Nape JF sio sawa na Facebook | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape JF sio sawa na Facebook

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Saint Ivuga, May 25, 2011.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  May 25, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,434
  Likes Received: 19,774
  Trophy Points: 280
  Nape tunashukuru sana kwa kuja hapa JF, tunajua una kazi nyingi ila mtindo wako wa kuweka bandiko hapa na kukimbia sio fresh, hapa JF ukiweka bandiko lazima ulitetee, sio lazima ujibizane au ujibu watu /post zenye jazba au matusi.
  Kuna post nyingi tu zenye hoja.
  Hapa sio sawa na facebook, kule wamejaa watoto wa wakubwa na rafiki zako ambao siku zote watakusifia ila humu ndani hatusifii kila kitu , ukipiga kazi lazima tukusifie ila ukiharibu hatukuachi, kwa hiyo ukianzisha mada au thread usiikimbie hapa.
  Amani iwe nawe:
  Saint Ivuga @Mbagala kipati
   
 2. Radio Producer

  Radio Producer JF-Expert Member

  #2
  May 25, 2011
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Salam mheshimiwa!

  Mimi Radio Producer napenda kukuandikia barua hii kwa hisia zangu ili kutoa mchango wangu kwako katika siasa ya sasa ambayo hata watoto wameielewa! Kwanza mimi sijui kabisaaa mambo ya undani kuhusu siasa ila napenda nikuelezea mtizamo wangu kwenye technologia ya mawasiliano!

  1. Mkuu Nape mi nadhani umepewa heshima ya Ukatibu Enezi katika chama chako ili ufanye mambo mazuri ambayo yatakiletea sifa na uhai chama chako. Kwa mtu makini hiyo siyo nafasi ya kuonyesha ubabe au uwezo wa kuponda na kuharibu nguvu ya wapinzani, bila kutathimini athari zake kwa jamii. Ukweli kama alivyosema Mzee Mwanakijiji kwamba kazi ya chama pinzani ni kukisoa chama tawala na kumulika madhaifu yake ili kukidhoofisha na hatimaye kupewa dhaman ya kutawala na wanachi! Hata kwa chama tawala nadhani ni the same! Kwa kiasi umejitahidi kulifanyia kazi hilo make nimekuona kila ukisismama ukipata fursa ya kuponda upinzani unafanya hivyo. Lakini.......

  2. Ijue vizuri teknolojia ya mawasiliano ya mtandao. Mtandao unaweza kukuharibia sifa zako sana! au kukuongezea sifa zako sana! Wataalamu wanasema kwamba moja ya negative effect za social network zinakuonyesha kwa jamii kiasi gani ulivyomweupe kichwani au ulivyo na nguvu kichwani! Nape nimesoma sana post zako nyingi hapa JF na hata kule Facebook hoja zako au topic zako unazotoa hata kwa mtu mwenye ufahamu wa kawaida anakuona wewe ni mtu wa kawaida sana! Wewe ni kiongozi mkubwa katika chama chako na hata nchi hii huwezi kuwa na post za ajabu ajabu kiasi hicho! Angalia wall zote za marais, hata watu wenye heshima uone kama utakuta post nyepesi kama zako. Moja ya post ulizopost ni hizi:-

  Nape Nnauye
  CHUO KIKUU CHA. DODOMA2 hours ago via BlackBerry · Like · kwenye facebook.
  Majibu uliyoyapata unajua wewe!


  post zingine:-
  Nape Nnauye
  Nimeona kikatuni mahali mtu mmoja kavaa kombati akiwaammbia wafiwa subirini msizike msubiri maandamano yetu hapa.......hii ni dhihaka au kweli?

