Narudi kijijini kutafuta mke

Wana MMU....

Kwa heshima na taadhima bila taraghani wala tahanani naomba mniweke kwenye sala zenu ili safari yangu iwe ya mafanikio.

Ni ombi la dhati kabisa na nawasihi msilichukulie kuwa takriri wala tashtiti za Ngabu.

Hii si mara yangu ya kwanza kujaribu bakhti yangu katika medani za wapendanao.

Miaka takriban hamstaashara ilopita nilijaribu lakini mambo yakaenda mramba.

Sasa napiga tena moyo konde nijaribu nione.

Naomba niwashirikishe kwa picha mtiririko wa safari yangu kuanzia Ubungo hadi Ikungulyabashashi....karibuni sana.

Safari ni hatua na yangu ilianza jana saa kumi na mbili asubuhi pale Ubungo....

View attachment 366753

Mishale ya saa tano hivi tukaigongea hodi Morogoro.....mimi huyo hapo naongea na mchepuko kwenye simu.

View attachment 366754

Shinyanga tukaingia usiku....nikalala hapo hapo stendi kwenye vibanda na asubuhi nikajidamka na kupanda Ally's hadi Ikungu....

View attachment 366755

View attachment 366756

Hatimaye majira ya alasiri nikakanyaga nyumbani Ikungulyabashashi...

View attachment 366758

Karibuni nyumbani. Karibuni sana. Na karibuni wanzuki.

Hii Wazungu wanaita ,,midlife crisis" hakuna kingine!
 
Mi nakuombea wanaomsubiri mkeo town wabadili nia maana wanafurahije unaenda kuwaletea kitu OG.
 
mzee mwenzangu unaukumbuka ule wimbo wa profesa j....nikusaidiaje...
hiyo hapo nimekuambatanishia isikilize kwa makini sana kisha kuwa makini sana katika swala la kutafuta mke....mke mwema anakuja mwenyewe hatafutwi mke mwema ni kama zawadi kutoka kwa Mungu, muombe sana Mungu na popote anaweza akakukutanisha na mke mwema.
 
Yaani wewe jamaa wewe... salute, hiyo si ni stand ya zamani hapo Shy. Piga picha pande za Ikungulyababshashi naweza kuikumbuka pia.

Ni dalili nzuri za kutafuta mke toka usukumani maana hawa wengine ni vichomi.

Hapo niaje.....unapatambua? Ni maeneo ya mnadani. Ila Wasukuma tuko washamba eeh heheeee

20160509_165716.jpg

Downtown Ikungulyabashashi....cheki kikwangua anga hicho. Owner wake alikuwa Nyarugusu huko teh teh

20160509_183756.jpg

Hiyo bodaboda ni yangu by the way....
 
Huh!?!

Basi nimeghairi...acha nikimbizane tu na hawa akina Ralina wa mjini manake naweza kufa kwa shengesha na shinikizo bure!
..tena ukimpeleka huko USA ndio atakupa shinikizo la damu hadi usahaulike. Nakumbuka jamaa alienda US akaishi huko miaka kadhaa, baadae akaona arudi home kuoa. Alioa na kumpeleka mkewe US ili kuendelea na maisha, kumbe yule dada alikuwa na mtuwe huko.
....naamini unaweza kubashiri kilichoendelea.
 
Umezoea mitumba yenye nywele bandia, kope bandia, nyusi bandia, uso poda, marangi mdomoni, manyonyo mdindisho, kalio mjaladio, kucha bandia, sikio tundu tano, pua kipini, ulimi kipini, kwapa mpulizo, papuchi kipini, kitovu kipini, kiuno cheni, mguu kikuku, shupi bikini wa kijiji utamuweza kweli Mkuu.
 
Hapo niaje.....unapatambua? Ni maeneo ya mnadani. Ila Wasukuma tuko washamba eeh heheeee

View attachment 366781

Downtown Ikungulyabashashi....cheki kikwangua anga hicho. Owner wake alikuwa Nyarugusu huko teh teh

View attachment 366788

Hiyo bodaboda ni yangu by the way....

DFPA ni plate # za miradi, hahahaa. Hii story ya si ya kuichukulia kibubusa. Bodaboda ya mradi....
 
Wana MMU....

Kwa heshima na taadhima bila taraghani wala tahanani naomba mniweke kwenye sala zenu ili safari yangu iwe ya mafanikio.

Ni ombi la dhati kabisa na nawasihi msilichukulie kuwa takriri wala tashtiti za Ngabu.

Hii si mara yangu ya kwanza kujaribu bakhti yangu katika medani za wapendanao.

Miaka takriban hamstaashara ilopita nilijaribu lakini mambo yakaenda mramba.

Sasa napiga tena moyo konde nijaribu nione.

Naomba niwashirikishe kwa picha mtiririko wa safari yangu kuanzia Ubungo hadi Ikungulyabashashi....karibuni sana.

Safari ni hatua na yangu ilianza jana saa kumi na mbili asubuhi pale Ubungo....

View attachment 366753

Mishale ya saa tano hivi tukaigongea hodi Morogoro.....mimi huyo hapo naongea na mchepuko kwenye simu.

View attachment 366754

Shinyanga tukaingia usiku....nikalala hapo hapo stendi kwenye vibanda na asubuhi nikajidamka na kupanda Ally's hadi Ikungu....

View attachment 366755

View attachment 366756

Hatimaye majira ya alasiri nikakanyaga nyumbani Ikungulyabashashi...

View attachment 366758

Karibuni nyumbani. Karibuni sana. Na karibuni wanzuki.
Mkuu wanzuki inangenezwaje kweli nisaidie maana ilikuwa kinywaji changu miaka ya 90 wakati nikiwa kanda hiyo.
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom