Natafuta binti wa kazi kwa ajili ya Mama Ntilie. Mshahara Tsh. 3,000/- kwa siku

Kiwanda cha MMI Steel kinawalipa vibarua wake 3500/=per day ,kazi ni masaa 12,nashangaa mnaomkejeli mleta mada.
nimegundua watu wengi humu wanamisha mazuri....agesema anhitaji mwanaume hii kazi hata mimi ningefanya kulingana na hesabu zangu.....

Assume mtu analinda kuanzia saa 12 jioni hadi asubui....hapo angeweza kufanya hiyo kazi anasevu 3000 na pesa ya chakula cha asubui na mchana.....kila kitu plan
 
Mkuu japo umejitetea na operation cost lakini ukweli kwa maisha ya Dar pesa yako bado ni ndogo! Maana unasema mfanyakazi wako anaanza kazi saa 1 asubuhi na kumaliza saa 7.

Hii manake anafanya kazi kuanzia asubuhi mpaka mchana! Offa zako umesma nje ya mshahara atapata chakula cha asubuhi, hii mana yake mchana na usiku gharama za chakula ni zake mwenyewe! Je kwa malipo hayo ya elf tatu anaishije kumbe?

Si itakuwa inaishia tu kwenye mlo wa mcha na usiku? Vipi kuhusu nauli yake ya kumleta na kumrudisha kazini everyday? Vipi kuhusu pesa ya sabuni ya kufungulia nguo zake maana unadhifu nao ni muhimu kwa mama ntilie, hata kama anavaa zile uniform na kofia lazima kuzifua kila wakati! Je kwa hiyo 3k ataweza kweli? Na kama kila siku unamlipa hiyo buk 3 means mwisho wa mwezi hana chake, Je akiugua upo tayari kumgharamia matibabu?

Mshahara wako unakaba kwa kila namna, mi binafs nashauri kama haiwezekani kuongeza japo ikafika buk5, basi fanya kumpa hifadhi ukae nae ili apate milo yote 3 kwako, alafu mkubaliane mshara hata ukipunguza mpaka 50k kwa mwezi ni nafuu kuliko hali hiyo ni ngumu, nina uhakika hata ukimpata hatodumu ataacha tu maana kama anaishi amepanga nyumba, kwa mshahara huo hawezilipa kodi ya nyumba!

Na kama anaishi kwao ni lazima watambana atoe pesa ya mahitaji nyumbani maana mabint wa nature hiyo hata makwao huwa hawajiwezi kiuchumi hivyo unawezakuta yeye ndo akawa tegemeo wa familia na mshahara wa buku 3 kwa siku!
Mleta uzi huu ushauri hujauona ama??
 
Jf ina vijana wa ajabu sana, mbona hamsemei mishahara ya viwandani huko watu wanafanya kazi masaa 12 kwa elfu 4? Chakula juu yao!

Nendeni hapo ubungo external mkaone nyomi ile ndo mje hapa kukashifu ajira nyingine..
Nimeulizia hapa naambiwa wanalipwa 110,000 per month na nyongeza ya 1000 kwa kila saa unayoongeza,na inategemea pia na kitengo ulichofanya

Wanaingia saa 2 asubuhi-11jioni
Duh hali siyo hali
 
Nimeulizia hapa naambiwa wanalipwa 110,000 per month na nyongeza ya 1000 kwa kila saa unayoongeza,na inategemea pia na kitengo ulichofanya

Wanaingia saa 2 asubuhi-11jioni
Duh hali siyo hali
Umeona eeh. Kuna raia zaidi ya elfu 1 wanaingia humo daily na hawachoki wala kulalamika.

DAR MAISHA MAGUMU SANA

Kwa huo mshahara kuna nauli, kula, vocha, kodi ya nyumba na mengine kibao
 
Hello Jf

Binti wa kazi anatafutwa.

Sifa
1. Ajue kupika chapati
2. Awe na Lugha nzuri kwa wateja na mchangamfu
3. Ajue hesabu
4. Awe anajua kuhudumia vizuri

Kazi ni ya mama ntilie, kuuza supu na chapati

Mshahara ni 3000 kwa siku, nyongeza utajadiliana na boss wako.

Chakula utapata hapo hapo asubuhi.

Kazi inaanza saa 1 asubuhi mwisho saa saba

Piga simu 0744033555

Tupunguze comment za kejeli, ukiona mshahara mdogo endelea na mishe zako.u
Usitishe watu wewe, mshahara huo unakufanya usijiamini ndio maana unasema tupunguze kejeli. Kama unaona mshahara huo ni mzuri na haupaswi kuchalenjiwa fanya kazi yako mwenyewe,amka asubui mpaka saa 7 uchukue 3000/ yako.
 
Usitishe watu wewe,mshahara huo unakufanya usijiamini ndio maana unasema tupunguze kejeli.Kama unaona mshahara huo ni mzuri na haupaswi kuchalenjiwa fanya kazi yako mwenyewe,amka asubui mpaka saa 7 uchukue 3000/ yako.
Masaa 6 unalipwa elfu 3.

Halafu ukiangalia hii kazi anaweza pata uzoefu akaja kujiajiri kama mama ntilie.

Wasomi na Degee zao wanajitolea mwaka mzima kwa malipo ya chai na lunch.

Paza sauti na huko mkuu
 
Back
Top Bottom