  Nape Nnauye
  BINADAMU HAENDELEZWI ILA HUTENGENEZEWA MAZINGIRA MAZURI YA KUJIENDELEZA MWENYEWE"JK NYERERE

  Nape Nnauye
  TUSIKILIZE RADIO UHURU.....RADIO YA CHAMA CHETU

  Hizi ni moja tu ya post zinazonifanya nikuone mtu wa kawaida sana! Angalia wall ya Obama, hata maraisi wengine kama inapost za kitoto kiasi hicho! Nape unajivunjia heshima! Halafu huoni hizo wall wanazokupostia watu zikiwa na matusi makubwa kiasi hicho?? Huoni kuwa jamiii iko kinyume nawewe zaidi? Je unatumia hoja gani sasa kujiweka vizuri katika jamii? Mafanikio huanzia katika jamii kama watu wengi wanakuponda jiulize cha kufanya ili hali hiyo iishe! WEWE BINAFSI UNAWEZA UKAWA MTU MZURI SANA LAKINI CHAMA KIKAHARIBU KABISA SIFA YAKO! Fikiria zaidi kaka yangu, sijaona hoja zako za kiuongozi!

  3. Post ya katuni ya kombati. Kwa mimi hata kama ningekuwa balozi wa kitongoji nisingeweza kupost hoja ya hivyo wakati taifa lina msiba! Vifo vilivyotokea Mara ndugu yangu vinaumiza mno hasa kwa walengwa! Jiulize hata kama ungekuwa wewe ukatokwa na mtoto wako kwa hali hiyo ungepost post ya hivyo kweli? huu ni wakati wa kufikiria mara 3 zaidi kabla ya kusema chochote! Ni wakati ambao wafiwa wanahitaji maelezo ya kuridhisha na ya msingi! Unatakiwa kuwa na Empathies na Sympathies! Uchukulie kama msiba wako! Toa maneno yasiyo ya kisiasa wakati huo linda nafsi yako! Kadri unavyotoa maneno makali na ya kuumiza ndivyo unavyopata laana za wanachi na kudharauliwa! Kaka yangu Nape kaa chini basi kaka ufikirie vizuri uanze moja, ulivyoanza watu wengi wamekuwa kinyume hautafanikisha kile chama kimedhamiria!

  4. Mtandao, Kaka yangu sijui elimu yako kuhusu mtandao iko level gani, lakini nakuomba kaa na watalaamu wa mitandao badili matumizi ya mtandao haraka iwezekanavyo. Hata facebook ingebidi ujitoe ni sawa tu au utengeneze page siyo kutumia kama hivyo unavyotumia! Mtu yeyeote anakupostia matusi tu kwenye wall yako anakudhalilisha mno kaka! Weka privacy yako kwenye Fb iwe kubwa! social network ziko hivi:- Walio kwenye mtandao wanaweza kuwa watatu hao wakitoka wanamarafiki zao wataenda kuwaambia yaliyotokea na hao watatu watafanya hivyo hivyo! Unachoandikiwa ama kuandika kinasomwa na wengi mno kaka yangu! Hata hapa JF, wewe kila hoja ukitoa watu wanakuponda tu ulishawafanyia nini? Hao wanaokupinga hapa wanafuatwa na jamii nyuma usitarajie jamii nayo itakukubali hamna! Kuna picha uliweka kwenye mtandao umebeba kanga za CCM wanaume wanakugombea wanataka wapate hata moja, NI AIBU KUBWA KWA TAIFA NAYAWEZA KUWA LAANA KWAKO! Wewe uliona fahari sana kuwa unafanya kazi, hebu fikiria angekuwa mzazi wako anajitoma kiasi hicho kugombania kamga ungefurahi? Wanachi wanahitaji kupewa haki yao sasa hivi sioyo vitenge wala kanga! Watanzania ni matajiri kwa vitu vya asili walivyopewa na Mungu, lakini leo wewe ndo unaneemeka na wao unawapelekea kanga???? ni tusi kubwa hilo kaka yangu! Kaka badili msimamo wako! jisikie Utanzania wa Watanzania maskini ili uwasaidie!

  Namalizia kwa kusema Nape mtandao unakuharibia sifa zako, waachie wanaojua kuutumia vinginevyo wewe binafsi utapoteza heshima yako maisha yako yote!

