Napitia katika changamoto kubwa

Napitia katika changamoto kubwa

Dada, kufunga novena bila juhuzi ya ziada ni kasi bure. Fuatilia mfumo wako wa maisha. Namna unavyoishi na watu. Unawachukuliaje, unawasiliana nao vipi, unawajibika vipi kwao.

Jambo moja linalonishangaza ni kutaka kujiingiza kwenye mapenzi na mume wa mtu. Fikiria angekuwa ni mume wako. Ni nafuu ukaridhika na maisha hayo kuliko kukubali kufanya mambo mabaya kama ya kutembea na mume wa mtu. Madhara yake ni makubwa zaidi.

Fuatilia maisha yako. Badili staili ya maisha. Mume utampata kwenye maisha yako ya kila Siku. Badili namna unavyohusiana na watu. Ninaona kuwa, una changamoto fulani hapa.

Kila la kheri.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hili ndio jibu sahihi.
Na kuna ile hali ya kuchaguaaa sana nayo ni mbaya Na inaponza.Ni vizuri kuchagua but isiwe too much mpaka basi.Kila MTU ana mapungufu yake kikubwa kuchukuliana Na kuvumiliana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana umenikumbusha mbali sana,nakumbuka nilikuwa na rafiki mmoja a wakati huo alikuwa kama na miaka 33,hana mume wala mtoto,kuona umri unamtupa mkono sababu hata waliokuwa wanampa mambo ikawa shikamo dada,mara ghafla nakutongozwa na maneno kama nakupenda yakapungua,ghafla akajikuta anahitaji mtoto kwa khali na mali,mimba akapata mwisho wa siku akajifungua baada ya wiki moja akafa mtoto akabaki,na mbaya zaidi hata baba wa mtoto aliingia mitini ni kama vile alimlazimisha wazae ingawa inaoneka jamaa hakutaka kabisa,toka dada ana mimba mpaka anakufa jamaa hakutokea kabisa ikabidi siku za kliniki unavaa uhusika sababu tulikuwa tunaheshimiana mno,ushauri wangu kwako usilazimishe vitu unaweza pata hitaji la moyo wako kwa gharama kubwa,yote mkabidhi Mungu
Kuna watu wameolewa lakini hawana vizazi,kuna watu hawajaolewa lakini wana watoto,kuna watu hawajaolewa na pia niwagumba,Mungu ndiye hutoa yote,lakini pole sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni Kweli uliyosema but ungechagua mfano mwingine wa Kufa tena.
Nimesikitika kwa huyo Dada aliyekufa Na kuacha Mtoto I can imagine how it feels like.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari za jumapili wana jamii.
Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 32 kwa sasa. Napitia katika changamoto kubwa sana.
Hapo mwanzo kipindi ninasoma niliona si vyema kujiingiza katika mahusiano ya kufanya mapenzi kwani niliona yatanivuruga na ningejikuta napitia katika mahusiano mengi kitu ambacho sijawahi kukipanga maishani.
Nikamaliza chuo vizuri namshukuru Mungu.katika kutafuta ilikuwa ngumu kidogo nilitafuta mpaka nikakata tamaa nikaomba Mungu mpaka nikaona inatosha. Katikati ya kukata tamaa nikamuomba Mungu basi anipe kitu kimoja kwanza mme au kazi. Ila la kazi ndio nililoliwekea msisitizo kwani kwa kipindi hicho familia yangu ilikuwa inapitia changamoto nyingi kwa hiyo nikaona kazi itanisaidia kupunguza changamoto ama la basi niolewe ili nipunguze mzigo kwa familia yangu.
Siku isiyotarajiwa nikaitwa interview na nikapata kazi nzuri ambayo sikuwahi hata kufikiria wala kuiwaza.
Nikashukuru Mungu na kuanza maisha mapya ya kazi na kusaidia familia yangu. Nikajikita kwenye kumuomba Mungu anijalie mme mwema atakayenifaa na kuongoza familia tutakayoipata katika misingi ya imani ta dini ya kikristo. Sikubagua kabila wala atakuwa mkirsto wa aina gani maadamu awe anaabudu jumapili maana mimi nilikuwa tiari kuhama katoliki ili tulee familia yetu tukiwa na muongozo wa dini moja.

