Nape na madai ya uchagga ndani ya CHADEMA

Nape na madai ya uchagga ndani ya CHADEMA

Hivi nikitaja viongozi wa ccm mkoa wa Mtwara ama Tanga nikasema ccm ni ya wadigo ama wamakonde nitakuwa right?Wekeni ushahidi wa ku convince.

Hiyo orodha sio ya Chadema mkoa ni Chadema Taifa wamejazana wachaga tupu!
 
Yeye kama kiongozi wa chama hakutakiwa kuingia kwenye mtego na kuanza kuwadhalilisha wachaga, sasa yeye na kabila lake ni nini cha ajabu wameifanyia Tanzania kuliko wachaga? Huyu anatakiwa siyo kuomba samahani tu bali NEC inatakiwa imfukuze haraka saana ni sumu mbaya kuanza kutoleana kidole kwa ukabila.
 
Hiyo orodha sio ya Chadema mkoa ni Chadema Taifa wamejazana wachaga tupu!

Rais : Jakaya Mrisho Kiwete
Makamu wa Rais: Mohamed Ghalib Bilal
Makamu wa Pili wa Rais: Mohamed Shein
Makamu wa Tatu wa Rais: Seif Sharif Hamad
Makamu wa Nne wa Rais: .............
Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa:
Jaji Muu....

Ningekuwa nina Akili kama za Nape au Zako Basi Ningesema kwamba Hii Serikali ni ya Kiislam
 
Sasa viongozi mgondo na waliofilisika, wavivu wa kufikiri na wanaotamani damu wameanza rasmi kuligawa taifa kwa tabaka za kikabila. Nape kwa kuwadharau wachaga na kuwatolea mfano wa watu wa kukataliwa na kutengwa anamaanisha nini? Ana tofauti gani na kaburu wa Afrka kusini huyu? Hawa ndio watu Nyerere aliosema tuwaogope kama ukoma. Maana chizi mwenye mtizamo wa kibaguzi hana mda mrefu kusababisha umwagaji wa damu. Nape nakushauri uitishe mkutano na waandishi wa habari na kuombe radhi kwa kuwatukana wachaga. Laa sivyo pamoja na kwamba RACHEL wanakuwinda kwa kuwanyanyapaa dhidi ya mafisadi wengi wa ccm, naamini wachaga watakuwinda kwa hamu zaidi ili kuondoa uovu huu wa kibaguzi ndani ya ardhi ya Tanzania. Hawatavumilia kamwe ifikie hali kama iliyopo mashariki ya kati dhidi ya Wayahudi na wapalestina.
Ccm naona mmedhamiria kuiingiza nch katika vita ya wenyewe kwa wenyewe, kumbukeni ubaguzi ulioazimiwa katika mkutano wa Uv-ccm Pwani, ya kuwabagua watu kwa ukanda wanaotoka.
Msipojirekebisha mtaliangamiza taifa baada ya kuiangamiza serikali chini ya Rais dhaifu Jk.
.
 
Mimi si mtoa hoja sana kwenye hii tovuti, lakini ni mzuri wa kusoma na kufuatilia.
Kwanza sikubaliani na suala la kuanzisha topic za ukabila, kwa hili ninawaunga mkono wanaozipinga, lakini pia sikubaliani na kikundi kidogo cha watu wanaoonyesha hali ya kutawala kundi kubwa kwa kutumia ukabila.

Hili nalo nakubaliana na wale wanaopinga kundi la watu wachache kutoka kabila fulani kutaka kuendesha kundi kubwa la kabila mchanganyiko. Tusipofuta dhana hii na vitendo hivi, basi mwelekeo wetu wa kusaidia nchi yetui ni batili.

Jambo la pili, tujadili issues hapa bila majazba, maana kwanza hatuonani na hatujuani ila tunawasiliana tu kupitia chombo hiki kujaribu kuiweka sawa nchi yetu. Matusi na maneno ya kejeli mara nyingi huzaa ugomvi.

