Nape na madai ya uchagga ndani ya CHADEMA

Nape na madai ya uchagga ndani ya CHADEMA

Nimekwambia ni kweli kwa mujibu wa swali lako. Umeuliza "eti kuna fununu ...", ni kweli kuna fununu lakini Mwalimu Nyerere hakuwahi kutaja kabila lolote. Kwa kuwa IQ yako ni zero utaendelea kuishi kwa fununu. Fanya utafiti acha kuleta umbea wa mtaani hapa! Mwalimu hakuwa mjinga kama wewe na makuwadi wenzako; aliitazama Tanzania kama Tanzania na sio propaganda zenu muflisi.
wadau watanisaidia sasa sijui mi na wewe nani ni zoba au ana IQ ZERO coz kwenye hii thread hakuna sehemu niliyisema neno "FUNUNU" au kusoma ni ishu mzee wa ubaoni?? so jipange kwanza acha kukurupuka mzee
 
Kama hamtaki kabila langu litoe kiongozi basi msije kutawala hata eneo langu, ni bora turudi kwenye enzi za kina Mkwawa.
 
Pipozzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzz Poweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeer, wawe wachaga au vinginevyo mkoa unaongoza kwa wabunge wengi wa CDM ni Shinyanga wako 4 na 1 viti maalum Mwanza 3 na 1 Vit maalum, sisi (Natokea huko) siyo wachaga ni bashosha ng'ombe huo ni msamiati wa kale Nape atafute msamiati mpya.
 
CCM wanadhani wanaikomoa Chadema kwa kui-lable kama chama cha wachagga.in the process wanaleta taifa letu katika line similar na ile iliyosababisha genocide Rwanda.Hili ni jambo la hatari.There is a difference between political disagreement,tribal bash and racism. We cannot continue to let tribal bickering hold us back from fulfilling our destiny as a nation.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Tatizo sio utani, tatizo ni kwamba Regia Mtema alisisitiza sana kwamba ccm ni koo tano ndo zinaongoza lakini sikuona watu kujadili kwa hamasa namna hii na kuilaani kauli hiyo vikali. Na je kauli ya Regia ilikuwa haichochei watanzania kuichukia koo hizo alizozitaja?

Hao ama koo hizo sizitetei, lakini huyu dada na mbunge wa chadema alikuwa anajenga chuki ya hatari zaidi ktk koo hizo, tena unaweza kuta ktk koo hizo kuna walalahoi ambao wanaombea mabaya kila siku viongozi waliotoka ktk koo zao, sasa kuwajumuisha nao ni kauli jumulishi sana. Ambayo nayo ilitakiwa kukemewa vikali, kama kweli watu wanapigania masilahi ya Taifa na si masilahi wezeshi binafsi.

Nonetheless, yawezekana kabisa hizo koo ni coincidence kuwa ndani ya ccm kama ilivyo coincidence ya wachaga kuwa wengi ktk uongozi wa CHADEMA.

Sitaki kuamini kama mtu anaweza kukimea kauli ya Nape na kui- bypass kauli ya Mtema na kinyume chake pia ni sahihi.

Poor Mkamap, how can you go so low as to make such comparison ! At this rate si ajabu ukadai kuwa Dr. Slaa kwa kuwataja mafisadi kumi na moja alikuwa anajenga tu chuki dhidi ya koo hizo. Je, Nape anapodai hawezi kujiunga Chadema kwa hoja ya kutokuwa mchaga ni sawa na mtu yeyote kudai hawezi kuwa si fisadi kwa sababu hatoki koo hizo ? Je anawaambia nini Wachaga walioko CCM au wasio Wachaga ambao wako Chadema, cant you really see the difference ? Koo na kabila, wapi na wapi !
 
