Nape JF sio sawa na Facebook

Nape JF sio sawa na Facebook

BARUA KWA NAPE ..........uliyemuandikia Nape Mosess Nnauye barua hiyo ww naona na mshabiki wa siasa na kundi hilo lilokutuma humu jamiiforum kufanya hivyo waambie wamechemsha ww ni mfuasi tu wa kundi la MAFISADI UKIJIFANYA MPINZANI WA CCM huna lolote kwa jinsi unavyojieleza ww ni CCM NA MFUASI WA KUNDI LA MAFISADI ila aahh..ahhh Nape nyie hamummsumbui yote mnayotaka kumfanyia mtachemsha na mshachemsha.

-Nape ataendelea kuandika anachoona kiko sawa kwake kama kiongozi wa CCM TAIFA katika Mtandao wa FACEBOOK na wewe ukiwa mfuasi wa kundi hilo la MAFISADI endelea tu kusema unachoona kwako sawa DOMO LAKO NDIO MALI YAKO HAKUNA ANAYEKUZUIA maana usiposema watakulipa mshahara wa bure kwani mnalipwa nyie vijana wa mafisadi, sasa endeleeni weee maana huo ndio mwisho wenu wa haya madudu yenu mnayoyafanya katika nchii, malizeni tu miaka yenu hii, ila mjue AWAMU INAYOKUJA MNAKAZI KWELI....nasema mnakazi kweli.....subirini mtaona nchi hii yetu sote, nyie mwaigeuza yenu peke yenu watu msiozidi 100

Ama kweli kuna watu wenye fikra za uvunguni! Lakini nakushauri sana! Attitude can be changed try your level best to change your attitude
 
Kaka umenena tena kwa busara kubwa sana, kazi kwakweli kujiangalia akiwa kavaa viatu vyake mwenyewe. Kama uwezo wake ni mdogo basi aanze kusoma na kunyanyua uwezo wake nadhani pia silazima atumie akili zake maana ameonyesha hana kitu kichwa kabisa, anaweza kutumia wataalam wakulipwa kumpa mambo ya kuongea na nini cha kufanya.

Kinachoniuma katika nchnin yetu na ninacho pigia kelele kila siku ni matumizi mabovu ya rasilimali watu; hapa kwa harahara naona kama wewe ndie ulipaswa kuwa Katibu wa Itakadi na Uenezi wa CCM na si Nape nimefanya thathimini ya haraka inaonyesha wewe kama rasilimali ambayo ingeweza kuitumikia nchni yako ujapata nafasi yako staili na moja ya nafasi imezibwa na mtu hasiye na uwezo anaitwa Nape.

Asante sana mkuu! ushauri alioupata hapa hawezi kuupata kwingine kokote hata lini never!
 
Nape hawezi siasa za sasa, bahati mbaya sana wenye chama wamemkabidhi madaraka wakati wenyewe yamewashinda, hajui aanzie wapi zaidi sana anajichafua kwa kauli zake mwenyewe.

Kila mkutano, anatoa tafsiri tofauti ya kujivua gamba. Mkama kamtosa na ili tumkamate vizuri tunasubiri siku 90 tuone maajabu yake!
Kweli kabisa mkuu tena wanena kweli kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Mkuu Radio Producer, mbona unajipotezea muda mwingi kushauri Nape? Viongozi wa CCM tangu lini wakajua kutumia mtandao?

Je unaweza kula pipi tamu iliyookotwa kwenye mtaro? Tafakari
Asante mkuu! mimi nilifikiria sana maisha yake binafsi nikamhurumia nikaona nimshauri tu!
 
Salam mheshimiwa!

Mimi Radio Producer napenda kukuandikia barua hii kwa hisia zangu ili kutoa mchango wangu kwako katika siasa ya sasa ambayo hata watoto wameielewa! Kwanza mimi sijui kabisaaa mambo ya undani kuhusu siasa ila napenda nikuelezea mtizamo wangu kwenye technologia ya mawasiliano!

1. Mkuu Nape mi nadhani umepewa heshima ya Ukatibu Enezi katika chama chako ili ufanye mambo mazuri ambayo yatakiletea sifa na uhai chama chako. Kwa mtu makini hiyo siyo nafasi ya kuonyesha ubabe au uwezo wa kuponda na kuharibu nguvu ya wapinzani, bila kutathimini athari zake kwa jamii. Ukweli kama alivyosema Mzee Mwanakijiji kwamba kazi ya chama pinzani ni kukisoa chama tawala na kumulika madhaifu yake ili kukidhoofisha na hatimaye kupewa dhaman ya kutawala na wanachi! Hata kwa chama tawala nadhani ni the same! Kwa kiasi umejitahidi kulifanyia kazi hilo make nimekuona kila ukisismama ukipata fursa ya kuponda upinzani unafanya hivyo. Lakini.......

2. Ijue vizuri teknolojia ya mawasiliano ya mtandao. Mtandao unaweza kukuharibia sifa zako sana! au kukuongezea sifa zako sana! Wataalamu wanasema kwamba moja ya negative effect za social network zinakuonyesha kwa jamii kiasi gani ulivyomweupe kichwani au ulivyo na nguvu kichwani! Nape nimesoma sana post zako nyingi hapa JF na hata kule Facebook hoja zako au topic zako unazotoa hata kwa mtu mwenye ufahamu wa kawaida anakuona wewe ni mtu wa kawaida sana! Wewe ni kiongozi mkubwa katika chama chako na hata nchi hii huwezi kuwa na post za ajabu ajabu kiasi hicho! Angalia wall zote za marais, hata watu wenye heshima uone kama utakuta post nyepesi kama zako. Moja ya post ulizopost ni hizi:-

Nape Nnauye
CHUO KIKUU CHA. DODOMA2 hours ago via BlackBerry · Like · kwenye facebook.
Majibu uliyoyapata unajua wewe!

post zingine:-
Nape Nnauye
Nimeona kikatuni mahali mtu mmoja kavaa kombati akiwaammbia wafiwa subirini msizike msubiri maandamano yetu hapa.......hii ni dhihaka au kweli?

Nape Nnauye
BINADAMU HAENDELEZWI ILA HUTENGENEZEWA MAZINGIRA MAZURI YA KUJIENDELEZA MWENYEWE"JK NYERERE

Nape Nnauye
TUSIKILIZE RADIO UHURU.....RADIO YA CHAMA CHETU

Hizi ni moja tu ya post zinazonifanya nikuone mtu wa kawaida sana! Angalia wall ya Obama, hata maraisi wengine kama inapost za kitoto kiasi hicho! Nape unajivunjia heshima! Halafu huoni hizo wall wanazokupostia watu zikiwa na matusi makubwa kiasi hicho?? Huoni kuwa jamiii iko kinyume nawewe zaidi? Je unatumia hoja gani sasa kujiweka vizuri katika jamii? Mafanikio huanzia katika jamii kama watu wengi wanakuponda jiulize cha kufanya ili hali hiyo iishe! WEWE BINAFSI UNAWEZA UKAWA MTU MZURI SANA LAKINI CHAMA KIKAHARIBU KABISA SIFA YAKO! Fikiria zaidi kaka yangu, sijaona hoja zako za kiuongozi!

3. Post ya katuni ya kombati. Kwa mimi hata kama ningekuwa balozi wa kitongoji nisingeweza kupost hoja ya hivyo wakati taifa lina msiba! Vifo vilivyotokea Mara ndugu yangu vinaumiza mno hasa kwa walengwa! Jiulize hata kama ungekuwa wewe ukatokwa na mtoto wako kwa hali hiyo ungepost post ya hivyo kweli? huu ni wakati wa kufikiria mara 3 zaidi kabla ya kusema chochote! Ni wakati ambao wafiwa wanahitaji maelezo ya kuridhisha na ya msingi! Unatakiwa kuwa na Empathies na Sympathies! Uchukulie kama msiba wako! Toa maneno yasiyo ya kisiasa wakati huo linda nafsi yako! Kadri unavyotoa maneno makali na ya kuumiza ndivyo unavyopata laana za wanachi na kudharauliwa! Kaka yangu Nape kaa chini basi kaka ufikirie vizuri uanze moja, ulivyoanza watu wengi wamekuwa kinyume hautafanikisha kile chama kimedhamiria!

4. Mtandao, Kaka yangu sijui elimu yako kuhusu mtandao iko level gani, lakini nakuomba kaa na watalaamu wa mitandao badili matumizi ya mtandao haraka iwezekanavyo. Hata facebook ingebidi ujitoe ni sawa tu au utengeneze page siyo kutumia kama hivyo unavyotumia! Mtu yeyeote anakupostia matusi tu kwenye wall yako anakudhalilisha mno kaka! Weka privacy yako kwenye Fb iwe kubwa! social network ziko hivi:- Walio kwenye mtandao wanaweza kuwa watatu hao wakitoka wanamarafiki zao wataenda kuwaambia yaliyotokea na hao watatu watafanya hivyo hivyo! Unachoandikiwa ama kuandika kinasomwa na wengi mno kaka yangu! Hata hapa JF, wewe kila hoja ukitoa watu wanakuponda tu ulishawafanyia nini? Hao wanaokupinga hapa wanafuatwa na jamii nyuma usitarajie jamii nayo itakukubali hamna! Kuna picha uliweka kwenye mtandao umebeba kanga za CCM wanaume wanakugombea wanataka wapate hata moja, NI AIBU KUBWA KWA TAIFA NAYAWEZA KUWA LAANA KWAKO! Wewe uliona fahari sana kuwa unafanya kazi, hebu fikiria angekuwa mzazi wako anajitoma kiasi hicho kugombania kamga ungefurahi? Wanachi wanahitaji kupewa haki yao sasa hivi sioyo vitenge wala kanga! Watanzania ni matajiri kwa vitu vya asili walivyopewa na Mungu, lakini leo wewe ndo unaneemeka na wao unawapelekea kanga???? ni tusi kubwa hilo kaka yangu! Kaka badili msimamo wako! jisikie Utanzania wa Watanzania maskini ili uwasaidie!

Namalizia kwa kusema Nape mtandao unakuharibia sifa zako, waachie wanaojua kuutumia vinginevyo wewe binafsi utapoteza heshima yako maisha yako yote!

Sina nia mbaya mwana wa mtu kama nimekukera leave me Alone.
Radio Producer.

Kaza uzi Nape , ukisikia paaaaaaa ujue imempata, ndivyo alivyo fanya huyu aliyeleta thread hii, yamemuingia na ujumbe umefika
 
Jamani mwacheni huyo OMR, mtashindwa kujadili hoja za msingi na kuanza kumjibu yeye, just ignore her.
Mkuu mwache huyu mpumbavu na mshenzi ajibiwe, mpaka hicho kitu kigumu alichokalia kinachomfurahisha kivunjike! Hawezi kuleta upuuzi wake humu ndani Forum ategemee kuachwa hiyo haiwezekani nasisitiza hiyo haiwezekani.
 
Kuna mdau alitundika uzi mmoja matata sana kumhusu nape. Sasa nilipotaka kupost na mm nadhani wakawa wameshainyonga. Kwa nini?
 
Kuna mdau alitundika uzi mmoja matata sana kumhusu nape. Sasa nilipotaka kupost na mm nadhani wakawa wameshainyonga. Kwa nini?

Mods wanamuonea huruma, pia kuna post niliwahi kuchana sana coz namfahamu Nape kupitia kwa wazee wake wa Bagamoyo University!
Nikamchana humu ila Mods wali-edit sana hata ule utamu ukapungua.
Ila sio ishu coz mwenyewe Nape amejipambanua sana kwa jamii mithiri ya vazi la kahaba!
Kila mtu kamuelewa kuwa hawezi tena kukomboa anachojaribu kukomboa.

Mtu mwenye picha Udom atutumie tujionee show yake!
 
Na Saed Kubenea - Imechapwa 18 May 2011

Gumzo la Wiki

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye sasa amebeba “gunia la kokoto” na hajui mahali pa kulitua.

Hadi sasa Nape amejiingiza katika mgongano wa ndani kwa ndani katika chama chake; amepanua wigo wa maadui kwa kuandama anaowaita “watuhumiwa wakuu wa ufisadi;” na anabembea katika malumbano na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Tangu kukabidhiwa wadhifa wa ukatibu mwenezi wa CCM, Nape amekuwa akisisitiza, “…kung’oa mafisadi ndani ya CCM, ni jambo ambalo halina tena mjadala.”

Amesema, “Kinachosubiriwa sasa ni suala la utekelezaji tu; NEC imetoa siku 90 kwa mafisadi kuondoka” katika chama hicho.

Katika hili, Nape alijiapiza kuwa barua za kujulisha mafisadi kuondoka katika chama tayari zimeandaliwa na zitatolewa kabla ya kumalizika Sikukuu ya Pasaka. Hazijatoka.

Viongozi ambao wametajwa na Nape kuwa wanatakiwa kujiondoa kwenye uongozi au chama ndani ya siku 90 kwa kuwa ni “mafisadi wanaochafua sura ya chama mbele ya jamii,” ni Edward Lowassa, Rostam Aziz na Andrew Chenge.

Wote watatu ni wajumbe wa NEC na wabunge wa Bunge la Muungano.

Hata hivyo, Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama aliwaambia waandishi wa habari wiki mbili zilizopita jijini Dar es Salaam, “…hakuna mahali popote katika maazimio ya NEC panapotaja siku 90.”

Alisema, “Kama ni muda basi ni pale mwenyekiti wetu aliposema NEC ijayo. NEC hukutana kila baada ya miezi minne na kwa hiyo kama ni siku, basi ni 120 na siyo 90.”

Hatua ya Nape ya kutamka kuwapo kwa barua za kufukuza mafisadi ndani ya chama chake au azimio la NEC, lilikuwa kosa la kwanza kisiasa.

Hata kama Nape alikuwa ametumwa na mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete kusema aliyosema, bado alipaswa kuwa makini na mzigo aliobebeshwa.

Kwa wanaomfahamu Kikwete tangu alipokuwa Tanga Sekondari, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) hadi ikulu, wanajua jinsi alivyo bingwa wa kutumia wenzake na kisha kuwaacha njiani pale maslahi yake yanapoguswa.

Hili linathibitishwa na hatua yake ya kuridhia kujiuzulu kwa Edward Lowassa katika wadhifa wake wa waziri mkuu.

Lowassa ambaye mwaka 1995 aliandamana na Kikwete kuchukua fomu ya kuwania urais na kufanikisha harakati zake za kuingia ikulu katika uchaguzi wa mwaka 2005, alitoswa huku akiona.

Kisa: Kikwete alihofia kile kilichoitwa na aliyekuwa mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge, Dk. Harrison Mwakyembe “hatukusema yote, ili kuokoa serikali na rais.”

Taarifa zinasema, Kikwete aliamua kuepusha malumbano ambayo yangeweza kumhusisha na ujio wa makampuni tata ya Richmond na Dowans.

Si hivyo tu. Kikwete ameridhia kuondoka katika nafasi yake ya uspika, Samwel Sitta ambaye tangu mwaka 1995 walikuwa wote katika kutafuta urais.

Ni Sitta aliyemjengea Kikwete msingi wa mbio za urais tokea mwaka 1995 alipokubali kumpeleka kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kupata baraka za kugombea urais.

Katika uchaguzi wa mwaka 2005, Sitta alikuwa makamu mwenyekiti wa kundi la mtandao uliomuingiza Kikwete madarakani.

Lakini bila sababu za msingi zenye kuathiri maslahi ya taifa, Kikwete aliamua kuweka sharti la kutaka spika mwanamke; sharti ambalo lilimuondoa Sitta katika kinyang’anyiro hicho.

Wengine ambao walitumiwa na Kikwete na wakaachwa njiani kwa sababu hizohizo au zinazofanana, ni pamoja na Bernard Membe, Amos Makalla na Zakia Meghji.

Makala ndiye alikuwa katibu wa mtandao wa Kikwete, huku Meghji akitajwa kuwa ni miongoni mwa watu waliofanikisha, kwa kiasi kikubwa, kampeni za urais wa Kikwete.

Wakati Membe alitumika “kufanikisha mkakati” wa kuwafukuza Rostam, Lowassa na Chenge katika vikao vya maamuzi, Kikwete katika staili yake ya kuuma na kupuliza, aliamua kutopeleka jina lake katika kinyang’anyiro cha uchaguzi wa wajumbe wa Kamati Kuu (CC) na sekretarieti ya chama.

Hata kuondoka kwa Yusuf Makamba na kuingizwa kwa January Makamba, mtoto wake, kumefanywa kwa njia hiyohiyo.

Hivyo basi, hatua ya Nape ya kujiingiza katika mgongano wa ndani kwa ndani na wenzake ; na kung’ang’ania hoja ya kufukuza wanaoitwa “mafisadi ndani ya chama,” inaweza kumgharimu.

Kikwete anaweza kuamua kumuacha Nape solemba kwa kuwa kibarua alichompa kimemshinda; hawezi kutetea alichoagizwa; hafahamu anachotakiwa kufanya na hajui anachotenda.

Kwanza, badala ya kujibu hoza zilizosheni takwimu na uhalisia wa maisha ya kila siku ya wananchi zinazotolewa na CHADEMA, kwa mfano “serikali kufilisika,” yeye amejiingiza katika hoja dhaifu ya posho za watendaji wa chama hicho akiwamo katibu mkuu Dk. Willibrod Slaa.

Anasema Dk. Slaa analipwa mshahara wa Sh. 7.5 milioni kila mwezi. Anadai kitendo hicho ni sawa na ufisadi. Anamtuhumu kuwa huko nyuma aliwahi kunukuliwa akisema mishahara ya wabunge ipunguzwe kwa kuwa inaangamiza taifa.

Nape haishii hapo. Amezungumzia pia kile anachoita “ununuzi wa magari chakavu” yaliyonunuliwa kutoka kwa mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.

Hatua ya Nape kunyooshea kidole CHADEMA, haiwezi kukisaidia chama chake katika mkwamo wa tuhuma dhidi ya ufisadi, badala yake imekizamisha chama chake katika tope.

Kwa mfano, wakati Nape anasema mshahara wa katibu mkuu wa CCM, ni Sh. 1.5 milioni, ukweli ni kuwa kima cha mshahara kwa watendaji wakuu wa chama hicho, kinategemea mhusika ametokea wapi kabla ya kupewa kazi hiyo.

Yusuph Makamba, katibu mkuu aliyeondoka madarakani, alikuwa anatakiwa kulipwa Sh. 1.5 milioni. Huu ni mshahara ambao alikuwa anapata wakati akiwa mkuu wa mkoa.

Lakini Makamba aliamua kuachana na mshahara huo kwa kuwa yeye tayari alikuwa mbunge. Alibaki na mshara wake mmoja wa ubunge ambao ni zaidi ya Sh. 7.1 milioni anazolipwa Dk. Slaa.

Aidha, katibu mkuu wa CCM anamiliki magari matatu – la kwake, linalotumiwa na wasaidi wake katika msafara wake na lile linalotumiwa na mkewe. Magari yote haya matatu huhudumiwa na CCM.

Mbali na Makamba kupewa magari matatu, alikuwa analipwa posho ya Sh. 135,000 (laki moja na elfu thelathini na tano) kwa kila siku ambayo anakuwa nje ya Dodoma. Hapa Makamba atakuwa amejichukulia kitita cha zaidi ya Sh. 11.5 milioni kwa mwezi.

Kwa kuwa Makamba alikuwa mbunge, aliendelea kunufaika na stahiki zote za mbunge. Alilipwa mafuta – Sh. 2.5 milioni kila mwezi. Alilipwa posho ya dereva – Sh. 400,000 kila mwezi, huku chama chake kikigharamia dereva, mafuta na baadhi ya safari zake zikiwamo zile za nje ya nchi.

Hata safari yake ya matibabu nchini India, pamoja na safari za kikazi mkoani Dodoma, zote hizo ziligharamiwa na Bunge na chama chake.

Ndivyo ilivyokuwa pia kwa Jaka Mwambi aliyekuwa naibu katibu mkuu wa chama hicho. Mwambi alilipwa Sh. 1.5 milioni kwa mwezi kwa kuwa kabla ya kushika wadhifa huo alikuwa mkuu wa mkoa wa Rukwa.

Baada ya muhula wake wa ubunge kumalizika, ndipo Makamba akaanza kulipwa fedha hizo, lakini alijilipa mamilioni mengine ya shilingi kama posho ya kujikimu.

Katibu mkuu mpya, Wilson Mukama, kwa kuwa ameacha utumishi akiwa katibu mkuu serikalini, atachota kitita cha Sh. 3.8 milioni; posho ya Sh. 135,000 kwa kila siku asiyokuwapo Dodoma na atakuwa na wasaidizi sita wanaolipwa posho ya kati ya Sh. 30,000 na 55,000 kwa siku.

Mukama amekabidhiwa magari matatu yanayohudimiwa na chama chake – mawili yake na moja la mkewe – na atakuwa anaendelea kulipwa stahiki yake ya kiinua mgongo kama katibu mkuu mstaafu.

Je, Nape alikuwa anafahamu haya kabla ya kuamua kuangamiza chama chake? Anajua kuwa maelezo haya yametosha kuwapa mtaji wa kisiasa wapinzani wake?

Kimsingi kabla ya Nape kuzungumza alichokusudia, alipaswa kupima maelezo yake. Alipaswa kuangalia athari zitakazokipata chama chake.

Matokeo yake, sasa analazimika kufanya kazi tatu kwa mpigo – kuokoa chama chake, kujiokoa yeye mwenyewe na kuendelea na kibarua cha Kikwete kwa kuhubiri “mwisho wa mafisadi” usiowadia.

Badala ya kusisitiza umuhimu wa chama chake kuachana na mafisadi, analazimika sasa kujibu madai yaliyoporomoshwa na CHADEMA na kuthibitishwa na Fred Mpendazoe juu ya ushiriki wake katika kuunda, kusajili na kutumikia Chama cha Jamii (CCJ).

Badala ya kutumia muda na akili yake kueleza wanachama na viongozi wenzake jinsi chama hicho kilivyodhoofika kisiasa kwa kukumbatia ufisadi na mafisadi, sasa anapaswa kujibu hoja juu ya jinsi alivyonufaika na fedha za wizi wa EPA kupitia kwa mmoja wa watuhumiwa, Jeetu Petel.

Badala ya kujenga chama chake, Nape anapaswa kujielekeza sasa katika tuhuma juu ya usaliti kwa chama chake; na hatua yake ya kutaka kugombea ubunge katika jimbo la Ubungo, kupitia CHADEMA.

Atachoka au tuseme tayari amechoka asubuhi. Amejitwisha vineno asivyoweza kutetea na amekitumbukiza chama chake katika mbio ambazo hawezi kushinda.

Huyo ndiye Nape Nnauye. Kijana anayedhani anaweza kuokoa CCM kwa kuvurumisha madai dhidi ya upinzani.

Waswahili husema aendaye mbio za Nape, amebeba gunia la kokoto. Je, Nape anapeleka wapi gunia hilo? Atamuuzia nani?
 
Kitu kimoja tujisifu Watanzania, makala kama hii kwenye nchi nyingi sana duniani, hata zilizotupita kimaendelea, kama China, haiwezi kuandikwa gazetini. Kubenea, unajitahidi sana katika research zako, sidhani kama kuna dirt-dredging journalist Tanzania kama Kubenea. Ahsante.
 
Salam mheshimiwa!

Mimi Radio Producer napenda kukuandikia barua hii kwa hisia zangu ili kutoa mchango wangu kwako katika siasa ya sasa ambayo hata watoto wameielewa! Kwanza mimi sijui kabisaaa mambo ya undani kuhusu siasa ila napenda nikuelezea mtizamo wangu kwenye technologia ya mawasiliano!

1. Mkuu Nape mi nadhani umepewa heshima ya Ukatibu Enezi katika chama chako ili ufanye mambo mazuri ambayo yatakiletea sifa na uhai chama chako. Kwa mtu makini hiyo siyo nafasi ya kuonyesha ubabe au uwezo wa kuponda na kuharibu nguvu ya wapinzani, bila kutathimini athari zake kwa jamii. Ukweli kama alivyosema Mzee Mwanakijiji kwamba kazi ya chama pinzani ni kukisoa chama tawala na kumulika madhaifu yake ili kukidhoofisha na hatimaye kupewa dhaman ya kutawala na wanachi! Hata kwa chama tawala nadhani ni the same! Kwa kiasi umejitahidi kulifanyia kazi hilo make nimekuona kila ukisismama ukipata fursa ya kuponda upinzani unafanya hivyo. Lakini.......

2. Ijue vizuri teknolojia ya mawasiliano ya mtandao. Mtandao unaweza kukuharibia sifa zako sana! au kukuongezea sifa zako sana! Wataalamu wanasema kwamba moja ya negative effect za social network zinakuonyesha kwa jamii kiasi gani ulivyomweupe kichwani au ulivyo na nguvu kichwani! Nape nimesoma sana post zako nyingi hapa JF na hata kule Facebook hoja zako au topic zako unazotoa hata kwa mtu mwenye ufahamu wa kawaida anakuona wewe ni mtu wa kawaida sana! Wewe ni kiongozi mkubwa katika chama chako na hata nchi hii huwezi kuwa na post za ajabu ajabu kiasi hicho! Angalia wall zote za marais, hata watu wenye heshima uone kama utakuta post nyepesi kama zako. Moja ya post ulizopost ni hizi:-

Nape Nnauye
CHUO KIKUU CHA. DODOMA2 hours ago via BlackBerry · Like · kwenye facebook.
Majibu uliyoyapata unajua wewe!

post zingine:-
Nape Nnauye
Nimeona kikatuni mahali mtu mmoja kavaa kombati akiwaammbia wafiwa subirini msizike msubiri maandamano yetu hapa.......hii ni dhihaka au kweli?

Nape Nnauye
BINADAMU HAENDELEZWI ILA HUTENGENEZEWA MAZINGIRA MAZURI YA KUJIENDELEZA MWENYEWE"JK NYERERE

Nape Nnauye
TUSIKILIZE RADIO UHURU.....RADIO YA CHAMA CHETU

Hizi ni moja tu ya post zinazonifanya nikuone mtu wa kawaida sana! Angalia wall ya Obama, hata maraisi wengine kama inapost za kitoto kiasi hicho! Nape unajivunjia heshima! Halafu huoni hizo wall wanazokupostia watu zikiwa na matusi makubwa kiasi hicho?? Huoni kuwa jamiii iko kinyume nawewe zaidi? Je unatumia hoja gani sasa kujiweka vizuri katika jamii? Mafanikio huanzia katika jamii kama watu wengi wanakuponda jiulize cha kufanya ili hali hiyo iishe! WEWE BINAFSI UNAWEZA UKAWA MTU MZURI SANA LAKINI CHAMA KIKAHARIBU KABISA SIFA YAKO! Fikiria zaidi kaka yangu, sijaona hoja zako za kiuongozi!

3. Post ya katuni ya kombati. Kwa mimi hata kama ningekuwa balozi wa kitongoji nisingeweza kupost hoja ya hivyo wakati taifa lina msiba! Vifo vilivyotokea Mara ndugu yangu vinaumiza mno hasa kwa walengwa! Jiulize hata kama ungekuwa wewe ukatokwa na mtoto wako kwa hali hiyo ungepost post ya hivyo kweli? huu ni wakati wa kufikiria mara 3 zaidi kabla ya kusema chochote! Ni wakati ambao wafiwa wanahitaji maelezo ya kuridhisha na ya msingi! Unatakiwa kuwa na Empathies na Sympathies! Uchukulie kama msiba wako! Toa maneno yasiyo ya kisiasa wakati huo linda nafsi yako! Kadri unavyotoa maneno makali na ya kuumiza ndivyo unavyopata laana za wanachi na kudharauliwa! Kaka yangu Nape kaa chini basi kaka ufikirie vizuri uanze moja, ulivyoanza watu wengi wamekuwa kinyume hautafanikisha kile chama kimedhamiria!

4. Mtandao, Kaka yangu sijui elimu yako kuhusu mtandao iko level gani, lakini nakuomba kaa na watalaamu wa mitandao badili matumizi ya mtandao haraka iwezekanavyo. Hata facebook ingebidi ujitoe ni sawa tu au utengeneze page siyo kutumia kama hivyo unavyotumia! Mtu yeyeote anakupostia matusi tu kwenye wall yako anakudhalilisha mno kaka! Weka privacy yako kwenye Fb iwe kubwa! social network ziko hivi:- Walio kwenye mtandao wanaweza kuwa watatu hao wakitoka wanamarafiki zao wataenda kuwaambia yaliyotokea na hao watatu watafanya hivyo hivyo! Unachoandikiwa ama kuandika kinasomwa na wengi mno kaka yangu! Hata hapa JF, wewe kila hoja ukitoa watu wanakuponda tu ulishawafanyia nini? Hao wanaokupinga hapa wanafuatwa na jamii nyuma usitarajie jamii nayo itakukubali hamna! Kuna picha uliweka kwenye mtandao umebeba kanga za CCM wanaume wanakugombea wanataka wapate hata moja, NI AIBU KUBWA KWA TAIFA NAYAWEZA KUWA LAANA KWAKO! Wewe uliona fahari sana kuwa unafanya kazi, hebu fikiria angekuwa mzazi wako anajitoma kiasi hicho kugombania kamga ungefurahi? Wanachi wanahitaji kupewa haki yao sasa hivi sioyo vitenge wala kanga! Watanzania ni matajiri kwa vitu vya asili walivyopewa na Mungu, lakini leo wewe ndo unaneemeka na wao unawapelekea kanga???? ni tusi kubwa hilo kaka yangu! Kaka badili msimamo wako! jisikie Utanzania wa Watanzania maskini ili uwasaidie!

Namalizia kwa kusema Nape mtandao unakuharibia sifa zako, waachie wanaojua kuutumia vinginevyo wewe binafsi utapoteza heshima yako maisha yako yote!

Sina nia mbaya mwana wa mtu kama nimekukera leave me Alone.
Radio Producer.

- Mhhhhhh! Mkuu mbona personal sana kuliko Taifa, I mean utawala wa Chama kimoja cha siasa katika siasa Za vyama vingi, hauwezi kuwa ishu unless kama kuna ushahidi wa kutosha na wa wazi kwamba kuna kiongozi wa chama flani anafanya matendo kinyume na Taifa kwa kutumia chama chake, I begg to respectfully differ na mtoa mada hii,

- Mh. Nape ni kiongozi wa CCM ametimiza masharti ya uongozi ndani ya CCM, ndio maana wamempa nafasi, sasa CCM ndio wanaweza kudai kwamba hafai, lakini sio sisi wananchi wengine ambao sio wanachama wa CCM, mimi ni mwanchama wa CCM, ninaamini kwamba Mh. NaPE ANA mandate ya CCM na pia kuungwa mkono na Mwenyekiti wa CCM Taifa kwa yote anayoyafanya kwa CCM, US wanasema kwa vile W.Bush alikuwa anachukiwa na Dunia nzima, basi ni Rais anayewafaa sana Wamarekani, so labda hizi kelele nyingi sana kwenye Blogs dhidi ya Mh. Nape, ni kwamba anawafaa sana CCM, can you Imagine kiongozi wa CCM, anayeweza kuja hapa na kukubalika kwa wakati huu?

- I mean tumuache MH. Nape afanye kazi ya chama chake, kama anaharibu ni kwenye chaguzi ndio tuwaelimishe wananchi madhara ya uongozi wa Nape, I mean it is becoming a Nape fiesta sasa hapa JF, kama ametoa hoja nje ya mstari wa Taifa sawa, lakini hoja ambazo ni samba mba na Ilani za chama chake, then it is not our business, labda tushambulie the Ilani, lakini sio the messenger, otherwise tunaangaukia kwenye ule ule mtego wa siasa za majina badala ya hoja muhimu kwa taifa, zilizotufkisha hapa tulipo hili taifa!

William @ NYC, USA.
 
mi namchukia sana nape kwa sababu anatuchukia sana sisi wachaga!
nape ole wako uje rombo, marangu au old moshi.
utajua kwa nini kunguru hakojoi!
 
Mkuu umenena! sasa hivi mkewe kamkimbia kwa ufuska wake! anahangaika na lile jimama jamvi la wageni mhe. M..... (name withheld) mbunge wa Viti maalum Singida. Namba ya Nape ni 0715 131977

Si lile limama linalojifanya limeokoka? Sasa Nape ana share ule mzigo na Mwenyekiti?
 
Nape endeleza libeneke wakosoaj wanaumwa ugonjwa wa kupindwananape so dalili kubwa nikuharisha so nasikia wao wanamisuli na mataulo tu
 
Back
Top Bottom