X_INTELLIGENCE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2014
- 9,667
- 12,238
ndugu zangu wanajamiiforums, poleni kwa majukumu mazito yanayotukabiri kila kukicha. maisha yamenipiga Mtanzania mwenzenu, hali yangu kiuchumi inazidi kuwa mbaya kila kukicha nipo kwenye ajira sekta binafsi, lakini naishi nikiwa nimeshaumaliza mshahala kabla sijaupokea. Naona kabisa kwenye hii ajira niliyopo sitotimiza malengo yangu.
Watanzania wenzangu, nawaomba kwa moyo mnyoofu kabisa kwa yeyote mwenye kujua sehemu ambayo naweza nikafanya kazi anipe ramani hali inazidi kuwa ngumu sana kwangu.
Ujuzi wa ziada nilio nao ni Diploma ya uandishi wa Habari. Nina mke na mtoto ambao wananitegemea. Kwa mshahara ninaopata hivi sasa ikitokea bahati mbaya mmoja wetu ameumwa nitaumbuka vibaya sana kwani pesa zote zitatumika kutoa huduma za hospitali bajeti haitokidhi kabisa.
Ki makazi nipo Dar es Salaam.
Ieleweke kuwa nipo tayari kufanya kazi yoyote. Nitafurahi sana kama nitapata msaada haraka iwezekanavyo.