Nape mdogo wangu nakushauri anzisha chama chako

Nape mdogo wangu nakushauri anzisha chama chako

Nape anapokea malipo stahiki, alisahu msemo usemao "malipo ni hapa hapa duniani"
 
Tatizo LA Nape hakujiandaa kuwa Mbunge asiye na Mamlaka ndicho kinachomtesa huyu DOGO lengo lake lilikuwa kushika Nyazifa za juu, ikumbukwe hata baada ya JPM kuteua waziri mkuu , Nape na January Makamba ni miongoni mwa wanasiasa ambao hawakuwa na furaha hii inamaanisha hawa wawili walitamani mmoja wao awe Waziri Mkuu huku wakisahau Rais ndo mwenye Mamlaka ya kuteua amtakae bila kupangiwa na ndio maana Rais ndo Mwenyekiti was Chama. Anachokifanya Nape kwa sasa hakuna asiyefamu kuwa huyu jamaa anayafanya haya kwa kuwa amepigwa chini uwaziri, mbona alipokuwa waziri hakuwa mropokaji kama sasa? Nape anaamini kuwa ndani ya CCM yeye ndo mwenye akili kuliko wengine. Nape ndo waziri was kwanza kuonyesha utovu wa nidhamu baada ya kutumbuliwa huku akisahau cheo ni dhamana tu. Ushauri wangu CCM wasimfukuze ila 2020 vikao ndo viamue agombee au apigwe chini. Ushauri mwingine kwa Nape ni kutafuta chama chake kipya ambacho yeye ndo atakuwa Mwenyekiti kwa maana inaonyesha Nape haiwezi kukaa chini ya mtu . Nape aliwahi kufukuzwa hivihivi na Kikwete lakini baadae Kikwete alimrudisha kwa kumpangia ukuu wa wilaya Nachingwea baadae akarudishwa chamani kama katibu mwenezi
nape karopoka kitu gani hadi sasa
 
Back
Top Bottom