Kwanza nikupe pole sana, hizi ndizo gharama za kuutetea ukweli daima. Lakini kumbuka kwenye siasa hakuna rafiki wala adui wa kudumu. Bila wewe na mzee Kinana kuifufua CCM leo tungekuwa tunasema mengine.
USHAURI:
Ninayeandika haya ni kiongozi ndani ya UKAWA, tungekuhitaji sana kwetu na tunakuhitaji sana lakini siyo saa hizi. Kwa jinsi nchi inavyoendesshwa tunahitaji wapinzani ndani ya CCM. Tunawahitaji wengi sana.
CCM inafika mwisho lakini tunataka kifo chake kitoke ndani ili utabiri wa mwalimu ukamilike. Nadhani umenielewa na nitarudi ku-comment chochote baada ya wewe kuonyesha msimamo wako.
Asante