Tunashukuru kwa ufafanuzi huu lakini wenye akili wanajua kwamba Sekretarieti ni sehemu ndogo tu ya mfumo wa uongozi wa chama. Tupewe orodha ya wajumbe wa Kamati Kuu, Halmashauri/Baraza Kuu, pamoja na orodha ya wabunge wa viti maalum na uhusiano wao na viongozi wakuu wa chama waliopo na wale wastaafu. Maana dhambi hapa siyo ya ukabila tu, hata nepotism ni issue ambayo inalalamikiwa sana na ni sehemu ya Ufisadi. Tuambiwe mahusiano ya baadhi ya wabunge wa vitu maalum na viongozi wafuatao:

1. Zitto Kabwe,
2. Tundu Lissu,
3. Philemon Ndesamburo,
4. Wilbroad Slaa,
5. Freeman Mbowe.

Tuambiwe pia uhusiano wa Anna Komu na viongozi wakuu wa chama.

Ndiyo mkuu
Nimejaribu kufuatilia ktk tovuti ya CHADEMA, wabunge wapo, viti maalum na sekretariati wapo. Lakini cha kushangaza hakuna wajumbe wote wa kamati kuu ya CHADEMA, pia hakuna wajumbe wa baraza kuu, ktk sehemu hizo wameweka viongozi wa waliowaita wa taifa. Sijui nini wanakiogopa.Hebu fuatilia ktk tovuti yao
Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo

Kuhusu Komu nafikiri ni mke wa jamaa wa fedha makao makuu CHADEMA .
 
Kwa swali hili utadanganywa sana ndugu yangu. Mwalimu alikuwa mpondaji mkubwa sana wa mitazamo ya kuhukumu watu kwa makabila yao. Hata ktk hotuba zake kama ile ya waandishi wa habari pale Kilimanjaro hotel (hii hurudiwa mara nyingi ktk TV nyingi hapa nchini) alitoa msisitizo huo akisema huwezi kumkataa kiongozi anayefaa kwa sababu tu ya kabila lake.

Hofu yangu ni kwamba isije kuwa hata wewe umeianzisha hoja hii sasa hivi ili watu waseme wachaga, wahaya, wanyakyusa (sababu ya tabia za kupendeleana japo si lazima iwe kweli) na wasukuma (kwa sababu ya wingi wao - prone to upendeleano). Kama hiyo ndiyo nia yako nakushauri utafakari upya maana wanasiasa wa nchi maskini wapo tayari kutumia chochote kufanikisha juhudi zao kuifikia dola na wakifika wanawaza kula tu na kujitajirisha jambo ambalo tunapaswa kulipiga vita kwa gharama zozote zile ili walau nchi yetu ipige hatua.

Unaiona spidi ya Rwanda lakini? Unaiona Kenya na Uganda wanavyopiga hatua? Mimi na wewe tukiendeleza ushabiki wa kijinga kama kufagilia ukabila, udini, n.k. ili kulinda utawala wa CCM mwisho wake ni mbaya sana. Hii ni kwa kuwa jamaa zetu na siye tusio na fedha ndiyo tutaendelea kuuwawa na umasikini na vurugu zozote nyingine zinazoweza kutokea. Wao mambo yakiharibika wanahama nchi na utajiri waliotupora.

Acha ushabiki huo mara moja maana gharama yake ni kubwa sana.
 
Msimsingizie Nyerere, wakati wa ukoloni, nchi zote chini ya mkoloni Mwingereza, walifanya mtihani mmoja wa Cambridge. Baada ya uhuru, tukaendelea na mtihani huu, ndipo akagundua kuna watu wa makabila fulani fulani tuu ndio wanaochaguliwa. Makabila hayo ni kutoka mikoa yenye mazao ya biashara ikiongozwa na Kahawa (Kilimanjaro na Bukoba), ikifuatiwa na Pamba (Mwanza), Chai (Iringa na Mbeya). Yale ile mikoa ya mazao mengine kama Tumbaku, Katani, Pareto etc hawakuwa na mashiko kabisa. Mikoa ambayo haikuwa na mazao yoyote ya biashara ikiwemo Singida,Dodoma, na kanda ya Kusini, watoto wao wengi waliishia middle school kwa vile hawakuwa na fedha za ada. Weingi wa waliosoma zamani toka mikoa hiyo, walisoma kwa ukombozi wa wamishenari.

