Imma_Magira
Member
- Jan 8, 2022
- 18
- 26
Na Emmanuel Magira BHRM‐Mzumbe,
Kwa miaka kadhaa sasa, tumeshuhudia kampeni nyingi sana, za kuwapongeza viongoz wa nchi katika kutimiza majukumu yao. Mfano kama CCM wanavyofanya kumpongeza mwenyekiti wao wa chama. Zaidi ya hvyo tunaona mabango yaliyobandikwa kwenye taa za barabarani zikishangilia juhudi za Rais.
Kwa hali ya kawaida haipingiki kwamba, Rais na viongozi wengine wa serikali huchaguliwa kwa lengo la kuwatumikia wananchi. Bila shaka dhana inayokuja hapa ni Uwajibikaji, ikimaanisha wanawajibika kwa wananchi waliwapa dhamana.
Ukakasi na sitofahamu kwangu binafsi ni kwamba, uwepo wa uanzishwaji wa vikundi na asasi mbalimbali zinazolenga kumpromote na kumpongeza Rais katika majukum yake ni sahihi?...
Soma kwa makini maelezo haya, bila shaka wanaosoma sheria watakibaliana na mimi. "Katika kutimiza majukumu ambao inabidi uyatimize (wajibu wako) sio lazima kupokea pongezi au shukrani kwa sababu ni lazima uyatimize, na badala yake pongezi na shukrani zinaweza tolewa kwa mtu ikiwa amefanya jambo kwa utashi wake binafsi na haikuwa na lazima kufanya jambo hilo, kanakwamba hata asipolifanya hatawajibika kwa namna yeyote ile."
Hivyo je, kuna ulazima wowote wa kutumia rasilimali nguvu na muda kupongeza au kutoa shukrani kwa kiongozi ambae inabidi atimize majukumu yake hata pasipo kumshukuru na kumpongeza?
NB: Naomba nisinukuliwe vibaya, sababu mtazamo huu ukiupeleke kidini zaidi utaniona nakosea, ila ni kujaribu kufkilia kwa sisi kama wasomi, kisha tupambanue mambo.