  Sina nia mbaya mwana wa mtu kama nimekukera leave me Alone.
  Radio Producer.
   
 3. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #3
  May 25, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  You are hopeless, ccm wamejitia kuvamia hizi social networks waache yawakute unamtahdharisha wa nini? Acha ayakoge matusi hadi avuliwe nguo za ndani
   
 4. Radio Producer

  Radio Producer JF-Expert Member

  #4
  May 25, 2011
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Mimi natoa ushauri kwa Nape siyo kwa CCM!
   
 5. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #5
  May 25, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Nape wa CCM au CCJ?
   
 6. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #6
  May 25, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kwanza mimi naona nape ni mwepesi mno kwa nafasi aliyopewa, Alitakiwa kwanza kuelewa itikadi ya CCM kabla ya kuanza kuzungumza sana. Sasa amesoma nini kwa Azam. Anasema nini kuhusu azimio la Arusha, ana mtazamo gani kuhusu siasa ya ujamaa. Hii ni kabla ya kurudi kwanye neno Gamba. Huyu kijana ajifunze kujipanga kama akina mnyika na Zito. Amekuwa ni kijana wa kukurupuka, na nina wasiwasi ataachwa katikati kwenye mataa. Mukama ndo hivyo keshamtema, kwamba hakuna aliyepewa siku tisini, sasa amehamia vyama vya upinzani. Vipost vyake kwenye JF ndio kabisaaa, vinamuonyesha alivyo na mapungufu katika falsafa. Ushauri huu ni mzuri, kwa maana anakwenda shimoni.:A S 103:
   
 7. Radio Producer

  Radio Producer JF-Expert Member

  #7
  May 25, 2011
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Yaani jaman muonaoweza fungueni facebook ya Nape muangalia hizo post anazopata toka kwa watu! Namhurumia kwa sababu hakuna anachojenga! mtazamo wake binafsi ndio shida hapo baadae! Make ameshajivunjia heshima sasa atapataje kibali kenye jamii tena?? Aangalie kukubalika katika jamii na si kwa CCM. maana kuna siku CCM watatoka madarakani je atafanya nini kwenye chama kitakachokuwa madarakani? Pole Nape tizama mbali zaidi!
   
 8. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #8
  May 25, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Muache aendelee kuumpa matumaini Kama mhonjwa wa ukimwi huku akijua aliyoyafanya nyuma.Ktk page zake facebook nimekuwa nikipita huko mara kwa mara hakuna cha maana anachoandika nyingi zimezidiwa na mipasho Kama ya kwenye taarabu.Pili dharau anayoionyesha waziwazi mbele ya jamii kupitia post zake ktk mitandao juu ya viongozi wa upinzani ndio anajimaliza kabisa.Unaleta dharau kwenye vifo vya Wstanzania?nani ataluvumilia na kukupenda?labda punguani.Go to hell ccm go tunaitaka Tanzania yetu
   
 9. Radio Producer

  Radio Producer JF-Expert Member

  #9
  May 25, 2011
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Nape si unaona watu wanavyokupa feedback, kama unajua kutumia maoni ya watu chukua haya hapa kajifunze kuadapt
   
 10. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #10
  May 25, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Acha kupigia maiti gitaa, hawezi kujiadapt coz anatafuta platform mpya baada ya kunyang'anywa ile aliyoingia nayo katika wadhifa mpya ya kuwapa RACHEL siku 90 kujiondoa katika CCM. Alipaswa kujiuzulu baada ya Katibu Mkuu wa CCm kukanusha kuwa hakuna majina yaliyotajwa katika vikao vya CC na NEC ya CCM ilihali Mukama hakuhudhuria vikao hivyo. Badala yake Nape aliishia kulalamika mbele ya wahariri kuwa majina yalitajwa na kuibuka na staili mpya ya kuiponda CHADEMA hakujua kuwa nondo zake za CCJ zilikuwa jikoni. Sasa anatakiwa kujivua Gamba yeye na akina RACHEL kwa kuisaliti CCM.
   