Hapa naona kuna member wengi wa chadema, ndio mara nyingi naona wanaweka hoja na kuzijibu pia. Ila tatizo langu ni kuwa kila lisemwalo na mtu ambaye si chadema linapingwa vikali sana na wala halipewi nafasi ya kujadiliwa.

Sasa hiyo si demokrasia, kuna mambo yanaongelewa na watu wa ccm, ni mazuri na yana ukweli hamna haja ya kuyapinga, lakini pia kuna mabaya yanafanywa na cc, hayo nayo inabidi kuyapinga vikali kwa hoja.

Vilevile kwa upande wa chandema sio kwamba wao ni malaika, kuna hoja nyingine zinatolewa kuhusu mambo mabaya ya chadema, na zina ukweli kwa hiyo ni lazima zijadiliwe, pia kuna zile ambazo zinatolewa kwa uzushi, hizo nazo zipingwe kwa hoja.

Tuache hiyo kasumba kwa kupinga kila kitu kinachosemwa na mpinzani wako, tuchukue ule ukweli tuufanyie kazi sawasawa, na ule uongo wala tusijali.

Ninaanzia hapo, na naomba anayetaka kujibu, basi ajibu kwa hoja, sio matusi na kejeli.

Hapa si mahala pa kuvunjiana heshima, bali ni sehemu safi sana ya kujifunza yanayoendelea nchini kwetu na pia kuibua mikakati ya kusaidia.

Mkuu,
hapo nilipokoleza na kupigia mstari naomba maelezo zaidi..hii itasaidia kupunguza manung'uniko dhidi ya chama kilichojipambanua hivi majuzi kama chama cha magamba
 
Nimeshindwa kuelewa unasema nini? Jambo alilosema Nape ni la kijinga na linabidi kupingwa na kila mtu mwenye akili timamu. Hizi chuki za dhahiri zinazojengwa juu ya kabila fulani ni mbaya kwa nchi yetu. Kusema CHADEMA ni chama cha Wachagga ni uongo mkubwa! CHADEMA imeshinda viti Kigoma, Mwanza, Mbeya, Dar es Salaam sehemu ambazo wakazi wake sio wa kabila tajwa.

Pili, kuna chuki ambazo zinajengwa juu ya watu wa Kaskazini kitu ambacho sio chema kabisa. Sikutegemea maneno kama hayo kunatolewa na Katibu wa Chama Tawala, kitu tunachotakiwa kujiuliza leo kawasema Wachaga kesho atawasema kina nani? Kwani hii ni kama Slippery slope, ukishaanza kutereza basi....
 
Nape Nauye hafai hata kwa tambiko, sishangai sana maana ccm yote akili zao zinafanana na nape anaicheza zaidi ngoma ya CHADEMA kuliko babu yake mlezi Makamba. Akitia maguu Moshi atajuta kuijua ccm.
 
Mhhh mbona watu wamekuwa wakali sana, yawezekana kuna ukweli ndani yake

Kwa hiyo unaamini yawezekana;

  • Wachaga walioko CCM wanajipendekeza, kwa nani ?
  • Wasio Wachaga walioko Chadema nao wanajipendekeza, kwa nani ?
  • Anayosema Nape Nnauye ndio msimamo wa Kikwete na CCM.
  • Serikali ya CCM kwa kuisajili Chadema ina sera ya ubaguzi wa kikabila, kwa faida ya nani ?
  • Wachaga walioko CCM ndio wanaichafua kwa ufisadi hivyo waondoke.
  • Kiwete kwa kupitia msemaji wake wa chama anatangaza vita dhidi ya Wachaga.
  • Ndio maana serikali ya CCM haikusita kuwapiga risasi na kuwaua watu Arusha.
  • Nape Nnauye ndiye mjumbe mwafaka aliyetumwa kueneza chuki ya kikabila dhidi ya Wachaga.
  • kumbe.................................................................................n.k.
Mkamap, kuna mambo unaweza ukayafanyia utani katika kuyajadili lakini si hili la huyu kijana anayeonyesha wazi kuchanganyikiwa. Katika hili CCM inatakiwa kutoa tamko rasmi la kulaani kwa nguvu zoote huu upuuzi na uropokaji wa Nape na wala si Chadema kukanusha. Hili halitamalizika kimya kimya kama ilivyokuwa kuropoka kwa Nauye kuhusu mapacha watatu na siku 90, la hapana, hili halifagiliwi chini ya meza. Na kwa usalama CCM tamko lisipotolewa mapema la kuwaomba radhi Wachaga, linaweza kuleta madhara makubwa kwa serikali na taifa kwa ujumla.
 
Kwanza Kabisa nikiri kwamba Sifahamu Kabila la Nape Nnauye, silifahamu kwa Sababu hata siku moja sikuwahi kufikiri kwamba Kabila la Mtu laweza kuwa Kigezo cha Mtu kuongoza au Kujiunga na Chama au Kuajiriwa na Taasisi

Nape Ametukana Wachagga

1: Kwamba Wachaga siyo watu wa Kuchangama nao ndio maana Hakujiunga CHADEMA kwa sababu aliamini ni Chama cha WACHAGGA.

2. Kwamba Ili Uwe CCM ni Lazima kwanza Usiwe Mchagga, kwamba Wachaga wa CCM wanajipendekeza

Hayo ni Maneno yaliyotoka Kinywani Mwa Kiongozi wa Juu wa CCM ( Chama kinachotawala) Ambaye Mwenyekiti wake alsema kwamba Linasemwa na Nape ni Lake ( yeye Mwenyekiti)

Nape Unaweza kuja clear na Kueleza ni nini Hasa hawa Watanzania Wenzetu wamekukosea?

Je WACHAGGA wakiamua Kurevenge Utaweza kweli kuhimili?

Je huna Mpango wa Kwenda Moshi kuvua Magamba Chama Chako?

Je Uko Tayari Kuwaomba radhi WACHAGGA wote?

Pole Nape Vita uliyoianzisha unaifanya kuwa Ngumu sana

Kwa bahati mbaya au kwa makusudi hapo kwenye red ameacha haya yafuatayo kwani ndivyo hata makuwadi wa chama chake wanavyotaka kuaminisha watanzania:-

3. Watu wa dini ileee sio wa kuchangamana nao, hakujiunga CHADEMA kwa kuwa aliamini (kama ambavyo makuwadi wa CCM pia wanavyotaka kutuaminisha) ni chama cha watu wa dini ile ambayo sio yake. Hata Kiongozi wa dini yake si alisimama hadharani kuonya watanzania?

4. Watu wa kanda ileee sio wa kuchangamana nao pia. Kulee kaskazini mwa nchi yetu (yako makabila kibao na dini zote), si CHADEMA ni cha huko?

Kwa nini analeta vitu nusunusu? Amalizie kabisa, watanzania tutamwelewa. Asipokuwa makini ataharibu badala ya kukijenga chama chake.
 
Tumewazoea hawa wanaojifanya wakubwa. Muda s mrefu ataibuka na kusema alinukuliwa vibaya!!! Subirini mtasikia
 
Kweli nyie wapuuzi sana,.Nape you are stupid and for sure i hate your stance,and ways of thinking.Why be desparate like a prostitute kama unalipenda Taifa and you are young?This aint the way to go.Nape you are a member in here.Nadhani huna ujasiri tena wa kulog in na kujibu hoja coz unajuwa mmeishiwa hoja na sasa mnaleta viroja.
JMushi1, pole kwa vile umejibui kwa hasira. Niliwahi toa ombi kwa wana jf, tunawajibika kutunza heshima ya jf kwa kutumia lugha ya staha na kuepuka matukano. Maneno kama nyie wapuuzi sana, Nape you are stupid, for sure i hate your, desparate like a prostitute etc, ertc. Kwani hatuwezi kubishaja kwa hoja tuu bila kutukana?.

