Vita ya Uchumi haijawahi kuwa nyepesi, Hayati Magufuli aheshimiwe

Nehemia Kilave

JF-Expert Member
Jan 9, 2022
449
1,009
Habari JF, vita ya Uchumi kuanzia mitaani, mirathi na makazini hata iwe ndogo haijawahi kuwa nyepesi na haijawahi acha mtu salama.

Ukiwa kiongozi wa juu nchi za Africa huwa hakuna vita nyepesi ya uchumi sababu unakuwa unapigana watu wa ndani ya nchi lakini pia na mataifa ya nje.

Magufuli pamoja na mapungufu yake yote alieonyesha jitihada katika kupambana hii vita ndani ya nchi lakini pia nje ya kwa kupitia mikataba mibovu mbali mbali na kuivunja ingawa wimbi la kesi za kushindwa kimataifa limeongezeka. Kwanini hizi kesi ni kipindi hiki? Kuna watu wana nufaika na hizi kesi?

Ukimsikiliza hapa mwalimu Nyerere kuna kitu unaweza elewa.

Lakini JPM mwenyewe mara kadhaa kaongea kwa uchungu sana.

Kwa kifupi kabla hatujalaumu kwa yote tuliyopitia Awamu ya Tano au Tunayopitia awamu Hii cha kwanza jiulize unaweza vaa hivyo viatu na ukapigana na Mafisadi na Mabeberu?

Binafsi huwa namlaumu Magufuli kwa kitu kimoja tu, kutotuletea Katiba Mpya.

Tumuache mzee wetu apumzike kwa Amani.​
 
Attachments

  • 5416722-f2e41db15dcbb12961a981aac5f701a7.mp4
    9.5 MB

View attachment 2900394

Lakini JPM mwenyewe mara kadhaa kaongea kwa uchungu sana.
View attachment 2900408

Kwa kifupi kabla hatujalaumu kwa yote tuliyopitia Awamu ya Tano au Tunayopitia awamu Hii cha kwanza jiulize unaweza vaa hivyo viatu na ukapigana na Mafisadi na Mabeberu?

Binafsi huwa namlaumu Magufuli kwa kitu kimoja tu, kutotuletea Katiba Mpya.

Tumuache mzee wetu apumzike kwa Amani.​
Hiyo dhana ya ''vita ya uchumi'' ni moja ya vitu ambavyo Magufuli alifanikiwa kuwaaminisha wafuasi wake na mpaka kesho bado wataendelea kumsujudia. Ni kama vijijini, watu maskini wanavyoaminishwa na waganga au wenyewe kwa wenyewe kuwa umaskini wao unatokana na husda, vijicho na ulozi wanavyofanyiwa na maadui zao. Unakuta mtu ana nyumba ya nyasi na watoto 15, fedha yake yote inaishia kwa waganga kwa kuamini kuwa magonjwa, umaskini na kila aina ya masahibu yake yanatokana na kijicho cha maadui.
 
umewahi jiuliza kwanini africa ni maskini ?
 
Ukiwa kiongozi wa juu nchi za Africa huwa hakuna vita nyepesi ya uchumi sababu unakuwa unapigana watu wa ndani ya nchi lakini pia na mataifa ya nje.
Vita gani na mabeberu? Ufisadi unatumaliza kila siku alafu tunasingizia wazungu. Mfano kwa mwaka tu unakuta 30% ya makusanyo yanatapanywa je hapo vita ya kiuchumi inaingiaje. Huu ni msemo ulitungwa na CCM ili kutafuta mtu wa kumtupia lawama kwa failures zao. No wonder hata awamu ya 5 ilidai wapinzani walituchelewesha sana ilihali hawajawahi kusanya kodi au kupanga bajeti tokea uhuru!!

nje ya kwa kupitia mikataba mibovu mbali mbali na kuivunja ingawa wimbi la kesi za kushindwa kimataifa limeongezeka. Kwanini hizi kesi ni kipindi hiki? Kuna watu wana nufaika na hizi kesi?
Ni hivi mikataba inafuata sheria sio hisia au mihemko. Mfano tulidai Acacia wanatorosha makinikia. Ilipaswa twende ICSID tufungue kesi ya madai alafu tuweke ushahidi wa vifungu vilivyokiukwa mbona tungelipwa matrillion yote yale. Sasa cha ajabu tukaenda zuia makontena mara kamata kamata ya viongozi wa Acacia n.k. Kwa style ile wakifungua kesi hutoboi maana as much as wana makosa ila expropriation ya mali za mwekezaji ni serious offence!!

Kwa hiyo huyo huyo unayemsifia ilibidi atumie akili kuliko miguvu ili kupata popularity ya wapiga kura. So hatuna vita yoyote ila incompetence yetu ikiwa exposed tunalialia eti vita.
 
They say it's the White Man I should Fear, but its my Own kind doing all the Killing here....

Marginalization ya kweli na kipigo walipigiwa kina Nyerere, Patrice Lumumba na kina Thomas Sankara..., hawa wengine wa Sasa wanagawa mali hata bila kuombwa kwa ulafi na vijizawadi...
 
Hiyo dhana ya ''vita ya uchumi'' ni moja ya vitu ambavyo Magufuli alifanikiwa kuwaaminisha wafuasi wake na mpaka kesho bado wataendelea kumsujudia. Ni kama vijijini, watu maskini wanavyoaminishwa na waganga au wenyewe kwa wenyewe kuwa umaskini wao unatokana na husda, vijicho na ulozi wanavyofanyiwa na maadui zao. Unakuta mtu ana nyumba ya nyasi na watoto 15, fedha yake yote inaishia kwa waganga kwa kuamini kuwa magonjwa, umaskini na kila aina ya masahibu yake yanatokana na kijicho cha maadui.
Mbona wewe umeongea maneno mengi lkn hujasema chochote,umeishia kupinga na blabla zingine,jpm alikuwa na dhamira ya dhati ya kupigana vita ya kiuchumi,ila kwa nyie mliovaa miwani ya mbao za chuki na kupinga,ni ngumu sana kuelewa au kukubaliana na huo ukweli.
 
