Napitia katika changamoto kubwa

Napitia katika changamoto kubwa

Habari za Jumapili wanajamii.

Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 32 kwa sasa. Napitia katika changamoto kubwa sana.

Hapo mwanzo kipindi ninasoma niliona si vyema kujiingiza katika mahusiano ya kufanya mapenzi kwani niliona yatanivuruga na ningejikuta napitia katika mahusiano mengi kitu ambacho sijawahi kukipanga maishani.

Nikamaliza chuo vizuri namshukuru Mungu.katika kutafuta ilikuwa ngumu kidogo nilitafuta mpaka nikakata tamaa nikaomba Mungu mpaka nikaona inatosha. Katikati ya kukata tamaa nikamuomba Mungu basi anipe kitu kimoja kwanza mme au kazi. Ila la kazi ndio nililoliwekea msisitizo kwani kwa kipindi hicho familia yangu ilikuwa inapitia changamoto nyingi kwa hiyo nikaona kazi itanisaidia kupunguza changamoto ama la basi niolewe ili nipunguze mzigo kwa familia yangu.

Siku isiyotarajiwa nikaitwa interview na nikapata kazi nzuri ambayo sikuwahi hata kufikiria wala kuiwaza. Nikashukuru Mungu na kuanza maisha mapya ya kazi na kusaidia familia yangu. Nikajikita kwenye kumuomba Mungu anijalie mme mwema atakayenifaa na kuongoza familia tutakayoipata katika misingi ya imani ta dini ya kikristo. Sikubagua kabila wala atakuwa mkirsto wa aina gani maadamu awe anaabudu jumapili maana mimi nilikuwa tiari kuhama katoliki ili tulee familia yetu tukiwa na muongozo wa dini moja.

Sikuwahi kudhani nitafikia huku maana mpaka sasa imekuwa ngumu kama ni Mungu hachelewi ama hawahi basi kwangu mimi kwa sasa imekuwa ni shida kubwa. Nimefunga novena nimesali sana mpaka naona nimeanza kuathirika na hili swala. Mwaka jana tarehe moja nikaona basi kama mme wangu hayupo nipate tu mwanamme nitakae zaa nae lakini awe mkirsto maana siko tiari kumtenga baba na mtoto wake hata kama hamhudumii, nikiamini kuwa uwezo wa kulea mwenyewe ninao hata kama watoto watakuwa zaidi ya mmoja niko tiari kupambana na maisha.

Nikaona kwa sababu nitakuwa pekeangu nikaanza kuwekeza ili watoto wangu wanikute nimejiandaa. Na penyewe Mungu akaona wakati wangu bado. Mwaka huu mwezi wa pili akatokea mme wa mtu kitu ambacho sijawahi hata fikiria kuwa kunasiku nitaangukia huko, Mwanzoni nilitaka tuzungumze mapema kabla hatujazoena sana matakwa yangu lakini akawa mtu wa kuona nampangia sheria mapema na kudai hizo mipango ninazotaka kupanga nae tukiwa hatujafika mbali ni mipango gani. Nikaona isiwe tabu.

Ikafika siku ya kukutana nikamwambia mimi sijawahi kabisa hakuamini na nikamwambia kama anajiamini aendelee ila ajue atakuwa na deni la kulipa, akatafakari akaona viatu ni vikubwa akaondoka.

Chenga zikaongezeka nikajiuliza ni nini shida, tukapanga tukutane ili tuone hatima ni nini kati yetu. Akaja na kudai yeye hayuko tiari kutoa bikira ya mtu asiye na mpango nae. nikamuelewa na nikaona yuko sahihi.Nikamuuliza wewe ulivyoanza ulitegemea mimi ni mti sina hisia za kufanya mapenzi akadai alijua anajihusisha na mapenzi ya kila mtu ana mtu wake hivyo wanakutana kulizishana tu. Akaniambia nahitaji nini hasa kwake nikamwambia kama ulishaona hisia zangu unadhani nahitaji nini? Niliona nisianze kutaja shida niliyonayo kwanza nimsikilize yeye ndio na mimi niseme ya kwangu. Yeye akadai aliona ni mahusiano ya kula na kuondoka. Akaniambia kama niko tiari ataweka sheria za kutuongoza za maandishi ili baadae tusijekupeana shida. Nikamwambia sheria zako utazoniwekea nitazifuata vilivyo japo najijua ninawivu lakini wewe ni mme wa mtu tiari nitavumilia.

