Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,488
- 13,608
Binadamu husahau mapema sana. Nimekisikiliza kilio cha Msomi Kitwanga na nikagundua ni kinyongo halisi kinachokuwa katika maongezi ya kundi zima lililokuwa nyuma ya hayati JPM miaka ile akiwa ikulu.
Na maisha yanakwenda kasi sana. Wahenga tunaoazima mara nyingi busara zao wanayo misemo kuhusiana na huu unyonge walionao waliokuwa karibu na awamu ya tano katika kipindi hiki cha awamu ya sita. Utadhani sio wao waliokuwa wakilaumiwa kwa tabia hii hii inayoonekana kufanyika katika awamu ya sita.
Zipo tuhuma za chini kwa chini juu ya mambo mengi ya kikabila yaliyokuwa yakifanyika katika awamu ya tano. Halmashauri karibu zote nchini zilikuwa zikiongozwa na watu wa kabila la wasukuma na kibaya zaidi wakawa na tabia zile zie za kutaka kuonea watu wa makabila mengine.
Vikishamalizika tu vikao vya halmashauri ambavyo wao ni wengi kwa kubeba na kiongozi mkuu, wanaanza vikao vingine vya kwao wenyewe ambavyo lugha inayotumika humo inakuwa ni kisukuma kitupu!!.
Uongozi mzima kwa maana ya ule wa ngazi za kiutawala(kina TAMISEMI) ukawa ukikwazika na hulka hizi mpya. Majirani zangu hawa wa kanda ya ziwa wanayo ile superiority complex basi likawa ni tatizo juu ya tatizo.
Na binadamu tumeumbwa kujisahau, kumbe siku za hayati JPM juu ya uso wa ardhi hazikuwa zimebakia nyingi kama walivyokuwa wakijiaminisha, wakajikuta wameingiwa na ukiwa usioweza kuelezeka.
Hizi kelele nyingi zinazosikika miezi hii wakati SSH akija na mitazamo yao serikalini ni mchanganyiko wa huzuni/ukiwa/majuto na hasira za kwanini mkate wetu unatukimbia tena mchana kweupe mbele ya macho yetu.
Ndio serikali zinavyoendeshwa tuwe wapole tu. Tena awamu zote sita ni za chama kimoja, hivyo mtu anapokuja na malalamiko yake akumbuke kuwa SSH ni mpokeaji tu wa kijiti kutoka kwa hayati JPM, aliyepokea kijiti kutoka kwa JMK aliyepokea kijiti kutoka kwa hayati BWM na imekuwa ni desturi ya miaka na miaka kupokezana vijiti kwa njia ya amani na utulivu huku rais mpya akiapishwa mbele ya halaiki ya watu katikati ya uwanja wa mpira.
Tuwe wapole tu, ni nchi yenye amani na utulivu lakini misuguano midogo midogo lazima iwachubue watu na wajikute wamechunika ngozi zao hivyo kulialia sana pengine ni kusahau tu kuwa jana walikuwa nyuma ya mshika kijiti mkuu aliyetangulia mbele za haki.