Nawaombeni msameheni Nape, amekuwa mkweli kwa kutoa yale ya ndani kabisa jikoni kwa kuteleza ulimi.
wengi wana hasira na Nape huku silently ndani ya mioyo yao, wanajua wazi kuwa kuna makabila fulani yako sidelined kuwa kamwe hawawezi kushika urais wa nchi hii, no matter how good they might be!. Alichokifanya Nape ni kuteleza tuu ulimi kwa kuusema ukweli huo hadharani!. Please lets not deal na Nape aliyeusema ukweli huo, lets face the problem na tuing'oe the root cause ya tatizo hili, lipo kiukweli na mwanzilishi sio Nape!, yeye amelisemea tuu na huu ni moja ya uthibitisho wa hoja kama hizi, ndizo huwa zinazungumza kwenye corridors za ndani za chama chao, Nape kawa muwazi zaidi katudokeza, sio mtu wa kumlaani bali kumshukuru kutujuza!.

Kwa vile Nape ni memba humu, naamini he is bold enough kuja humu kutufafanulia, alimaanisha nini.
 
acheni kupotosha maneno aliyoongea NAPE jamani,haya maandishi yatakuja kutumaliza watanzania bila sababu,nahisi wote mmeshaona mwandishi wa habari wa kenya aliyeko the heague now,mauaji ya rwanda yalivyochangiwa na "kalamu" mnachofanya ni kuexaggerate aliyoongea Nape ili Wachaga wamchukie and that is a very dangerous propaganda! shame on you
 
kuna fununu eti NYERERE alitamka kuna baadhi ya makabila,nasikia aliyataja eti hayapaswi kupewa NCHI je kuna ukweli wa hili?
 
Tunashukuru kwa ufafanuzi huu lakini wenye akili wanajua kwamba Sekretarieti ni sehemu ndogo tu ya mfumo wa uongozi wa chama. Tupewe orodha ya wajumbe wa Kamati Kuu, Halmashauri/Baraza Kuu, pamoja na orodha ya wabunge wa viti maalum na uhusiano wao na viongozi wakuu wa chama waliopo na wale wastaafu. Maana dhambi hapa siyo ya ukabila tu, hata nepotism ni issue ambayo inalalamikiwa sana na ni sehemu ya Ufisadi. Tuambiwe mahusiano ya baadhi ya wabunge wa vitu maalum na viongozi wafuatao:

1. Zitto Kabwe,
2. Tundu Lissu,
3. Philemon Ndesamburo,
4. Wilbroad Slaa,
5. Freeman Mbowe.

Tuambiwe pia uhusiano wa Anna Komu na viongozi wakuu wa chama.
 
Nimeshindwa kuelewa unasema nini? Jambo alilosema Nape ni la kijinga na linabidi kupingwa na kila mtu mwenye akili timamu. Hizi chuki za dhahiri zinazojengwa juu ya kabila fulani ni mbaya kwa nchi yetu. Kusema CHADEMA ni chama cha Wachagga ni uongo mkubwa! CHADEMA imeshinda viti Kigoma, Mwanza, Mbeya, Dar es Salaam sehemu ambazo wakazi wake sio wa kabila tajwa.

Pili, kuna chuki ambazo zinajengwa juu ya watu wa Kaskazini kitu ambacho sio chema kabisa. Sikutegemea maneno kama hayo kunatolewa na Katibu wa Chama Tawala, kitu tunachotakiwa kujiuliza leo kawasema Wachaga kesho atawasema kina nani? Kwani hii ni kama Slippery slope, ukishaanza kutereza basi....