Akaja na sheria na mipango mingi sana asee.sheria nyingi nilivyotafakari nikaona nyingi zinamlenga mtoto ambaye mimi ndio ninayemhitaji zaidi. na yeye akaona labda ni mmoja tu wakati mimi nishajipangia wakunitosha kabisa. Kwa maelezo yake nikaona hayuko tiari kuwa na mtoto nje ya familia na nikitokea kumpata basi nitoe mimba ama atamchukua. Nilichoka viungo vyote. Akaniuliza unalolote nikamwambia nizungumze nini wakati sheria zimekuwa ngumu.

Haki ya Mungu yaani natamani siku zirudi nyuma nizunguke na wanaume kama wafanyavyo wengine. Hukukujitunza kwangu kunanifanya nilie kila siku na kuomba Mungu usiku kucha kisa nilimtunzia mtu bikira. Jamii inayonizunguka itanitia wazimu maana swali la unaolewa lini limenichosha kabisa. Basi kama siolewi hata mtoto tu ni shida kumpata.

Kwasasa ninashida na mtoto kuliko maelezo na niendako nadhani nitawehuka. Msaada wenu tafadhalini sana.

NB. Hapo mwanzo nilifunga novena kwa muda wa mwaka mmoja na kuomba na kukabidhi mwili wangu uwe kwa ajili ya mtu mmoja tu ambaye ndio atakayekuwa mme au baba wa watoto wangu. Ndio maana inaniwia vigumu kuingia mahusiano mbalimbali.
Dada Tunaomba mrejesho. Kuna maneno hapa yapo.
 
Sasa hivi naona kama umri unaenda sana hivyo nahofia kukosa mtoto kabisa. Tatizo kubwa nililonalo ninapenda sana watoto na kwa sasa namhitaji kuliko ninavyoweza zungumza.
Du pole sana unapatikana wapi? Mmmmmh nimekuonea huruma njoo nikupe hitaji la moyo wako
 
Unafunga novena ili upate Mume! Unapomuomba Mungu afu unampangia muda na matamanio yako jua tu Mungu hayupo hivo kabisa. Acha kunung’unika na tunza usichana wako. Mume atakuja maana kama umeamua Kumshirikisha Mungu basi jua Mungu hawahi wala hachelewi. Kamwe usitumie akili zako na fahamu zako na hayo ndiyo yanaleta mkwamo kwako.

Akili yako inapoishia ndo Mungu anapoanzia naona hutaki kukubali kwamba subiri. Kuna siku utaomboleza ukiendelea namna hiyo. Afu kufunga sio issue. Nashauri utubu na uhojiane na Mungu Isaya 45:11 kama ombi la kazi kakupa basi vumilia hata iwe 40 uwe mvumilivu mpaka kufa
 
Habari za Jumapili wanajamii.

Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 32 kwa sasa. Napitia katika changamoto kubwa sana.

Hapo mwanzo kipindi ninasoma niliona si vyema kujiingiza katika mahusiano ya kufanya mapenzi kwani niliona yatanivuruga na ningejikuta napitia katika mahusiano mengi kitu ambacho sijawahi kukipanga maishani.

Nikamaliza chuo vizuri namshukuru Mungu.katika kutafuta ilikuwa ngumu kidogo nilitafuta mpaka nikakata tamaa nikaomba Mungu mpaka nikaona inatosha. Katikati ya kukata tamaa nikamuomba Mungu basi anipe kitu kimoja kwanza mme au kazi. Ila la kazi ndio nililoliwekea msisitizo kwani kwa kipindi hicho familia yangu ilikuwa inapitia changamoto nyingi kwa hiyo nikaona kazi itanisaidia kupunguza changamoto ama la basi niolewe ili nipunguze mzigo kwa familia yangu.

Siku isiyotarajiwa nikaitwa interview na nikapata kazi nzuri ambayo sikuwahi hata kufikiria wala kuiwaza. Nikashukuru Mungu na kuanza maisha mapya ya kazi na kusaidia familia yangu. Nikajikita kwenye kumuomba Mungu anijalie mme mwema atakayenifaa na kuongoza familia tutakayoipata katika misingi ya imani ta dini ya kikristo. Sikubagua kabila wala atakuwa mkirsto wa aina gani maadamu awe anaabudu jumapili maana mimi nilikuwa tiari kuhama katoliki ili tulee familia yetu tukiwa na muongozo wa dini moja.

Sikuwahi kudhani nitafikia huku maana mpaka sasa imekuwa ngumu kama ni Mungu hachelewi ama hawahi basi kwangu mimi kwa sasa imekuwa ni shida kubwa. Nimefunga novena nimesali sana mpaka naona nimeanza kuathirika na hili swala. Mwaka jana tarehe moja nikaona basi kama mme wangu hayupo nipate tu mwanamme nitakae zaa nae lakini awe mkirsto maana siko tiari kumtenga baba na mtoto wake hata kama hamhudumii, nikiamini kuwa uwezo wa kulea mwenyewe ninao hata kama watoto watakuwa zaidi ya mmoja niko tiari kupambana na maisha.

Nikaona kwa sababu nitakuwa pekeangu nikaanza kuwekeza ili watoto wangu wanikute nimejiandaa. Na penyewe Mungu akaona wakati wangu bado. Mwaka huu mwezi wa pili akatokea mme wa mtu kitu ambacho sijawahi hata fikiria kuwa kunasiku nitaangukia huko, Mwanzoni nilitaka tuzungumze mapema kabla hatujazoena sana matakwa yangu lakini akawa mtu wa kuona nampangia sheria mapema na kudai hizo mipango ninazotaka kupanga nae tukiwa hatujafika mbali ni mipango gani. Nikaona isiwe tabu.

Ikafika siku ya kukutana nikamwambia mimi sijawahi kabisa hakuamini na nikamwambia kama anajiamini aendelee ila ajue atakuwa na deni la kulipa, akatafakari akaona viatu ni vikubwa akaondoka.

Chenga zikaongezeka nikajiuliza ni nini shida, tukapanga tukutane ili tuone hatima ni nini kati yetu. Akaja na kudai yeye hayuko tiari kutoa bikira ya mtu asiye na mpango nae. nikamuelewa na nikaona yuko sahihi.Nikamuuliza wewe ulivyoanza ulitegemea mimi ni mti sina hisia za kufanya mapenzi akadai alijua anajihusisha na mapenzi ya kila mtu ana mtu wake hivyo wanakutana kulizishana tu. Akaniambia nahitaji nini hasa kwake nikamwambia kama ulishaona hisia zangu unadhani nahitaji nini? Niliona nisianze kutaja shida niliyonayo kwanza nimsikilize yeye ndio na mimi niseme ya kwangu. Yeye akadai aliona ni mahusiano ya kula na kuondoka. Akaniambia kama niko tiari ataweka sheria za kutuongoza za maandishi ili baadae tusijekupeana shida. Nikamwambia sheria zako utazoniwekea nitazifuata vilivyo japo najijua ninawivu lakini wewe ni mme wa mtu tiari nitavumilia.

Akaja na sheria na mipango mingi sana asee.sheria nyingi nilivyotafakari nikaona nyingi zinamlenga mtoto ambaye mimi ndio ninayemhitaji zaidi. na yeye akaona labda ni mmoja tu wakati mimi nishajipangia wakunitosha kabisa. Kwa maelezo yake nikaona hayuko tiari kuwa na mtoto nje ya familia na nikitokea kumpata basi nitoe mimba ama atamchukua. Nilichoka viungo vyote. Akaniuliza unalolote nikamwambia nizungumze nini wakati sheria zimekuwa ngumu.

Haki ya Mungu yaani natamani siku zirudi nyuma nizunguke na wanaume kama wafanyavyo wengine. Hukukujitunza kwangu kunanifanya nilie kila siku na kuomba Mungu usiku kucha kisa nilimtunzia mtu bikira. Jamii inayonizunguka itanitia wazimu maana swali la unaolewa lini limenichosha kabisa. Basi kama siolewi hata mtoto tu ni shida kumpata.

Kwasasa ninashida na mtoto kuliko maelezo na niendako nadhani nitawehuka. Msaada wenu tafadhalini sana.

NB. Hapo mwanzo nilifunga novena kwa muda wa mwaka mmoja na kuomba na kukabidhi mwili wangu uwe kwa ajili ya mtu mmoja tu ambaye ndio atakayekuwa mme au baba wa watoto wangu. Ndio maana inaniwia vigumu kuingia mahusiano mbalimbali.
Kila Jambo na wakati wake, ukija kujua kuwa hadi ulipo hapo mzima, unatype kwa raha kabisa ni kwa sababu hukuwa na mtu hutoona umechelewa kitu na utasubiri kwa upole, endelea na mengine huenda mtu wako uliyepangiwa na Mungu ana majukumu mengine akimaliza atakuja na utakutanishwa naye. Ukiwa mnyenyekevu sana na mtii kwa Mungu atakufunulia ndotoni.
 
Una tatizo kwenye r na l au?
Huu uzi ukiupitia kuna baadhi ya koment zinaflaisha sana

Ila kiukwer miaka 32 bado mdogo sana

Binafsi nina dada angu yeye kaolewa ana miaka 39 kwa muda wote huo alikuwa nyumban

Na mtt kapatia huo umri nw day ana watoto wawil na wanapendana sana na mume wake na wanamaisha mazur tuu

Mi huwa naamin kira jambo na wakat wake kikubwa kusari sana na kuwa na iman kwa icho ukifanyacho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom