Nape na madai ya uchagga ndani ya CHADEMA

Nape na madai ya uchagga ndani ya CHADEMA

Huu mjadala unaanza kupoteza uelekeo maana kuna watu wanajadili utadhani wamethibitishiwa Mwalimu aliwahi kusema hivyo wakati nijuavyo si kweli. Wanaoamini mwalimu alisema watusaidie kutujulisha hotuba au maandishi yapi yanahusika kama chanzo maana, alipokuwa anapinga ukabila wengi tunazikumbuka hotuba hizo sasa sijui hii ya kukataa makabila fulani aliitoa wapi.
Hapa nchini kuna watu Mwalimu aliwapa nafasi kusoma lakini wao wakaona elimu si dili, leo waliosoma wanapopata nafasi za juu katika sekta mbalimbali za ajira wao wanamlaumu Mwalimu bila kufauatilia historia.
Kila mtu anajua shule nyingi wakati wa ukoloni zilimilikiwa na taasisi za kidini na pengine viongozi wa dini husika wangependa wafuasi wa dini zao pekee ndiyo wasome katika shule hizo. Baada ya uhuru Mwalimu alitaifisha nyingi ya shule hizo ili watanzania wote wasome pasipo kulazimika kubadili dini zao lakini wengine kwa maksudi au kwa kutojua umuhimu wa elimu walipuuza na kuwekeza katika ujenzi wa nyumba za ibada pekee sasa leo ni wachache kati yao wamesoma na wanamlalamikia Mwalimu kwa kupendelea baadhi ya watu katika swala la elimu. Huu ni uongo na ni elimu pekee ndiyo inaweza kuwasaidia watu kupima maelezo yapi ni ya kweli na yapi ni uzushi mtupu.
Mwalimu alipinga ukabila kwa nguvu zote na hakuwa na wakati mchafu wa kuzuia baadhi ya makabila wasipate nafasi ya kutawala nchi hii. Ujinga wa baadhi yetu ni kuamini kwamba maadamu kabila fulani wamesoma basi watapenda urais wakati ukweli ni kwamba wasomi wengi hawana time hiyo isipokuwa baada ya CCMafisadi kuigeuza siasa kuwa ulaji ndiyo tumeanza kuona rundo la maprofesa wanakimbilia siasa.
 
Kwa hiyo wana ccm kupitia kwa Nape mmetangaza vita na wachaga kutoshiriki siasa za nchi hii au wachaga wakiwa ccm ndo sio hatari? mmeanza kuwabagua wachaga, who is next? Wanyakyusa, wasukuma, wakurya? ccm mnapotea kwenye ramani ya siasa za nchi hii taratibu

EXECUTIVE
Ahsante sana ndugu kwa post zako nzito na zenye msingi.
Binafsi hadi nimeogopa baada ya kuisoma ile habari ya Nape,
Niliogopa sababu Mh JK alishasema, asemacho Nape ndicho asemacho yeye (Rais).
Sasa kama Rais wetu amefika huku kwa kweli hii inaogopesha sana na sio kitu cha kushabikia hata kidogo.
Siku 90 walizopeana zimewashinda, wametugeukia watz na kuanza kutugawa kwa kasi hii.
Umehoji kitu cha msingi sana, WHO IS NEXT jamani?
Ujumbe ulio mbele yao (ccm) ni kuwa miaka 50 ya kutukandamiza imewatosha sasa wanataka kutuangamiza kabisa, kitu ambacho watz hatutakubali na tunaenda kuwaondoa kwenye dola.
Ajenda ya msingi kwetu ni ukombozi, haijalishi ukombozi huo unaongozwa na watu gani, kikubwa ni watanzania wenyewe!
 
Kashaga ulishawahi kutuandikia thread ya uongo kuhusu karatu. Nimekushauri mara nyingi utuombe radhi lakini umekaa kimya! Leo umetuletea thread ya ukabila in the name of Mwalimu. Hakuna source ya habari wala data na imekaa kiudaku udaku! Nakushauri ujivue gamba kwa kutuomba radhi ili kurudisha imani yetu kwako. Otherwise hatutakuamini kwa lolote.
Ni ushauri tu.
 