Sikuwahi kudhani nitafikia huku maana mpaka sasa imekuwa ngumu kama ni Mungu hachelewi ama hawahi basi kwangu mimi kwa sasa imekuwa ni shida kubwa. Nimefunga novena nimesali sana mpaka naona nimeanza kuathilika nahili swala. Mwaka jana tarehe moja nikaona basi kama mme wangu hayupo nipate tu mwanamme nitakae zaa nae lakini awe mkirsto maana siko tiari kumtenga baba na mtoto wake hata kama hamhudumii, nikiamini kuwa uwezo wa kulea mwenyewe ninao hata kama watoto watakuwa zaidi ya mmoja niko tiari kupambana na maisha. Nikaona kwa sababu nitakuwa pekeangu nikaanza kuwekeza ili watoto wangu wanikute nimejiandaa. Na penyewe Mungu akaona wakati wangu bado.
Mwaka huu mwezi wa pili akatokea mme wa mtu kitu ambacho sijawahi hata fikiria kuwa kunasiku nitaangukia huko, Mwanzoni nilitaka tuzungumze mapema kabla hatujazoena sana matakwa yangu lakini akawa mtu wa kuona nampangia sheria mapema na kudai hizo mipango ninazotaka kupanga nae tukiwa hatujafika mbali ni mipango gani. Nikaona isiwe tabu.
Ikafika siku ya kukutana nikamwambia mimi sijawahi kabisa hakuamini na nikamwambia kama anajiamini aendelee ila ajue atakuwa na deni la kulipa, akatafakari akaona viatu ni vikubwa akaondoka.

Chenga zikaongezeka nikajiuliza ni nini shida, tukapanga tukutane ili tuone hatima ni nini kati yetu. Akaja na kudai yeye hayuko tiari kutoa bikira ya mtu asiye na mpango nae. nikamuelewa na nikaona yuko sahihi.Nikamuuliza wewe ulivyoanza ulitegemea mimi ni mti sina hisia za kufanya mapenzi akadai alijua anajihusisha na mapenzi ya kila mtu ana mtu wake hivyo wanakutana kulizishana tu. Akaniambia nahitaji nini hasa kwake nikamwambia kama ulishaona hisia zangu unadhani nahitaji nini? Niliona nisianze kutaja shida niliyonayo kwanza nimsikilize yeye ndio na mimi niseme ya kwangu. Yeye akadai aliona ni mahusiano ya kula na kuondoka. Akaniambia kama niko tiari ataweka sheria za kutuongoza za maandishi ili baadae tusijekupeana shida. Nikamwambia sheria zako utazoniwekea nitazifuata vilivyo japo najijua ninawivu lakini wewe ni mme wa mtu tiari nitavumilia. Akaja na sheria na mipango mingi sana asee.sheria nyingi nilivyotafakari nikaona nyingi zinamlenga mtoto ambaye mimi ndio ninayemhitaji zaidi. na yeye akaona labda ni mmoja tu wakati mimi nishajipangia wakunitosha kabisa. Kwa maelezo yake nikaona hayuko tiari kuwa na mtoto nje ya familia na nikitokea kumpata basi nitoe mimba ama atamchukua. Nilichoka viungo vyote. Akaniuliza unalolote nikamwambia nizungumze nini wakati sheria zimekuwa ngumu.

Haki ya Mungu yaani natamani siku zirudi nyuma nizunguke na wanaume kama wafanyavyo wengine. Hukukujitunza kwangu kunanifanya nilie kila siku na kuomba Mungu usiku kucha kisa nilimtunzia mtu bikira. Jamii inayonizunguka itanitia wazimu maana swali la unaolewa lini limenichosha kabisa. Basi kama siolewi hata mtoto tu ni shida kumpata.

Kwasasa ninashida na mtoto kuliko maelezo na niendako nadhani nitawehuka. Msaada wenu tafadhalini sana.

NB. Hapo mwanzo nilifunga novena kwa muda wa mwaka mmoja na kuomba na kukabidhi mwili wangu uwe kwa ajili ya mtu mmoja tu ambaye ndio atakayekuwa mme au baba wa watoto wangu. Ndio maana inaniwia vigumu kuingia mahusiano mbalimbali.
Njoo pm tupange...
 
Fanya subira - kila kitu kina wakati wake kuwa mkakamavu na imani yako kwa Mungu - haya yote inaweza kuwa yanatokea ni kwa masilahi yako na upendo wa Mungu kwako - usikate tamaa na kujipeleka mweyewe kwenye mitego na majanga
 
Stress ziko pale pale mkuu unless mawazo yako yatimie kama ulivyokusudia awali kinyume na hapo umetengeneza hisia ili kuendana na mazingira yanayokuandama!
Ukijifunza kuwa positive kwa kila jambo na subira utapata Amani ya moyo ukiwa na mihemko unajitaftia maradhi bure. Pia wataalamu wadai kukifikiria kitu na kikuumize hamainishi unakiondoa ila unajiandalia matatizo plus, in this life health, peace of mind, shelter ni mambo ya kumshukuru Mungu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani usipoangalia utaangukia pabaya sana utatolewa bikra utabeba mimba na utapata tabu sana hata kama upo tayari kulea mtoto tulia mwanamke. Calm down watu wanaolewa mpaka miaka 40 miaka 32 umekuwa chizi hivyo. Jichanganye nenda kanisani, harusini, sokoni, vikao vya harusi, jitoe hata out kidogo uonekane. Wakati wa Mungu ni wakati sahihi ukifika utapata mume tu endelea kuomba bila kuchoka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom