Natafuta binti wa kazi kwa ajili ya Mama Ntilie. Mshahara Tsh. 3,000/- kwa siku

Mkuu japo umejitetea na operation cost lakini ukweli kwa maisha ya Dar pesa yako bado ni ndogo! Maana unasema mfanyakazi wako anaanza kazi saa 1 asubuhi na kumaliza saa 7.

Hii manake anafanya kazi kuanzia asubuhi mpaka mchana! Offa zako umesma nje ya mshahara atapata chakula cha asubuhi, hii mana yake mchana na usiku gharama za chakula ni zake mwenyewe! Je kwa malipo hayo ya elf tatu anaishije kumbe?

Si itakuwa inaishia tu kwenye mlo wa mcha na usiku? Vipi kuhusu nauli yake ya kumleta na kumrudisha kazini everyday? Vipi kuhusu pesa ya sabuni ya kufungulia nguo zake maana unadhifu nao ni muhimu kwa mama ntilie, hata kama anavaa zile uniform na kofia lazima kuzifua kila wakati! Je kwa hiyo 3k ataweza kweli? Na kama kila siku unamlipa hiyo buk 3 means mwisho wa mwezi hana chake, Je akiugua upo tayari kumgharamia matibabu?

Mshahara wako unakaba kwa kila namna, mi binafs nashauri kama haiwezekani kuongeza japo ikafika buk5, basi fanya kumpa hifadhi ukae nae ili apate milo yote 3 kwako, alafu mkubaliane mshara hata ukipunguza mpaka 50k kwa mwezi ni nafuu kuliko hali hiyo ni ngumu, nina uhakika hata ukimpata hatodumu ataacha tu maana kama anaishi amepanga nyumba, kwa mshahara huo hawezilipa kodi ya nyumba!

Na kama anaishi kwao ni lazima watambana atoe pesa ya mahitaji nyumbani maana mabint wa nature hiyo hata makwao huwa hawajiwezi kiuchumi hivyo unawezakuta yeye ndo akawa tegemeo wa familia na mshahara wa buku 3 kwa siku!
Ww ndo hujaelewa hii n ajira ya aina gan, yaan ajira kama hiz lazma uishi kwenu na uish karib na eneo la kaz. Hayo maelezo yako ni level za juu kulinganisha na kaz hii. Kuna watu wanafanya kazi zaid ya huo mda na malipo n hayohayo.
Labda kama hujawahi kuzunguka mtaani kutafuta dayworker.
 
Umeona eeh. Kuna raia zaidi ya elfu 1 wanaingia humo daily na hawachoki wala kulalamika.

DAR MAISHA MAGUMU SANA

Kwa huo mshahara kuna nauli, kula, vocha, kodi ya nyumba na mengine kibao
Watu kama hao hawategemei hiyo tuu kuendesha maisha wengi n wake za watu, wadada wanaoish makwao, vijana wa kiume wanaoish makwao au mageto ya bei chee kama 20k-25k tena mnaish wawil au watatu. Na Milo yenu mara nying mihogo ya jero unalala usk. Kikubwa maisha yaende..
 
Tusiwabeze wawekezaji!! Ajira ni ajira hata kama ni 3000/= hiyo hela ni kubwa Kuna mtu anakaa tu nyumbani kwa wazazi hata kupata 1000 ni shida kwake! Fursa ya 3000 kwa siku ni kubwa mno kwa awamu hii ya tano, swala la usafiri sio lazima atoke mbali, hata kama anatoka mbali akifanya kazi kwa kujituma na biashara ikawa na wateja, sidhani kama boss wake atashindwa kumpa nauli, au kumuongezea mshahara, biashara is dynamic kila siku zinabadilika huwezi jua! Tatizo wabongo ni waongeaji Sana wa wa wanatanguliza, maslahi mbele kuliko kazi! Hata kama mshahara ni mdogo kafanye utapata uzoefu na ww utafungua yako!
 
Nampongeza sana huyo mama kwa kuweza kutengeneza ajira moja. Hii ni hatua kubwa mno. Mshahara wa 3000 kwa masaa 7 ni mwingi ikiwa mtu anakula hapohapo. Kwa sababu nimeguswa sana naomba mtoa post uje DM na mimi nichangie mtaji wa huyo mama endapo ni mdogo mno ili azidi kuchanja mbuga.
 
Nampongeza sana huyo mama kwa kuweza kutengeneza ajira moja. Hii ni hatua kubwa mno. Mshahara wa 3000 kwa masaa 7 ni mwingi ikiwa mtu anakula hapohapo. Kwa sababu nimeguswa sana naomba mtoa post uje DM na mimi nichangie mtaji wa huyo mama endapo ni mdogo mno ili azidi kuchanja mbuga.
Asante sana mkuu
Kwa kipindi hiki cha mvua huyu mama amekwama sana maana biashara haifanyiki tena.
Bati zinavuja sana hivyo kupelekea kazi kusimama.
Nitashukuru endapo ukisaidia
 
Jf ina vijana wa ajabu sana, mbona hamsemei mishahara ya viwandani huko watu wanafanya kazi masaa 12 kwa elfu 4? Chakula juu yao!

Nendeni hapo ubungo external mkaone nyomi ile ndo mje hapa kukashifu ajira nyingine..
Umebadili ID mkuu,300 anapika na chapati??akianza kuumwa kifua hyo 3000 itamtibu??acheni kunyanyasa watoto wa wenzenu kukanda ngano na kucjoma chapati kunaumiza kifua sana.
 
Mama ntilie na watu wa bar huwa wanahitaji mabinti kwa sababu nyingi tu.

Nadhani wanaume wanaelewa hili kwa kirefu..

Karibu supu kongoro mixer karafuu

Sipendi kuhudumiwa Supu au wali/ugali na Mwanamme!! Ila kwenye Chips sipendi naenda sehemu wanazopika wanaume ,Mwanammke hajui kupika chips.
 
Umebadili ID mkuu,300 anapika na chapati??akianza kuumwa kifua hyo 3000 itamtibu??acheni kunyanyasa watoto wa wenzenu kukanda ngano na kucjoma chapati kunaumiza kifua sana.
daaaaaah wabongo sisi gubu tunazidisha aisee kwani kuna mtu kashikiwa fimbo mkuu? hebu weka ofa yako na ww umlipe mtu 50k per day ili umfundishe kwa vitendo
 
mimi natafuta dem wa kuwa nachapa kila siku...3000/= kwa siku
Tunapima kwanza win win situation
 
Mkuu tangaza na ww kazi basi uwe unalipa 7,000/= kwa siku , mwenzako katangaza kutokana na mtaji wake na nature ya biashara yake, sasa na ww tangaza yako ili watu wasiende kungine waje kwako ww mwenye huruma
Acheni ubwege nyinyi hizo kazi muwape ndg zenu toka kijijini huko, hawezi toka mtu gmboto mpk mwenge mshahara 3000 si ufanye na mkeo mkalipe deni lenu benki.
 
Acheni ubwege nyinyi hizo kazi muwape ndg zenu toka kijijini huko, hawezi toka mtu gmboto mpk mwenge mshahara 3000 si ufanye na mkeo mkalipe deni lenu benki.
Mkuu kwan kuna mtu kalazimishwa kifanya hiyo kazi, ndio maana Jamaa kaweka tangazo tu , ukiona haina maslah kwako unaacha hakuna alielazimishwa , kingine uwe unaacha uongo jamaa kasema yupo tabata, hiyo gongolamboto na mwenge umeitoa wapi.

Pia kuna post ipo hapo juu kuna mtu kasema kuna watu wanafanya kazi kiwanda cha nondo kutwa nzima wanalipwa 3500/= na wanafanya unadhani nani yupo kwenye risk zaidi kati ya huyu mchoma chapati kwa masaa 6 na huyo Wa kiwandani .

Pia mkuu kama wewe umejaliwa ridhiki mshukuru mungu kuna watu wanaifatuta buku kwa tochi hawaipati .

Usipende kudharau na kudhihaki watu kisa wewe unakipato kikubwa
 
chapati kupikwa na moto huo wote na zilivyo za moto... wewe si ufikirie unategemea kuingiza kiasi gani.. ndio maana watu huwa wafanyakazi wanaondoka kila kukicha.. wakila zikawa tamu.. atavutwa tu na kupewa pesa zaidi..
 
Masaa 6 unalipwa elfu 3.

Halafu ukiangalia hii kazi anaweza pata uzoefu akaja kujiajiri kama mama ntilie.

Wasomi na Degee zao wanajitolea mwaka mzima kwa malipo ya chai na lunch.

Paza sauti na huko mkuu
Acha assumptions lipa mshahara mfanyakazi awe na furaha kwanza ndio kitu muhimu zaidi..
 
Back
Top Bottom