Aissee babangu, ndo kweli Chadema ni chama cha kichagga. Ndo maana wafanya kampeni za mikoa ya Wachagga tu, aissee babaangu. Aissee babaangu, wamekishtukia chadema, aissee babaangu.

hizi post mnaandika mkiwa mnakunya nini?
 
kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikisikia maneno eti mwl Nyerere kipindi fulani alitamka eti kuna makabila fulani hapa Tanzania hayapaswi kupewa nafasi ya kuongoza nchi yetu ya Tanzania,inasemekana aliyataja" LIVE" je kuna mtu mwenye taharifa zozote kuhusiana na hilo? kwavile JF ni sehemu ya ma great thinkers na wanazuoni mbalimbali,nategemea tutapata majibu ya kuridhisha kuhusiana na uvumi huu


Kashaga Nyerere alisema hivi (naomba kunukuu)
"Hatutamkataa mtu kwa sababu ya kabila lake lakini hatutamchagua mtu kwa sababu ya kabila lake." Vivyo hivyo, "haitatusaidia kumkataa mtu kwa sababu ya dini yake wala kumchagua mtu kwa sababu ya dini yake". Mwisho wa kunukuu.Mungu ilaze roho ya marehemu pahala pema peponi -AMINA.
Naomba uleje hoja za walio 'hai' maana mpambano wa ulioko sasa si juu ya nini marehemu alisema au hata kutenda, ila juu ya usanii wa watu walio hai.
 
Nape ameonesha kushindwa nafasi ya propaganda, na si yeye tu hata Tambwe Hiza alishindwa maana alikuwa na hasira sana japo muda mwingine alijifanya kutabasamu maliciously. Nape amenyooshewa mti mkavu na yeye akaukamata bila kujali kama una miba au ni smooth. Kitendo cha CHADEMA kuweka wazi kuwa alitaka kujiunga CHADEMA kwa sharti la kuwa mgombea wa jimbo la UBUNGO wakamtosa lilimfanya NAPE ashindwe kufikiria na kujikuta anaropoka kuwa ni CHADEMA ni chama cha wachaga. Kwa mtu anayeshikilia nafasi kubwa katika chama tawala kama yeye ajue tayari ameshageuka gamba gumu sana kwa chama chake ambacho hakina budi kulichuna tena. Maana anaweka wazi kuwa waasisi wa siasa za kutugawa watanzania ni CCM japo huko nyuma hakuna kiongozi wa juu wa CCM aliyewahi kutamka hivyo hadharani na kutumia mamluki kupenyeza hoja. Hii inahitimisha dhana kuwa CCM inawagawa watanzania kwa kutumia ukabila, ukanda, udini, rangi ili mradi tu iendelee kutawala kwa vyovyote.
 
  • Thanks
Reactions: 911
Hata kama alisema,hayo mambo ni irrelevant kwa sasa.Uwezo wa mtu haupimwi kwa kabila wala dini.
 
Nyie sasa mwaleta ukabila humu ndani, siasa zenu majitaka!
 
Lakini
Regia Mtema , mbunge wa viti maalum , aliposema ccm inaongozwa na koo tano, mbona hamukukasirika kama leo? leo yule mnyama mwizi wa asali amejapa ktk muzinga wa nyuki nini?

Si dhani kama alichokianzisha Nape unakielewa. Subiria mziki wake ndio utajua. Nahisi anampango wa kutokugusa kilimanjaro. Kumbuka Nape kuwakataa Wachaga na kawatukana Mapadre eti hawana maadili. Ukiangalia mlolongo huu utaona ni mwendelezo wa CCM wa kubagua watu wake na kuwatusi.

Swali je CCM inawachama wachaga? kama wapo na uongozi wa juu unausema hauwezi kukaa nao wala kufanya nao kazi unawaambia nini hawa wananchama? Na kesho ni nani au ukanda gani utatengwa, kumbuka umoja wa vijana wa CCM pwani nao walitenga baadhi ya kanda na mikoa kwenye uraisi 2015. je Nape kafanya ajali au ni maelekezo ya boss wake?
 
JMushi1, pole kwa vile umejibui kwa hasira. Niliwahi toa ombi kwa wana jf, tunawajibika kutunza heshima ya jf kwa kutumia lugha ya staha na kuepuka matukano. Maneno kama nyie wapuuzi sana, Nape you are stupid, for sure i hate your, desparate like a prostitute etc, ertc. Kwani hatuwezi kubishaja kwa hoja tuu bila kutukana?.

Nawaombeni msameheni Nape, amekuwa mkweli kwa kutoa yale ya ndani kabisa jikoni kwa kuteleza ulimi.
wengi wana hasira na Nape huku silently ndani ya mioyo yao, wanajua wazi kuwa kuna makabila fulani yako sidelined kuwa kamwe hawawezi kushika urais wa nchi hii, no matter how good they might be!. Alichokifanya Nape ni kuteleza tuu ulimi kwa kuusema ukweli huo hadharani!. Please lets not deal na Nape aliyeusema ukweli huo, lets face the problem na tuing'oe the root cause ya tatizo hili, lipo kiukweli na mwanzilishi sio Nape!, yeye amelisemea tuu na huu ni moja ya uthibitisho wa hoja kama hizi, ndizo huwa zinazungumza kwenye corridors za ndani za chama chao, Nape kawa muwazi zaidi katudokeza, sio mtu wa kumlaani bali kumshukuru kutujuza!.

Kwa vile Nape ni memba humu, naamini he is bold enough kuja humu kutufafanulia, alimaanisha nini.
Sasa kama ni kweli alisema hayo hapo chini,then nani achangamane na wapuuzi?Sasa kuchochea ukabila si upuuzi?Kama ana sababu zake za kutochangamana na wachagga,na wachagga nao wasiwe na sababu zao?Sababu yangu mimi ndiyo hiyo.Sababu yake yeye ndo matusi yenyewe.Mimi si mwanachama wa chama chochote cha kisiasa Tanzania.However kama ameleta shutma,basi awe na vigezo alivyotumia,na aviainishe.Hayo mambo ya corridors za chama cha kina nani?chadema ama ccm?Halafu unasema eti Nape ameteleza ulimi kwamba wachagga hawatatawala Tanzania?Go straight to the point usimung'unye.Ila kwa taarifa yako,wananchi ndo wenye kuamuwa nani atawale na siyo hao uliowataja.Wanaweza kuzuia haki ya watanzania sometimes lakini haitawezekana all the time.Naona unazidi kudhihirisha kuwa uchakachuaji ulikuwepo kwa sababu ulizozitaja ndugu mwandishi?
1: Kwamba Wachaga siyo watu wa Kuchangama nao ndio maana Hakujiunga CHADEMA kwa sababu aliamini ni Chama cha WACHAGGA
 
Heh he
Kuhusu Regia hakutaja mafisadi, alitaja koo tano ndizo zinaoongoza ccm , the same way kama alivyotaja wachanga wanaongoza CHADEMA. Tofauti ni kwamba wenda ktk koo zile 5 hukuwemo ama hawakuwemo lakini naamini walikuwemo waliumia sana kama wewe ama yule anayeumia leo kwa kuwemo.

Tatizo ni ukipenda siasa za kutajana tajana lazima nawe ukubali kutajwa either the case, kwa kusingiziwa ama kwa ukweli. sio mimi muasisi wake bali ni Newton third law.

Niambie tofauti ya koo na kabila, kwa jinsi ninavyofahamu koo inaweza kuwa kabila pia.
Mkamap,elewewa tofauti kati ya "Koo" na "Kabila" Unaweza kuwa kabila moja na koo tofauti.At the same time unaweza kuwa na koo tofauti na makabila tofauti lakini mkawa tabaka moja.Hizo koo tano maybe ni tabaka linalotawala Tanzania kwa muda wote toka tupate uhuru na kama unataka kupima walicholifanyia Taifa,then angalia maisha ya mtanzania wa kawaida.
Kwa upande wa Nape,napenda kusema kwamba amechemsha.Aliposema chadema ni chama cha wachagga alitumia vigezo gani?Siyo kwamba napinga anachosema as if haki exist.Ila siwezi kuamini coz sioni ni vigezo gani ametumia na pia naamini anapanda sumu mbaya ya ku divide Taifa.Kama amesoma basi anajuwa lazima uje na facts kuback up hoja yako.Pia amesema ni chama cha ukoo.Ningependa aseme ni ukoo gani.Halafu unapolinganisha ccm na cdm,basi kuna standards zake kwasababu kimojawapo kimetawala toka uhuru na kingine ni chama kichanga tu.Heavy weight si sawa na light weight.Kwahiyo kwa wale wenye nia ya dhati na mageuzi ya watanzania,basi maneno ya Nape ni kama pumba tu. Unless atuwekee facts hapa.
 
Tatizo sio utani, tatizo ni kwamba Regia Mtema alisisitiza sana kwamba ccm ni koo tano ndo zinaongoza lakini sikuona watu kujadili kwa hamasa namna hii na kuilaani kauli hiyo vikali. Na je kauli ya Regia ilikuwa haichochei watanzania kuichukia koo hizo alizozitaja?

Hao ama koo hizo sizitetei, lakini huyu dada na mbunge wa chadema alikuwa anajenga chuki ya hatari zaidi ktk koo hizo, tena unaweza kuta ktk koo hizo kuna walalahoi ambao wanaombea mabaya kila siku viongozi waliotoka ktk koo zao, sasa kuwajumuisha nao ni kauli jumulishi sana. Ambayo nayo ilitakiwa kukemewa vikali, kama kweli watu wanapigania masilahi ya Taifa na si masilahi wezeshi binafsi.

Nonetheless, yawezekana kabisa hizo koo ni coincidence kuwa ndani ya ccm kama ilivyo coincidence ya wachaga kuwa wengi ktk uongozi wa CHADEMA.

Sitaki kuamini kama mtu anaweza kukimea kauli ya Nape na kui- bypass kauli ya Mtema na kinyume chake pia ni sahihi.

Kwa hiyo una maanisha kuwa kwa kuwa Regia Mtema alisema hilo basi ni jambo zuri kusemwa na mtu mwingine yeyote na hata wa kutoka chama tawala. Je si zaidi kwa chama tawala kuwa makini na kauli zinazotolewa na viongozi wake kuliko vyama vya upinzani ambavyo vipo kuichachafya serekali na chama kinachotawala hata kwa kusema uongo? Na je si zaidi kwa CCM kuwa makini na kauli na matendo ya viongozi na wanachama wao zaidi sasa wakati kinatafuta kuaminiwa tena na watanzania?

Koo tano zinaweza kutoka sehemu mbalimbali za nchi, na kabila tofauti, lakini ukisema kabila fulani, au dini fulani, unaingia kwenye issue kubwa zaidi. Koo zinahushishwa zaidi na usultani, na hilo ndilo linaloelekea kutokea katika utawala wa ccm, waliopo madarakani kuwaandaa vijana wao kuja kushika uongozi wa nchi, na nadhani hilo haliwezi kuamsha hasira mbaya dhidi ya hizi koo kwa kuwa sio ukoo mmoja. Kulinganisha koo na kabila unahitaji uwe makini zaidi kwani unaweza kufikia suluhisho ambalo si kweli katika uchambuzi wako.

But ukisema kabila moja say Wahaya tayari unasandwitch koo zoote zilizopo katika kabila hilo kwenye kapu moja. Na kusema kuwa huwezi kujiunga na kikundi fulani kwa kuwa ni cha kabila fulani, then huko ni kulibagua lile kabila. South Africa walio wengi wa chama cha ANC ni waafrika weusi, wale makaburu hawako ANC na huo ni ubaguzi na tunajua. Tuseme Nape angejiunga na CDM kama kisingekuwa na wachagga?

Kwa sababu kama hoja ni utaifa, CDM kina sura ya kitaifa, kweli kina chimbuko lake toka Kaskazini kwa kuwa mwanzilishi alikuwa mtu wa kutoka kaskazini, lakini alijitahidi kukipa sura ya kitaifa. Sote tutakubali hilo kwani Ndugu Mtei alimuachia Bob Makani - Msukuma uenyekiti wa chama. Na sasa CDM imeenea nchini kote bara na visiwani.

Najua kuna vijembe kwenye siasa, but ukileta vijembe kwenye sensitive issues kama ya udini au ukabila ndani ya siasa si tu kuwa unakosa hekima bali unahatarisha mshikamano na utengano wa taifa. Nape hapa amefail kama kiongozi kwani amekosa busara na uchambuzi wa kauli zake.

Mwalimu nyerere alishasema kuwa ukianza ubaguzi wa "wabara" na "wazanzibari" hutaishia hapo tu, "dhambi" ya ubaguzi itakutafuana, utaanza kuwabagua "waunguja" na "wapemba" na utashuka hadi ubague nyumba hadi nyumba na labda kitanda hadi kitanda, and who knows shuka hadi shuka.

Maneno hayo ya kibaguzi nadhani yasingepashwa kutoka katika mdomo wa mtu aliyapewa jukumu la kuirejeshea CCM imani kwa wananchi. Nape amefanya yaliyotokea Dodoma kuwa upuuzi, kwa kuwa ameonyesha kuwa CCM haikuwa makini katika kubadilisha uongozi wake, au CCM imesihiwa viongozi wenye mvuto kwa watanzania. Sijui wazee wa CCM kama kina Kisumo, Lusinde, Msuya, Warioba, Salim, Mwinyi Mkapa etc wako wapi kukemea kauli chafu kama hizo zinazoonekana kubomoa misingi imara na tunu za taifa letu!!
 
Ni hatari kwa taifa kwa wanasiasa kuingiza mambo ya ukabila na dini katika siasa, tujifunze toka kwa wenzetu rwanda kenya nk. Kwa hiyo wale wote wanasiasa wanaohubiri udini, ukabila na sasa uzanzibari na utanganyika wakome kabisa, mambo yakiharibika hatutasita kuwashtaki katika mahakama za jinai za umoja wa mataifa. HILO NA WALIZINGATIE.
 
I have to admit that I'm really disappointed, I mean more than disappointed kama haya ndiyo matumaini yenyewe basi nikazi.
 
ukiona mwanasiasa ameshindwa kuwashawishi wananchi na anaelekea kufilisika kisiasa hukimbilia kwenye hoja dhaifu kama udini, ukadila, rangi, jinsia n.k ccm wamefilisika hawana ambacho wananchi watawaelewa tena hivyo wanajaribu kuwashawishi wananchi katika hoja za ukabila. bye bye ccm
 
Back
Top Bottom