Nashauri kuwe na Database rasmi kwa ajili ya wote wanaofanya kazi zisizotegemea ujuzi wowote

Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
12,506
2,000
Hello JF,

Kwa muda mrefu sasa malalamishi ya housegirls kunyanyaswa katika nchi za kiarabu kama Oman, Turkey, etc. yamekua mengi.

Ninachoona hapa ni kutokua na taarifa ama records to identify those at risk.

Kama ilivyo vitambulisho kwa wafanyabiashara ndogo ndogo (Machinga), then kuwe na vitambulisho kwa WOTE wanaofanya kazi zisizohitaji ujuzi, nursing attendants, makuli, fundi towashi, bar attendants, and house girls.

Sijui if this will work, but tukishajua list ya hao kwa mfano house girls then itakua hata rahisi kujua wapo wapi,kama wameenda nje then itajulikana from database wapo nchi gani, huko nje sasa mabalozi iwe kazi yao kujua hao watu wana mikataba gani,inaisha lini, na ikiwezekana ujira wao, kukiwa na sheria au utaratibu wa kufuata haya.hasa hasa mikataba haya malalamishi yatapungua,(ninavyodhani).

Kingine ningependa kushauri serikali ni kuweka kiwango minimum ambacho hawa wafanyakazi wanaofanya kazi zisizohitaji ujuzi watalipwa, kiwango kisiwe kidogo, at least mtu amudu basics.

Ukiweka kiwango ambacho mtu anaweza akaendesha maisha yake, wengi hawatashawishika kwenda nje kufanya kazi ambazo wangeweza kufanya nchini.

Kukiwa na database na pia minimum wage housegirls ama kuli, fundi etc, itapunguza hata unanyanyasaji wao. Itakuwa rahisi to solve disputes.

It's time hawa wanaofanya kazi zisizo rasmi watambulike rasmi kwenye soko la ajira, wawe respected maslahi yao.

Becky.
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
3,845
2,000
Hapo ulipoishauri serikali kuwwka kiwango maalum cha mshahara kwa hao watu naona umekosea, kila mtu anajiwekea yeye kiwango cha kumlipa housegirl wake kutokana na hali yake kiuchumi, sasa kama serikali itawawekea kiwango cha juu hapo hata hao wafanyakazi hawatapata kazi na hali zao kiuchumi zitazidi kuwa mbaya.

Binafsi hapo ningeshauri, kutokana na hiyo database yako, serikali iwe inafuatilia kama hao watu wanalipwa mishahara yao kwa wakati kwa kile kiwango walichowekeana kwa makubaliano na mabosi wao, kama hilo likifanyika kwa ufasaha naamini tutakuwa tumepiga hatua kubwa kuwasaidia hao watu.

Hilo kwangu ni bora zaidi kuliko kuitaka serikali iwapangie mabosi nini cha kuwalipa, naamini mabosi wengi hawatakuwa na uwezo huo kutokana na hali ngumu ya kiuchumu tuliyonayo kwa wakati huu na mishahara ya wengi kutopandishwa karibia mwaka wa tano sasa.
 

Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
12,506
2,000
1611128246060.png
haya hizo ndio kazi za nursing attendants, je kusaidia wagonjwa kuoga.napo ni ujuzi??
 

Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
12,506
2,000
Hapo ulipoishauri serikali kuwwka kiwango maalum cha mshahara kwa hao watu naona umekosea, kila mtu anajiwekea yeye kiwango cha kumlipa housegirl wake kutokana na hali yake kiuchumi, sasa kama serikali itawawekea kiwango cha juu hapo hata hao wafanyakazi hawatapata kazi na hali zao kiuchumi zitazidi kuwa mbaya...
Sawa, asante mkuu kwa input yako.
 

Grahams

JF-Expert Member
Mar 19, 2016
1,519
2,000
Ninavyofahamu unapotafuta Visa ubalozini lazima utaje unaenda huko Nje ya Nchi kwa shughuli gani, labda itokee umedanganya shughuli unayokwenda kuifanya. Otherwise hizo taarifa zipo kwenye Balozi zetu.

Kwa upande walioko Tanzania nadhani ni ishu ya kuweza kuwatambua mfano Wafanyakazi wa viwandani nadhani wana Association yao, kwahiyo ni rahisi kutambulika. Wengine labda Machinga kupitia kanzi data ya Vitambulisho vya Ujasiriamali.

Kundi ambalo limesahaulika ni hilo la Wafanyakazi wa Majumbani (Ma House Girl) nadhani hao pia kuna haja ya kuwasajili na kuwatambua.

Sambamba na hilo kundi la mwisho ambalo pia ni muhimu kutambulika ni Machangudoa au siku hizi wanaitwa Wadangaji. Hawa pia kuna ambao huwa wanasafiri kabisa Nje ya Nchi kwa lengo la kukutana na wateja wao, hawa pia kama ni ishua ya ukatili huwa wanafanyiwa Sana i.e kutumika njia zote bila ridhaa yao, kufanywa Threesome/Foursome bila makubaliano sambamba na kutumika na Wanyama i.e Mbwa, Farasi, Punda n.k ikizingatia wanakuwa Ugenini kwahiyo unakuta hawana jinsi zaidi ya kukubali Ukatili huo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom