Uongozi wa miaka mitano ya urais: Nawakumbuka Nelson Mandela na Dkt. Magufuli, nani anafuatia? Je, ni dhambi kuongoza mhula mmoja?

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
949
2,865
Kwa pamoja tuangalie kama tuna cha kujifunza kutoka kwenye uongozi wa miaka mitano ya urais na historia nzuri waliyoiacha Hayati Nelson Mandela wa Afrika ya kusini,na Hayati Rais John Pombe Magufuli,kumbukumbu za uongozi wao wa miaka mitano na kumbukumbu zao za kiuongozi zisizofutika ni mfano bora wa kuigwa kwa viongozi wengine kwa maslahi mapana ya Taifa, ni heri kutawala na kuongoza kwa miaka mitano lakini ukaacha historia nzuri ya Uzalendo kwa Taifa lako na kwa Jamii yako, leo tunapokumbuka uongozi wa Marais awa wawili ambao wameacha alama katika mataifa yao.

Tujifunze kupitia maisha ya Madiba ambae alikuwa rafiki wa Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,tuangazie harakati zake tukijiweka kwenye nyayo zake Nelson Mandela,je angefanya nini kwenye matukio yanayojiri sasa hapa Tanzania,hususani sakata hili la mkataba wa bandari,Wapo wanaodai Rais Nelson Mandela aling'atuka baada ya kuona changamoto nyingi za kuwaongoza Waafrika kusini, wapo wanaodai Rais Nelson Mandela alishindwa kuumaliza umasikini wa Afrika kusini na hilo ni dalili ya kushindwa kwa sera za Madiba na aliamua kung'atuka na kumuachia Makamu wake, ndugu Thabo Mbeki.

Wapo wanaomtazama Madiba kwa kipindi cha miaka 20 iliyopita na kufikia hitimisho kuhusu legacy yake.

Wapo wanaojaribu kumweka pamoja na viongozi wa kisiasa katika mizani kama jiwe la kupimia na sukari upande mwingine.

Zipo hoja zisizo na takwimu zinazomhukumu Madiba.

Wapo wanaouliza Tata amefanya nini katika kipindi cha miaka 5 ya uongozi kama rais kiasi cha kupewa heshima hiyo ya kushangaza.

Je, Rolihlahla alikuwa mpigani haki na usawa au alibadilika kuwa mamluki wa nchi za Magharibi.

Je, kulikuwa na mkataba kati yake na makaburu wa kulindana baada ya kuachiwa kutoka kifungoni (usaliti)

Je, Khulu ameisadia vipi jamii ya Afrika kusini iliyoishi kwa mateso kwa karne nyingi za ubaguzi wa rangi.

Rejeo la majina ya Hayati Nelson Mandela yaliyotoa taswira kwenye maisha yake,Rolihlahla. Hili lilikuwa jina lake la kuzaliwa, lilikuwa jina la kabila ka Khosa lililokuwa na maana ya kuvunjavunja matawi ya miti.Nelson. Jina hili alipewa na mwalimu wake siku ya kwanza shuleni,Madiba. Hili ni jina la ukoo ambao hayati Mandela alitoka, jina la ukoo lilikuwa na umuhimu mkubwa kuliko na baba mzazi katika utamaduni wa vizazi vya Afrika kusini.Tata. Hili lilimaanisha "Baba" kwa lugha ya kikhosa, Mandela aliitwa jina hilo ikiwa ni heshima kwa kile alichokifanya katika taifa lake,Khulu. Mandela aliitwa Khulu ikimaanisha Mkuu, pia walimuita "Tat'omkhulu" likimaanisha "Babu" kwenye lugha ya kikhosa.Dalibhunga. jina hili alipewa akiwa na umri wa miaka 16 alipotoka jandoni, lilikuwa na maana ya uongozi wa baraza au muongoza mjadala.

Niwakumbushe Watanzania, Tanzania imemwaga damu yake kwenye kupigania Uhuru wa Mwafrika, Tanzania ikiwa mstari wa mbele imepoteza raia wake wengi kwenye kulikomboa bara la Afrika, Tanzania ina heshima kubwa katika Afrika,alipokufa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kuzikwa tarehe 26 Novemba 1999, Mzee Mandela alifunga safari hadi Butima mahali ambapo baba wa taifa alizikwa, alikuja na Ndege ya shirika la ndege la Afrika kusini na kutua katika uwanja wa ndege wa Mwanza kisha alipata usafiri wa helkopta na kwenda Butima kijijini kwa baba wa Taifa kwa ajili ya kwenda kuhani msiba huo wa rafiki yake kipenzi na Mwanamajumui mwenzake na baadae alirejea Mwanza na kupanda ndege kurudi kwao Afrika kusini.

Kwenye msiba wa Rais John Pombe Magufuli, walikuja Marais wote wa Jumuiya ya kusini mwa Afrika SADC, Rais wa Botswana alisema tumempoteza Rais ambae alibeba tochi ya umajumuhi wa Afrika,We have lost a Pan Africanist, na Rais wa Afrika kusini, Cyril Ramaphosa alisema,We have lost a true son of Africa na Rais wa Malawi,alisema "No body knew Magufuli was coming and no body knew Magufuli was going, rest in peace son of Africa, President John Magufuli,Rais John Pombe Magufuli aliongoza kwa miaka mitano lakini alirudisha sifa na heshima ya Julius Nyerere, Nkwame Nkrumah,Jommo Kenyatta,Haile Sellasie,Mnamdi Azikiwe,Edward Mondelane,Samora Mchel na kubeba tochi toka kwa Muammar Ghadafi awa wote, kwetu sisi tuliona kama watu waliowapenda watu wa Afrika nao hawapo tena.

Nimalizie kwa tafakuri Jadidi,Je tuongoze kwa miaka mingi na tuipoteze sifa ya Afrika!? Au tuongoze Muhula mmoja na kuirudisha sifa ya Afrika,naiona tochi ya Hayati Magufuli aliyoichukua toka kwa Muammar Ghaddaf ikirudi tena Afrika Magharibi hususani kwa Rais Ibrahim Traore wa Burkina Faso ambae anataka Afrika ijitawale na uchumi wake,Big up Rais Ibrahim Traore,kwa Burkina Faso wamemvisha kivuli cha Thomas Sankara kwa mienendo yake na matendo yake ni Thomas Sankara ndani ya Ibrahim Traore,hii ni heshima kubwa kwa Thomas Sankara ambae aliuawa na rafiki yake na Makamu wake aliyemuamini sana.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of business administration in International business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publications;-
-Assessment on the Effects of Micro-financing on Poverty Reduction.
 
Back
Top Bottom