Ni kweli tuipinge hii kauli na je kwanini unaona tuiunge kauli ya Regia Mtema kwamba ccm ni ya koo tano na je hii ni kauli sahihi. sikusikia mkiilaani kauli hiyo.
 
kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikisikia maneno eti mwl Nyerere kipindi fulani alitamka eti kuna makabila fulani hapa Tanzania hayapaswi kupewa nafasi ya kuongoza nchi yetu ya Tanzania,inasemekana aliyataja" LIVE" je kuna mtu mwenye taharifa zozote kuhusiana na hilo? kwavile JF ni sehemu ya ma great thinkers na wanazuoni mbalimbali,nategemea tutapata majibu ya kuridhisha kuhusiana na uvumi huu
 
acheni kupotosha maneno aliyoongea NAPE jamani,haya maandishi yatakuja kutumaliza watanzania bila sababu,nahisi wote mmeshaona mwandishi wa habari wa kenya aliyeko the heague now,mauaji ya rwanda yalivyochangiwa na "kalamu" mnachofanya ni kuexaggerate aliyoongea Nape ili Wachaga wamchukie and that is a very dangerous propaganda! shame on you
Poor you pole unalaumu risasi ilipotua badala ya kumlaumu aliyefyatua.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Kwa hiyo unaamini yawezekana;

  • Wachaga walioko CCM wanajipendekeza, kwa nani ?
  • Wasio Wachaga walioko Chadema nao wanajipendekeza, kwa nani ?
  • Anayosema Nape Nnauye ndio msimamo wa Kikwete na CCM.
  • Serikali ya CCM kwa kuisajili Chadema ina sera ya ubaguzi wa kikabila, kwa faida ya nani ?
  • Wachaga walioko CCM ndio wanaichafua kwa ufisadi hivyo waondoke.
  • Kiwete kwa kupitia msemaji wake wa chama anatangaza vita dhidi ya Wachaga.
  • Ndio maana serikali ya CCM haikusita kuwapiga risasi na kuwaua watu Arusha.
  • Nape Nnauye ndiye mjumbe mwafaka aliyetumwa kueneza chuki ya kikabila dhidi ya Wachaga.
  • kumbe.................................................................................n.k.
Mkamap, kuna mambo unaweza ukayafanyia utani katika kuyajadili lakini si hili la huyu kijana anayeonyesha wazi kuchanganyikiwa. Katika hili CCM inatakiwa kutoa tamko rasmi la kulaani kwa nguvu zoote huu upuuzi na uropokaji wa Nape na wala si Chadema kukanusha. Hili halitamalizika kimya kimya kama ilivyokuwa kuropoka kwa Nauye kuhusu mapacha watatu na siku 90, la hapana, hili halifagiliwi chini ya meza. Na kwa usalama CCM tamko lisipotolewa mapema la kuwaomba radhi Wachaga, linaweza kuleta madhara makubwa kwa serikali na taifa kwa ujumla.

Tatizo sio utani, tatizo ni kwamba Regia Mtema alisisitiza sana kwamba ccm ni koo tano ndo zinaongoza lakini sikuona watu kujadili kwa hamasa namna hii na kuilaani kauli hiyo vikali. Na je kauli ya Regia ilikuwa haichochei watanzania kuichukia koo hizo alizozitaja?

Hao ama koo hizo sizitetei, lakini huyu dada na mbunge wa chadema alikuwa anajenga chuki ya hatari zaidi ktk koo hizo, tena unaweza kuta ktk koo hizo kuna walalahoi ambao wanaombea mabaya kila siku viongozi waliotoka ktk koo zao, sasa kuwajumuisha nao ni kauli jumulishi sana. Ambayo nayo ilitakiwa kukemewa vikali, kama kweli watu wanapigania masilahi ya Taifa na si masilahi wezeshi binafsi.

Nonetheless, yawezekana kabisa hizo koo ni coincidence kuwa ndani ya ccm kama ilivyo coincidence ya wachaga kuwa wengi ktk uongozi wa CHADEMA.

Sitaki kuamini kama mtu anaweza kukimea kauli ya Nape na kui- bypass kauli ya Mtema na kinyume chake pia ni sahihi.
 
Back
Top Bottom