Nashangaa niliwezaje kujenga kipindi cha Hayati Magufuli lakini awamu ya sita najaribu mambo hayasomeki

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,403
Kipindi cha Magufuli cha awamu ya tano pamoja na madili kuwa magumi lakini kilichopatikana kilifaa hadi nikajenga nyumba si haba Nashukuru Mungu.

Siyo kujenga tu hata tuvituvitu nilinunua, watoto walikula vizuri, na walipendeza siyo haba.

Maduka yangu ya vifaa vya simu kariakoo niliyafunga nikabakisha moja tu baada ya kuzongwa na TRA, nilifunga yote nikabakiza kiduka kimoja tu kipindi cha magufuli.

Lakini kiduka hichohicho kimoja kilinipa faida kubwa nikajenga na mambo mengine yanakwenda.

Awamu ya sita imeingia nikasema alhamdullillah mambo yatakwenda.

Lakini ajabu awamu hii ya sita hata banda la kuku tu limenishinda! Kila pesa nayopata inapiliza kutibu shida ndogondgo za kila siku.

Mara Gesi imeisha, mara umeme, Mara ada, Mara spea, Mara chakula yaani pesa inaishia kwenye mambo ya kila siku tu hakuna jambo jingine nimeweza kufanya awamu ya sita.

kazi yangu ya awamu tano ni ileile ninayo awamu ya sita lakini sioni maendeleo je tatizo ni nini!?
 
Dah aisee upo km Mimi awamu ya magufuli nilikuwa nakiduka cha reja reja mtaani nilifanikiwa mpaka kujenga kinyumba kidogo japo nilikuwa nakiwanja tayari, awamu ya sita nimepata kazi nzuri alhamdulillah sikosi M2 per month lakini hakuna la maana inaishia kuwa Na mipango mingi kichwani hela inapotea kama mshale ila week hii kuna mbinu nazitumia za ku quit ile overspending naimani ni tabia zangu ndo zina cost japo kweli nowdays Nina kafamilia ila sio cha kunichakaza million aisee. Pumbaf pombe pumbavu Malaya hamnipati tenaaaa
 
Na pesa yake ni ile ile?

Au umeongeza micheps? Nayo inakukamua sana?
Sina Malaya wala mchepuko! Lakini nashangaa tu vihela navyopata vinaishia kwenye mboga mboga awamu hii sasa sijui shida iko wapi!
 
Awamu ya Jpm pesa zilikuwa kupatikana kwa tabu na ukakazana na duka na discipline ya pesa ilikuwa juu.. hata sasa unapata pesa sana ila umepunguza knowing mianja ya pesa ipo zitakuja tu acha nitumie, ndio maana huoni ukitunza
 
Mara Gesi imeisha, mara umeme, Mara ada, Mara spea, Mara chakula yaani pesa inaishia kwenye mambo ya kila siku tu hakuna jambo jingine nimeweza kufanya awamu ya sita.

kazi yangu ya awamu tano ni ileile ninayo awamu ya sita lakini sioni maendeleo je tatizo ni nini!?
Wakati wa Magu ulikuwa hununui gesi Mara chakula Mara spea mkuu?
 
Back
Top Bottom