Nyerere aliliona hili, na akaangalia the broad picture, hivya alichofanya ni baada ya uhuru, ni kutengeneza affimative action kuondoa hii imbalance. Kwanza alifua matumizi ya mitihani ya Cambridge na kulifutilia mbali darasa la 8. Alitangaza elimu bure kwa Watanzania wote, na kubadili pass mark kwa kuwa na cut off point ya kila mkoa. Pass mark ya Bukoba na Kilimanjaro ilikuwa juu sana, huku ukanda wa pwani ikiwa ndio lowest na ndiko walikoponea Wakwere. Kwa jamii za wafugaji na makabila madogo kama Wahadzabe, Wasandawe na Wabarbaig, pass mark ilifutwa kabisa kwa wanafunzi hao kusomeshwa sekondari za serikali straight, maana wengine mitiohani yote walipata sifuri!.

Kufuatia hali hiyo, bila kusema rasmi, it was logical kuwa rais wa nchi, akitoka kwenye hizi dorminant tribes, anaweza kuwa mkabila na kupendelea kabila lake hoja ambayo ina ukweli ndani yake. Ila pia tukubali tukatae, hebu fanyeni kajiutafiti tuu ambacho sio scientific, kuna sehemu fulani mkuu akiwa ni mtu wa kabila fulani, amini usiamini, mpaka medium of instructions kwenye corridors ni lugha yao na hapo ni bosi tuu, jee akiwa rais!, si atabadili mpaka lugha ya taifa!.
 
wadau watanisaidia sasa sijui mi na wewe nani ni zoba au ana IQ ZERO coz kwenye hii thread hakuna sehemu niliyisema neno "FUNUNU" au kusoma ni ishu mzee wa ubaoni?? so jipange kwanza acha kukurupuka mzee

Asante. Kwenye thread yako umeanza hivi: "... kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikisikia maneno eti mwl Nyerere kipindi fulani alitamka eti kuna makabila fulani hapa Tanzania ...". eti, eti, ... Umbea mtupu! Unganisha na ulichochangia kwenye thread hii: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/135184-nape-vita-ya-wachagga-utaiweza-7.html message #129. Ama kweli zoba hudhani wengine ndio mazoba. Pole kaka nakushauri uwe na kumbukumbu. Lakini pia sikushangai, mwenendo wako hapa JF unaeleweka na wadau wengi. Ama kweli heri uchi wa nyama kuliko wa akili.
 
Poor Mkamap, how can you go so low as to make such comparison ! At this rate si ajabu ukadai kuwa Dr. Slaa kwa kuwataja mafisadi kumi na moja alikuwa anajenga tu chuki dhidi ya koo hizo. Je, Nape anapodai hawezi kujiunga Chadema kwa hoja ya kutokuwa mchaga ni sawa na mtu yeyote kudai hawezi kuwa si fisadi kwa sababu hatoki koo hizo ? Je anawaambia nini Wachaga walioko CCM au wasio Wachaga ambao wako Chadema, cant you really see the difference ? Koo na kabila, wapi na wapi !

Heh he
Kuhusu Regia hakutaja mafisadi, alitaja koo tano ndizo zinaoongoza ccm , the same way kama alivyotaja wachanga wanaongoza CHADEMA. Tofauti ni kwamba wenda ktk koo zile 5 hukuwemo ama hawakuwemo lakini naamini walikuwemo waliumia sana kama wewe ama yule anayeumia leo kwa kuwemo.

