Ericus Kimasha
JF-Expert Member
- Oct 27, 2006
- 488
- 470
wabongo njaa zitawaua, we sema umepewa ngapi uje hapa ulete ukatuni wako.
RACHEL, hawa wamekisaliti vipi CCM? Mimi nadhani hatuwezi kuwaweka hawa sehemu moja na SIMWANA. Nadhani mkubwa wao aliogopeshwa na mlisho nyuma kuwa CHEL walikuwa na muswada kuwa sio lazima Rais akalie kiti cha chama. Hivyo akaanza kutafuta njia ya kuwatoa kabisa lakini kumbe aliyepewa usukani wa kuendesha hilo jahazi hajakomaa vizuri. Na hili litarudi tu kung'ata mkiani!
Tunatumia muda mwingi kwa kuwajadili akina RACHEL badala ya kuangalia matatizo ya wananchi na jinsi serikali inavyoyatatua au inavyoshindwa kuyatatua ili tutoe hukumu ya kweli 2015 badala ya kuwajadili watu wachache ambao kwa mawazo yangu mmoja wao akipewa nchi hii ataipeleka mbali kwa maendeleo kwani ni mtu ambayo anafuatilia mambo na hapendi porojo. Hao wanaoitwa wasafi ni akina nani ndani ya CCM? Hakuna hata mmoja, shida tu ni kwamba ndani mwao wamezidiana uwezo wa kuongoza na kuwa na mali.
Mkuu tatizo wanadhani tunapowapa ushauri sisi nitofauti na ccm, wengi wetu humu ni wale tunaotaka maendeleo ya nchi yetu ufike mda tukajivunia kuwa sisi ni WATANZANIA, mimi naipenda sana nchi yangu ila kwa yanayotokea nchini SIYAPENDI, NAPENDA TANZANIA IWE NA MIPANGO DHABITI YA KUTOKA KWENYE HUU UMASIKINI, nchi hii mpaka leo umeme ni tatizo maji safi na makazi ya watu hakuna, na watu wanazidi kujaa mijini tuu, Nililitegemea mtu kama NAPE aweze kuongelea mambo hayo! Mbona makamba jr huwa tunamuunga mkono baadhi ya mambo yake ( ingawa sometimes anakuwa kama baba yake) Nape tulikuunga mkono uliposema mafisadi watoke ndani ya ccm na siku Tisini tunazisubili, Ulitakiwa pia uongee ulipofikia achapumba kijana! ( mimi nimwanachama wa ccm lakini ile ya Nyerere na si hii ya MAGAMBA)
lakini mi si mlaumu anachokifanya ndio mwisho wa uwezo wake wa kufikiri hivyo anatuzihirishia kuwa yeye ni kilaza namna gani na hata cheo alichopewa si kwa uwezo wake wa kiuongozi bali ni muendelezo wa kujuana na kUpozana.