 11. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #11
  May 25, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,003
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  hajui falsafa ya kujivua gamba itafuatiwa na ya kujivua nguo.
   
 12. Radio Producer

  Radio Producer JF-Expert Member

  #12
  May 25, 2011
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45

  Akimaliza mkutano UDOM atakuja asome
   
 13. Radio Producer

  Radio Producer JF-Expert Member

  #13
  May 25, 2011
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Nape na Kibonde unawaonaje?
   
 14. O

  Omr JF-Expert Member

  #14
  May 25, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Producer mbuzi, ushauri kaa nao mwenyewe, we sema upewa ulfu ngapi na rostam uje ulete upuuzi wako hapa
   
 15. Radio Producer

  Radio Producer JF-Expert Member

  #15
  May 25, 2011
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Kama wewe ndio Nape pole sana maana huwezi kuadvance hata siku moja! Nimeuweka hapa ushauri wako ili hata watu wengine wachangie hoja zikujenge ujirekebishe! Kama unang'ang'ania na hali uliyonayo na huoni kuwa ni ugonjwa na hutaki kupokea feedback ni bora urudi darasani kwanza ukasome Advance Communication.
   
 16. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #16
  May 25, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Mkuu sijakubaliana na wewe kuhusu kuacha kutumia Mitandao ila namshauri nape atumie kama katibu mwenezi wa ccm, asifanye ujinga kabla hata hajapost anaweza kushauliana na wenzake kwanza! but kwa sasa naona kama yupo chini sana huwezi ukaenda kupata mawazo ya kujenga kwa Nape, anaweza kuangalia post za Zitto Kabwe, Dr Slaa, Mnyika, Malecela jr, n.k halafu awe anapost kama wao na asikimbie kwenye mijadala hiyo, kama afanyavyo sasa. JF SI YA KITOTO KAMA FACEBOOK WALIOPO HUMU NIWATU WANAOJUA MAMBO NA KUYATAFAKALI! sasa inakuwa afadhali ya M.S tena wakati yeye ni Kiongozi, na nibora asingeandika jina lake tujue ni jinga flani hv!
   
 17. O

  Omr JF-Expert Member

  #17
  May 25, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wabongo njaa zitawaua, we sema umepewa ngapi uje hapa ulete ukatuni wako.
   
 18. Radio Producer

  Radio Producer JF-Expert Member

  #18
  May 25, 2011
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Umenena kweli kabisa kiongozi!
   
 19. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #19
  May 25, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280

  huyu ni moja wa vijana wake aliowaajiri kwa ajili ya jf.......
   
 20. N

  Nanu JF-Expert Member

  #20
  May 25, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  RACHEL, hawa wamekisaliti vipi CCM? Mimi nadhani hatuwezi kuwaweka hawa sehemu moja na SIMWANA. Nadhani mkubwa wao aliogopeshwa na mlisho nyuma kuwa CHEL walikuwa na muswada kuwa sio lazima Rais akalie kiti cha chama. Hivyo akaanza kutafuta njia ya kuwatoa kabisa lakini kumbe aliyepewa usukani wa kuendesha hilo jahazi hajakomaa vizuri. Na hili litarudi tu kung'ata mkiani!
  Tunatumia muda mwingi kwa kuwajadili akina RACHEL badala ya kuangalia matatizo ya wananchi na jinsi serikali inavyoyatatua au inavyoshindwa kuyatatua ili tutoe hukumu ya kweli 2015 badala ya kuwajadili watu wachache ambao kwa mawazo yangu mmoja wao akipewa nchi hii ataipeleka mbali kwa maendeleo kwani ni mtu ambayo anafuatilia mambo na hapendi porojo. Hao wanaoitwa wasafi ni akina nani ndani ya CCM? Hakuna hata mmoja, shida tu ni kwamba ndani mwao wamezidiana uwezo wa kuongoza na kuwa na mali.
   
Loading...