Kama umeona ni maneno mengi na sijasema chochote basi pole sana. Siwezi kukusaidia zaidi.
 
Vita gani na mabeberu? Ufisadi unatumaliza kila siku alafu tunasingizia wazungu. Mfano kwa mwaka tu unakuta 30% ya makusanyo yanatapanywa je hapo vita ya kiuchumi inaingiaje. Huu ni msemo ulitungwa na CCM ili kutafuta mtu wa kumtupia lawama kwa failures zao. No wonder hata awamu ya 5 ilidai wapinzani walituchelewesha sana ilihali hawajawahi kusanya kodi au kupanga bajeti tokea uhuru!!

Ni hivi mikataba inafuata sheria sio hisia au mihemko. Mfano tulidai Acacia wanatorosha makinikia. Ilipaswa twende ICSID tufungue kesi ya madai alafu tuweke ushahidi wa vifungu vilivyokiukwa mbona tungelipwa matrillion yote yale. Sasa cha ajabu tukaenda zuia makontena mara kamata kamata ya viongozi wa Acacia n.k. Kwa style ile wakifungua kesi hutoboi maana as much as wana makosa ila expropriation ya mali za mwekezaji ni serious offence!!

Kwa hiyo huyo huyo unayemsifia ilibidi atumie akili kuliko miguvu ili kupata popularity ya wapiga kura. So hatuna vita yoyote ila incompetence yetu ikiwa exposed tunalialia eti vita.
Kinachofanyika kwa sasa juu ya hizo kesi ni mgawo,watu wana kaa meza moja na washitaki,wanapiga pasu,halafu ndio hukumu ya kisanii inatoka.
 
Vita gani na mabeberu? Ufisadi unatumaliza kila siku alafu tunasingizia wazungu. Mfano kwa mwaka tu unakuta 30% ya makusanyo yanatapanywa je hapo vita ya kiuchumi inaingiaje. Huu ni msemo ulitungwa na CCM ili kutafuta mtu wa kumtupia lawama kwa failures zao. No wonder hata awamu ya 5 ilidai wapinzani walituchelewesha sana ilihali hawajawahi kusanya kodi au kupanga bajeti tokea uhuru!!

Ni hivi mikataba inafuata sheria sio hisia au mihemko. Mfano tulidai Acacia wanatorosha makinikia. Ilipaswa twende ICSID tufungue kesi ya madai alafu tuweke ushahidi wa vifungu vilivyokiukwa mbona tungelipwa matrillion yote yale. Sasa cha ajabu tukaenda zuia makontena mara kamata kamata ya viongozi wa Acacia n.k. Kwa style ile wakifungua kesi hutoboi maana as much as wana makosa ila expropriation ya mali za mwekezaji ni serious offence!!

Kwa hiyo huyo huyo unayemsifia ilibidi atumie akili kuliko miguvu ili kupata popularity ya wapiga kura. So hatuna vita yoyote ila incompetence yetu ikiwa exposed tunalialia eti vita.
kwenye hiyo mikataba shida ni JPM au walioingia ?
 
Vita ya uchumi ni changamoto kubwa ambayo inahitaji uongozi thabiti na mikakati madhubuti. Hayati John Pombe Magufuli, Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alikuwa kiongozi aliyefahamika kwa ufanisi wake katika kutekeleza sera za maendeleo na mapambano dhidi ya rushwa. Baadhi ya sera na mikakati aliyoiweka ililenga kuimarisha uchumi wa nchi, kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima, na kukuza maendeleo ya miradi ya miundombinu.
Ni muhimu kutambua kwamba maoni kuhusu utendaji wa kiongozi fulani yanaweza kutofautiana kulingana na mtazamo wa kisiasa na maoni ya watu binafsi. Wapo wanaomsifia kwa hatua zake za kufanya mageuzi na kuchochea maendeleo, wakati wengine wanaweza kuwa na wasiwasi kuhusu madhara yoyote au athari za sera zake.
Katika kumuenzi Hayati Magufuli, ni muhimu kuchambua matokeo ya sera na mikakati aliyoiweka, pamoja na kujadili mafanikio na changamoto zilizojitokeza. Kila kiongozi ana athari zake kwa uchumi na jamii, na mjadala juu ya mchango wake unaweza kutoa mwanga zaidi kuhusu njia zinazofaa kwa maendeleo ya nchi.
Ni vizuri kuzingatia umuhimu wa mjadala wa wazi, heshima kwa maoni tofauti, na kutafuta mbinu za kuendeleza maendeleo na ustawi wa nchi. Historia ya kiongozi yeyote inahitaji kuangaliwa kwa kina na kwa uwazi ili kuweza kutoa tathmini yenye busara na haki.
 
kwenye hiyo mikataba shida ni JPM au walioingia ?
kwenye hiyo mikataba shida ni JPM au walioingia ?
Literally Hatujalipishwa mabilion kisa kuingia mikataba mibovu, tumelipishwa mabilion kisa kuvunja mikataba. So kosa ni la JPM.

Mfano hao indiana resources haukuwa mkataba ilikua leseni tu ya kufanya exploration iliyopatikana kihalali. Cha ajabu wanatengeneza sheria mpya eti inafuta leseni zote za nyuma? Kwani hapo utamlaumu vipi Kikwete?
 
Back
Top Bottom