Dunyua,
Kipindi cha jaribio la kwanza la kumpindua Nyerere mbona Muingereza aliingilia kati kumnusuru Nyerere?
Mkuu Coscated
Wakati naandika Kuchangia uzi huu nilikumbuka hilo la Waingereza kumsaidia Mwl wakati wa Uasi ule wa wanajeshi wetu. Si rahisi kusema kwanini Waingereza walimsaidia wakati ule lakini nikiangalia juu juu naweza sema miaka ile ambayo ilikuwa mwanzoni mwa 1960, haikuwa rahisi kumtambua Mwl na misimamo yake. Nafikiri sijui ingekuwaje kama mapinduzi yale yangekuja baada ya Azimio la Arusha au hata baada ya miaka ya kati ya 70 wakati mapambano ya Kusini mwa Afrika yamepamba moto.
Naweza sema baadae sidhani kama Waingereza waliendelea kuwa na mapenzi na Mwl ingawa mahusiano ya kibalozi yaliendelea. Mwl alikuwa mwiba kwenye makalio ya Mwingereza kwa muda mrefu sana.