Tatizo ni ukipenda siasa za kutajana tajana lazima nawe ukubali kutajwa either the case, kwa kusingiziwa ama kwa ukweli. sio mimi muasisi wake bali ni Newton third law.

Niambie tofauti ya koo na kabila, kwa jinsi ninavyofahamu koo inaweza kuwa kabila pia.
 
Nape ni kinyonga ni nani asiyejua kuwa baada ya kushindwa kugombea ubungo alioamba kuingia chadema.
 
fige!

Nakubaliana nawe kwa kiasi fulani.
Nionavyo mimi, Maamuzi, Misimamo, Maonyo na Mitazamo ya Mwl. Nyerere havikua misaafu kwamba havipaswi kubadirishwa kulingana na wakati. Mie naamini maamuzi mengi ya Mwl yalikua sahihi kulingana na wakati ule na mengine yanafaa hata kwa wakati huu(Azimio la Arusha), sikatai kama hakuwa na mapungufu au makosa lakini ningeshauri tuchukue yale yaliyokua mazuri na kuyarekebisha yaendane na wakati tulionao sasa pasipo kuondoa lengo la msingi isipokua jinsi ya kutekeleza. Kwa yale aliyokosea tuangalie umuhimu wake kwasasa na kwa mtazamo mzuri kabisa tuyachukulie kama sehemu ya kurekebisha ili yawe na ufanisi mzuri kabisa mfano, uanzishaji wa viwanda na mashirika ya umma, muungano, sekta ya madini, vijiji vya ujamaa, etc. Utakumbuka Mwl alipotoka madarakani, alituacha wengi tukijiuliza hii ndio nini na maana yake ni nini ''KUNG'ATUKA'' Hapa naamini kabisa Mwl alitumia ujasiri wa khali ya juu kuonyesha kua wakati uliokuwepo na unavyoelekea ulikua tofauti kutekeleza mabadiriko ya kile alichokihubiri wakati hiyo ndio ilikua suruhu. Akaona apishe aje mwingine kufanya hayo abadiriko na yeye abaki na yale aliyoweza yeye, hakutaka awe chanzo cha yote mazuri ya nchi hii peke yake, japo alipowapisha hao wengine walienda mbali zaidi hata kupitiliza na kuanza kuharibu, naamini ilimuuma sana na inawezekana hadi ana fariki alikua akisononeka kuona vurugu zilivyoibuka na misingi bora aliyoijenga ikibomolewa kuto jenga mingine iliyo imara zaidi, hapo mzee wetu akabaki akishuhudia na kukemea pembeni kwani hakupewa nafasi tena. Leo hii tuna shuhudia mengi tu khs jk aliyemkataa wakati wananchi tukiwa tumejaa upepo tukimhuhitaji kwa udi na uvumba, Mkapa ambaye tulisema ni chaguo lake tukamchukia leo hii tunamkumbuka kwa hata mazuri yake machache, Lowasa ndio huyo balaa tupu, Malecela nakumbuka Mwl alisema tutafanya kosa kubwa kumpa Uraisi ila akaonya ktk chama cha mapinduzi kwamba watakua wametenda dhambi ambayo hawatasamehewa endapo watathubutu kumtoa ktk chama. Mengi tunayaona sasa. Viongozi waliomfuata Mwinyi na Mkapa walifanya machache kwa nchi lakini mengi yakawa kwa viongozi(kufuta azimio la arusha). Kikwete sasa yeye amechukua mabaya ya awamu zote zilizopita na kuongezea ya kwake kuanzia kwenye serikali hadi chama na ndio tuna sikia sasa MAFISADI-serikalini na MAGAMBA-kwenye chama. Yani huyu sasa kafuta azimio la arusha na la zanzibar pia, hata kama kuna la Bagamoyo nalo katia kapuni na sijui sasa anafuata azimio la kimjini-mjini maana kila kitu ktk chama na serikali ni kimjini-mjini tu. Akitaka kuongea na mawaziri anapiga dili huyoo kwenye mahotel kama cyclical za makampuni binafsi vile wakati angeweza kuwaita ikulu na kuwapa maelekezo wakapata maji wakati wa kikao tena cha siku moja tu. Kwani hao mawaziri hawana maelekezo ya utendaji wao wanapoteuliwa kiasi kwamba wasijue wajibu wao? Mpe kazi hawezi piga chini hayo mambo ya semina elekezi ina maanisha ni kama walipewa kazi bila kujua maadili na mipaka ya utendaji wao plus majuku.
Mie nachoka kabisa!
 
Aissee babangu, ndo kweli Chadema ni chama cha kichagga. Ndo maana wafanya kampeni za mikoa ya Wachagga tu, aissee babaangu. Aissee babaangu, wamekishtukia chadema, aissee babaangu.
Wewe na wamagamba wenzio wote w*s*nge
 
Pia aliwakataa EL na JK. Nyie hamjajua Kashaga anataka kutpeleka wapi? Yeye na Nape ni kopo na mfuniko. Yako mambo mengi ambayo Nyerere aliyataa lakini CCM wanakiuka na wengine katika hotuba zao zote hawajawahi kumwita Baba wa Taifa ila wanamwita Mzee Nyerere. Naikumbuka hii "Mpaka karne hii mnapanda basi la ukabila' na hii " Mtu akifilisika hoja atakimbilia dini ya mtu au kabila lake" na dhambi ya ubaguzi ni hatari sana na ni sawa na kula nyama ya mtu" Naonekana nipo off point lakin nawakumbusha tu namna CCM wasivyomuenzi Mzee wa watu, laana i juu yenu
 
kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikisikia maneno eti mwl Nyerere kipindi fulani alitamka eti kuna makabila fulani hapa Tanzania hayapaswi kupewa nafasi ya kuongoza nchi yetu ya Tanzania,inasemekana aliyataja" LIVE" je kuna mtu mwenye taharifa zozote kuhusiana na hilo? kwavile JF ni sehemu ya ma great thinkers na wanazuoni mbalimbali,nategemea tutapata majibu ya kuridhisha kuhusiana na uvumi huu

hata mimi ndo nasubiri kama kuna ushahidi kuwa JKN alisema hivyo
 
Tujiridhishe kwanza ndani ya Chadema hii ina ashiria nini: Mdee(mchaga),Grace Kiwelu(mchaga),Owenya(mchaga),Komu viti maalum(mchaga),Komu afisa CDM makao makuu(mchaga),Mbowe(mchaga),Ndesamburo(mchaga),Erasto Kweka Afisa wa mambo ya. Bunge CDM(mchaga),Edwin Mtei(mchaga),Suzan Lyimo(mchaga)....... Jamani tumuogope Mungu tusimlaumu Nape angalia orodha hiyo hapo utapata jibu kama CDM sio ya Wachaga!
Mwalimu aliwahi kusema kwamba kati ya watu waliofilisika kisera basi ni wanaozungumza ukabila akina Nape Nnauye na ninyi ndo mifano hai
 
Nafikiri Mwl. Nyerere aliyasema hayo kutokana na kuhofia suala la ukabila katika Nchi yetu, naamini baadhi yetu tumeshuhudia vikundi vya kikabila kuanzia shule za boarding hadi vyuoni enzi hizo na katika vikundi hivyo kulikua na dalili za wazi za kujitenga kikabila na haikuishia ktk shule tu iliendelea hadi vyuoni na makazini. Naamini wale waliokuwepo miaka ya 90 kurudi nyuma wanaweza kubaliana na mimi, kumbuka maafisa mifugo enzi hizo na baadhi ya idara za serikali.

Una ujumbe muhimu lakini maelezo yako yemechangamanyana..
Tupe ufafanuzi wa ujumbe wako mkuu..
 
Back
Top Bottom