NASA kumpeleka mwanamke, mtu mweusi kwa mara ya kwanza mwezini kwa bajeti ya shilingi trilioni 55

Sam Gidori

Verified Member
Sep 7, 2020
93
150
Baada ya kutangaza hapa awali kuwa itampeleka mwanamke mwezini kwa mara ya kwanza, Shirika la Marekani la Anga za Juu (NASA) sasa limesema kuwa itampeleka mwezini mtu mweusi katika Mpango wake wa Artemis.

NASA imetoa pia ombi la bajeti yake itakayowezesha kumpeleka mwanadamu mwezini kwa mara ya kwanza baada ya zaidi ya miaka 50, bajeti inayofikia dola bilioni 24 za Marekani, sawa na Shilingi trilioni 55 na bilioni 661. NASA imesema kuwa lengo la kumpeleka mtu mweusi mwezini linaendana na jitihada za utawala wa Rais Biden wa kuongeza uwasa kwa wote.

Hii ni mara ya kwanza kwa NASA kudhihirisha kuwa inalenga kumpeleka mtu mweusi mwezini, ambapo hapo awali ilieleza kuwa inapanga kumrudisha binadamu mwezini na kumpeleka mwanamke kwa mara ya kwanza.

NASA imesema kuwa Mpango wake huo ni uwekezaji katika kesho ya ulimwengu na inaonesha ujasiri katika kile ambacho taasisi hiyo inaweza kufanikisha.

Mpango wa Artemis ulianza mwezi Mei mwaka 2019 wakati wa utawala wa Rais Trump na ulipangwa kukamilika mwaka 2024, lakini serikali ya Rais Biden haijaweka wazi ikiwa ipo tayari kutoa fedha kufanikisha mpango huo ndani ya muda uliopangwa.

Kumpeleka mwanadamu mwezini ni sehemu ya mwanzo ya Mpango huo ambao NASA inauita “Utafiti Endelevu wa Mwezi,” ikipanga pia kuendelea na kumpeleka mwanadamu katika sayari ya Mars.

Bajeti ya Mpango wa Artemis inatajwa kuwa ndogo ikilinganishwa na ile ya Mpango wa Apollo iliyompeleka mwanadamu kwa mara ya kwanza mwezini mpaka kukamilika kwake mwaka 1973, ikifikia dola bilioni 23.6 kwa wakati huo, sawa na dola bilioni 136 kwa thamani ya sasa, sawa na Shilingi trilioni 314.
Hata hivyo, NASA inakabiliana na kikwazo kutokana na kutopatikana kwa fedha hizo kwa wakati. NASA ilihitaji bajeti ya dola bilioni 3.2 ili kufanikisha shughuli zake kwa mwaka 2021, lakini Bunge la Marekani ilikuwa imepitisha dola milioni 600 tu kufikia mwezi Julai mwaka jana.

Chanzo: Live Science
 

Hakimu Mfawidhi

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
2,177
2,000
Ni billioni 2.4 ama 24, ikiwa ni 24 basi kwa kiwango cha kubadilisha pesa leo ya bank kuu ni dola moja shilingi 2309.89, hivyo dollar bilioni 24 ni shilingi trilioni 52 na ushee.

Ikiwa ni dollar bilioni 2.4 basi itakua trilioni 5 na ushee.
 

hearly

JF-Expert Member
Jun 19, 2014
42,740
2,000
Hawana lolote Wanataka kumpeleka Mtu mweusi huko akawe Kama sample ya majaribio yao
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom