Nape: Lowassa ameanza kufanya kampeni, yuko hatarini kuenguliwa

Nape: Lowassa ameanza kufanya kampeni, yuko hatarini kuenguliwa

CCM haiwezi kumeguka eti kwa sababu watamuengua Lowassa. Kama hafuati kanuni basi aenguliwe tu. Hayo mengine ni kutishana tu. Tena ataibuliwa madudu yake na kupelekwa mahakamani na hapo habari yake itakuwa imekwisha
 
EL n MTU Wa visasi Sana na ndiye aliyhakikisha wote ambao hawakuunga mkono mtandao wao 2005 wanatupiliwa mbali....

Namwonea huruma Nappe anapotumia dhamana aliyonayo kupigania mambo binafsi.....

maneno yake mbofumbofu na jeuri yake ya kumtukana lowassa hadharani yatamtokea puani oktoba. wewe muache amalizie kwanza hii miezi michache iliyosalia kabla hajarejea nyumbani kwao masasi akalime korosho. hata ukuu wa tarafa atausikia redioni tu.
 
Lowasa kawashika pabaya ccm sijui watachomokaje hapo.
 
Ni ujinga na uwendawazimu tu kuamini kuwa Lowassa anaweza kuwa Rais wa Tanzania.
 
Nape hana uwezo wa kusoma alama za nyakati hakika haioni nvua kubwa inayokuaja ikitokea milimani.
 
CCM haiwezi kumeguka eti kwa sababu watamuengua Lowassa. Kama hafuati kanuni basi aenguliwe tu. Hayo mengine ni kutishana tu. Tena ataibuliwa madudu yake na kupelekwa mahakamani na hapo habari yake itakuwa imekwisha
Hiki unachokisema hapa hakiwezi kutokea kwa Lowasa..
 
Sasa Kama Chama mnashindwa kuchukua maamuzi magumu kwa mwanachama wenu,mtaweza kusimamia serikali.chadema wao walipoona zito kaenda kinyume na Chama,hawakujali umaruufu wake,na umuhimu wake Bali walimtimua.sasa Kama mnamuogopa mwanachama tu,akiwa rais mtaongea chochote.
 
Maneno yako yanaukweli lakini Lowassa hatalipa kisasi amekomaa Mungu akimjalia atawapuuza tuu

Siasa za Tz ni za Kinafiki sana hao hao ikitokea Lowasa akapitishwa kuwa mgombea Urais utawaona wanajiunga pamoja kumpigia Kampeni na kusahau tofauti zao, wanasiasa wa Tanzania hawaminiki ni vigeu geu sana, Lowasa huwa hana Kinyongo atawasanehe hata vyeo atawapatia kwani anajua kuwa Membe ndiye amewanunua ili wamchafue na pesa za membe wakizimaliza watazinduka tu.
 
Tatizo biashara ya Nape ya kuumuza Membe imekosa wateja.
Na huo ni ukabila kwelikweli kama sio u-Kanda. Wanawasema bure CHADEMA kwamba wakanda na wakabila. Ona first lady katoka DSM kaenda kugombea unec wa ccm Lindi na sasa anataka awe mbunge wa lindi mjini. Ukabila hautaisha, motto wao huyooo kwao chalinze. Tunabadilisha vazi tu lakini mwili ni uleule.
 
Nape kula ukue huwezi mziki wa Lowasa na wala sio saizi yako.hayo maneno ageongea kinana au jk hapo sawa wewe ni bure subiri uone[/QU
Nape ni mouth piece wa Kikwete kwa hiyo anayoyasema yana baraka za mkuu wa kaya,chezea mbayuwayu yeye ni behind the scene.
 
Mbona unaanza kujihami kuwa hujatumwa?Thibitisha.

nasema hivi kwa kuwa mmoja wa watukanaji wanaomtukana lowassa amedai kwamba makundi yanayoenda kumshawishi lowassa achukue fomu yanatumwa na lowassa mwenyewe. ndio maana nimejiweka sawa katika hili.
 
Kuna ushahidi wa kuwa hao watu wametengenezwa yule.ni kiongozi mkubwa nyumbani kwake uende km kwenye gheto la msela lazima uombe kukutana nae je ni dhambi kwa mtu kumuandalia kiti na chakula mgeni wako je sahihi wagombea wasitembelewe na wageni
 
Nape hana hata chembe ya kosa afanyacho ni kuwakemea wanachama wanaobeza maagizo halali ya chama na kuwatahadharisha madhara yake.

Ukionywa usianze kampeni ukaanza basi unakemewa na kukumbushwa madhara ya ukaidi kwani mwana mkaidi hafaidi hadi Siku ya IDD!

kumbuka Nape hutoa matamko mabovu kila mkutano anaohutubia, achilia mbali kupambana na Lowassa, Cyprian Majura anayetumwa na mgombea mmoja kumnadi hadi kutukana wagombea wengine mbona hamwonyi? January mbona haonywi?

Ni utamaduni wetu watanzania, mgeni akija kwako kwa taarifa ama bila taarifa utamkaribisha na kumwonyesha upendo. Utampa hata juice bila kujali kaja kwd mema ama mabaya. Sasa huyu Nape sijui katoka lile kabila akija mgeni anakimbiza ugali uvunguni? Ulimi wake unamponza!
 
Kuna wtu waligawa simu nchi nzima kwa viongozi wa uvccm hawasemwi
 
Nnatumai Nape anao ushahidi wa anayoyasema na kutuhumu watu. Kwamba watu wanaoenda dodoma wamelipwa na nani, kwa njia zipi na kwa sababu gani, la sivyo atakiaibisha chama kwa mara nyengine tena! Wananchi wameamua....acheni uzushi na uongo. Kwa nini mnawadhalilisha wananchi kiasi hiki? Waache kazi zao kwa kulipwa na kupewa chakula? Hivi wote walioonekana huko hawawezi kujinunulia chakula? Tena tunawaingiza mpaka viongozi wetu wa dini; maimamu na wachungaji!

Nnaungana na mtu wa Mungu mmoja aliyemtaka aokoke.....atubu na aokoke!!

Nape amelipwa na Membe ahakikishe Lowasa hapenyi kokote
 
Ni kweli mkwere anaweza kukuuwa huku anatabasamu lakini cha kujiuliza huyu mzee mamvi hayajui yote hayo? Je hamjui rafikiye? Je haogopi kuenguliwa? Au hiki kibri anakipata wapi maana kapewa onyo lakini hajali what is he up to?

Tuspokuwa makini na mamvi atatuletea uvunjifu wa amani tanganyika kwetu,kama haeshimu utaratibu na kanuni za chama chake tena kinachomtambulisha ninauhakika hatoheshmu matakoe ya NEc pale atakapo enguliwa ama akashndwa uchaguzi.
Anaonekana ana uchu wa madaraka kama zzK.
 
Back
Top Bottom