Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,703
- 218,239
Kwa miaka yote tangu ateuliwe kuwa IGP, Mtukufu Sirro amejipambanua kuwa upande wa CCM, huyu ndio chanzo cha vurugu kwenye harakati zote za kisiasa za vyama vya upinzani, ameshiriki kuvuruga, kuumiza na kuua Raia wasio na hatia kwenye mikutano na maandamano ya amani ya vyama vya siasa yasiyo na vurugu zozote.
Ametumika sana na Serikali ya CCM kudanganya raia ili kunufaisha chama chake cha CCM, NENDENI TUNDUMA MKAJIONEE UNYAMA WALIOFANYIWA CHADEMA, Mauaji ya Akwilina na utekaji wa MO ni ushahidi wa uongo wa wazi na wa kishamba sana wa Simon Sirro, kama yeye mwenyewe au mpambe wake anabisha ajitokeze hadharani .
Mtesaji mkuu wa Wanasiasa wa Tanzania kwa awamu ya 5 na hii ya 6 ni Simon Sirro kupitia Jeshi analoliongoza la polisi , kwa kadri ya kumbukumbu zangu sijawahi kuona vurugu zozote za kisiasa zilizoanzishwa na upinzani, bali nimeshuhudia utesaji , manyanyaso , wizi wa kura wa aibu sana na utekaji wa viongozi wa upinzani ukisimamiwa na Jeshi la polisi lililo chini ya Sirro.
Mtu wa namna hii hana uwezo wa kuitisha kikao na vyama vya siasa vya upinzani kwa namna yoyote ile si tu kwa vile hana MAMLAKA YA KISHERIA YA KUFANYA HIVYO , Bali pia haaminiki na anao upande wake wa yule aliyemteua ambaye ni Mwenyekiti wa CCM.
NASHAURI CHAMA CHANGU CHA CHADEMA KUTOHUDHURIA KIKAO CHOCHOTE KITAKACHOITISHWA NA SIMON SIRRO akiwa yeye binafsi ama akivaa cheo cha IGP.
NAKALA: John Mnyika
=========
Maoni ya Tundu Lissu kuhusu jambo hili haya hapa .