huu waajiri wengi naona wamesitisha ajira, cha kufanya ndugu jitahidi kumaliza madeni na kata bajeti yako.
Kama unapoishi kodi ni kubwa sana nenda sehemu nyingine ambapo itakua nafuu.

Kwa kipato chako usiendekeze kula nje. Jitahidi uwe unakula vya kutosha nyumbani. Mzee wangu alikua anafanya hivyo na sio kwa sababu hakua na hela ila alijijengea tu hiyo tabia baada ya kuona hela nyingi inatumika kununua vyakula akiwa kazini. Utazoea tu.

Ukipata mshahara, nunua yale mahitaji muhimu ya ndani... Mf. Unga wa sembe, ngano, mchele, mafuta, dagaa, maharage.

Cha muhimu zaidi... Ongea na mkeo aanze biashara. Apike vitafunio asubuhi (skonzi, maandazi, mihogo etc.) Chochote kile... Hamtakosa vihela vya mboga. Pia afungue genge... Kama mtaji mdogo atembeze vitu vya genge ata kwenye beseni. Afanye chochote ili msaidiane.

Hakikisha unatunza vihela na huvigusi ata kidogo kwa ajili ya dharura kama ugonjwa. Yaani ata ukiweka 50 kila mwezi unaweza shangaa n mshahara huo huo unaanza kujenga.

Kuna mtu kazungumzia tenda za kubeba mizigo n.k jaribu na huko ujiongezee kipato wakati unaendelea kutafuta hiyo kazi ya kuajiriwa nyingine.

Kila la kheri mkuu!
Tusichoke kupambana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Asanate. Nnimesoma post yako hadi chozi limenitoka. Kuna baadhi ya mambo umezungumza as if unanifahamu. Asante sana rafiki yangu, nitayafanyia kazi hayo!
 
Nawaza kufanya hivyo ila kwa kazi ninayo ifanya mshahala huwa unaisha kabla sijaupata. Sijui nakosea wapi, mimi
Fanya kwa mwezi huo unaofuata, usilipe deni lolote mfungulie mkeo biashara ndogo...pia kwa hiyo taaluma yako ya uandishi wa habari huwezi kuandika andika hata makala za kichambuzi ukauzia vhombo vya habari?
 
Fanya kwa mwezi huo unaofuata, usilipe deni lolote mfungulie mkeo biashara ndogo. Pia kwa hiyo taaluma yako ya uandishi wa habari huwezi kuandika andika hata makala za kichambuzi ukauzia vhombo vya habari?

Tatizo ni jinsi ya kupata connection ya pakupeleka hizo habari ila kwa kuandika naandika sana.
angalia baadhi ya post zangu.

1. Ardhi imejaa inatapika matapishi ya damu
2. Joseph Senga umempelekea salamu Mwangosi?
3. Utata mauaji ya Mwangosi na hukumu yake
4. Oscar Pistorius Ni umaarufu, pesa, huruma au sheria?
5. Jamii ilivyoshindwa kumsaidia Christopher Alex Masawe
6. Kauli ya Mwalimu Nyerere ilivyowahi kumponza Tundu Lissu
7. Karim Seleman 'Chiba' akielezea mkasa wake ulipelekea akatwe mguu
8. Kesi ya Ditopile, Mramba, Yona na Babu Seya, nani alaumiwe hakimu au mpelelezi?
 
Mkuu iyo kazi acha nipe mimi..wewe una kazi afu unalalamika? Aise dah...!!
 
Ndugu yangu, nafanya kazi kwenye kampuni ya ulinzi. Mshahara baada ya makato unafikia 230,000/= kweli kidogo cha halali lakini kwa maisha ya Dar es Salaam huku nina familia inayonitegemea, inanipa mawazo sana. hapo hapo kodi, usafiri wa kunifikisha kazini, bado kazini sijala na nyumbani hiyo hiyo ndio tunayoitegemea. Nawaza hadi nachanganyikiwa.
Halafu kuna mtu analalamika mshahara wa milioni mbili haumtoshi, mahitaji hatufanani... Munhu atakuvusha hakuna mtihani Mungu kakupa usio wa kipimo chako, kuna mambo Mungu anakupitisha, utakua sawa, mbona humuamini Mungu wako, umekuja kutulilia wanadamu wenye makuu
 
Lakini mkuu nadhani bado maji hayafika shingoni Kama unavyodhani. mimi hata mlo wa Mara moja kwa siku sometimes nakosa. Nimehangaika Hadi nimekata tamaa ya kuishi. Wewe una uhakika walaki mbili kwa mwezi alafu unasema majiyamefika shingoni?! Acha kabisaa kufuru mkuu

Sent from my Infinix X650B using Tapatalk
Mwenzako ana familia wewe una familia ya kuitunza, msilinganishe mnachopokea, linganisha majukumu
 
Kuna rafiki yangu anafanyakazi mbili. Usiku nimlinzi na mchana anafanyakazi kweny maghala kubeba mizigo. Maisha yanaenda vizuri tu
Lazima kazi ya ulinzi haifanyi kwa umakini atakua anasinzia tu, ni hatari kubwa
 
Upo kwenye hatua ya kukua na kuvuka daraja mkuu. Haya mawazo ni dalili za kukomaa na kuingia hatua nyingine. Suluhu utakayoipata hapa itakua ya kudumu na utaisimamia ipasavyo.

Nimependa ulivyomuwazi na kuweka waka bayana kwamba msaada unaohitaji sio ajira pekee bali hata mawazo.

1. Tafuta kitabu kidogo sana kinaitwa The Richest Man in Babylon. Kisome, wana toleo la kiswahili pia.

2. Kuanzia mwezi ujao, watafute wadeni wako wote. Waambie hautaweza kuwalipa kiwango chote wanachokudai na utawalipa kidogo kidogo. Najua watacharuka na kukukatisha tamaa wengine watakudhalilusha lakini simamia hapo hapo ilimradi umaanishe kuwalipa kila mwezi.

3. Mshahara wako ukiupata, weka 10% kama akiba, najua utanitukana kimoyo moyo kwamba hapo tu hautoshi itakuaje ubakishe ziada ya kuweka akiba? Mshahara siku zote hautoshi. Hata ulipwe kiasi gani. Dhamiria kujilipa kwanza wewe hiyo asilimia kumi.

4. Baada ya kupunguza madeni na kuanza kuhifadhi hiyo akiba, tafuta mradi wife afanye mtaji ukiwa asilimia kumi uliyohifadhi.

Hii itakujengea msingi imara na nidhamu ya pesa.

Baadhi ya kauli za wanachama zisikukatishe tamaa. Tunatofauriana tabia, malezi, elimu n.k

Kikubwa usikate tamaa. Hii ni hatua ya kukuimarisha tu.
 

Attachments

Back
Top Bottom