Kwa hiyo una maanisha kuwa kwa kuwa Regia Mtema alisema hilo basi ni jambo zuri kusemwa na mtu mwingine yeyote na hata wa kutoka chama tawala. Je si zaidi kwa chama tawala kuwa makini na kauli zinazotolewa na viongozi wake kuliko vyama vya upinzani ambavyo vipo kuichachafya serekali na chama kinachotawala hata kwa kusema uongo? Na je si zaidi kwa CCM kuwa makini na kauli na matendo ya viongozi na wanachama wao zaidi sasa wakati kinatafuta kuaminiwa tena na watanzania?
Koo tano zinaweza kutoka sehemu mbalimbali za nchi, na kabila tofauti, lakini ukisema kabila fulani, au dini fulani, unaingia kwenye issue kubwa zaidi. Koo zinahushishwa zaidi na usultani, na hilo ndilo linaloelekea kutokea katika utawala wa ccm, waliopo madarakani kuwaandaa vijana wao kuja kushika uongozi wa nchi, na nadhani hilo haliwezi kuamsha hasira mbaya dhidi ya hizi koo kwa kuwa sio ukoo mmoja. Kulinganisha koo na kabila unahitaji uwe makini zaidi kwani unaweza kufikia suluhisho ambalo si kweli katika uchambuzi wako.
But ukisema kabila moja say Wahaya tayari unasandwitch koo zoote zilizopo katika kabila hilo kwenye kapu moja. Na kusema kuwa huwezi kujiunga na kikundi fulani kwa kuwa ni cha kabila fulani, then huko ni kulibagua lile kabila. South Africa walio wengi wa chama cha ANC ni waafrika weusi, wale makaburu hawako ANC na huo ni ubaguzi na tunajua. Tuseme Nape angejiunga na CDM kama kisingekuwa na wachagga?
Kwa sababu kama hoja ni utaifa, CDM kina sura ya kitaifa, kweli kina chimbuko lake toka Kaskazini kwa kuwa mwanzilishi alikuwa mtu wa kutoka kaskazini, lakini alijitahidi kukipa sura ya kitaifa. Sote tutakubali hilo kwani Ndugu Mtei alimuachia Bob Makani - Msukuma uenyekiti wa chama. Na sasa CDM imeenea nchini kote bara na visiwani.
Najua kuna vijembe kwenye siasa, but ukileta vijembe kwenye sensitive issues kama ya udini au ukabila ndani ya siasa si tu kuwa unakosa hekima bali unahatarisha mshikamano na utengano wa taifa. Nape hapa amefail kama kiongozi kwani amekosa busara na uchambuzi wa kauli zake.
Mwalimu nyerere alishasema kuwa ukianza ubaguzi wa "wabara" na "wazanzibari" hutaishia hapo tu, "dhambi" ya ubaguzi itakutafuana, utaanza kuwabagua "waunguja" na "wapemba" na utashuka hadi ubague nyumba hadi nyumba na labda kitanda hadi kitanda, and who knows shuka hadi shuka.
Maneno hayo ya kibaguzi nadhani yasingepashwa kutoka katika mdomo wa mtu aliyapewa jukumu la kuirejeshea CCM imani kwa wananchi. Nape amefanya yaliyotokea Dodoma kuwa upuuzi, kwa kuwa ameonyesha kuwa CCM haikuwa makini katika kubadilisha uongozi wake, au CCM imesihiwa viongozi wenye mvuto kwa watanzania. Sijui wazee wa CCM kama kina Kisumo, Lusinde, Msuya, Warioba, Salim, Mwinyi Mkapa etc wako wapi kukemea kauli chafu kama hizo zinazoonekana kubomoa misingi imara na tunu za taifa letu!!