Kwanza kwaajili ya kujenga uadilifu binafsi, Nape ungebadilisha jina lako, utumie jina la Baba yako mzazi kuliko kutumia jina la Mzee Moses Nnauye ambaye siyo biological father wako.
Pili, Nape jihadhari na ujifunze kutumia vizuri mdomo wako. Unataja afya ya Dr. Slaa, wewe ulimpima na kugundua kuwa anaumwa au ana afya mbaya? Sijawahi kusikia Dr. Slaa ameshindwa kufanya kazi zake kutokana na tatizo la afya au umri. Unamtaja Dr. Slaa kuwa ni babu yako, hivi kweli umri wa Baba yake Prof. mwandosya unalingana na wa Dr. Slaa? Kwa nini uongelee afya ya Dr. Slaa ambaye yu mzima na mwenye afya njema kuliko kuongelea afya ya Baba yako ambaye amekaa India kwa matibabu kwa mwaka mzima? Hivi umri wa Dr. Slaa una tofauti gani na umri wa Mwandosya? Na Prof. Mwandosya naye huwa unamwita Babu yako na siyo Baba yako?
Kumbuka kuwa Marehemu Komba alitoa maneno kama haya yako kwa Mzee Warioba lakini leo Komba yuko wapi na Mzee Warioba yupo mzima wa afya njema na wala hatujawahi kusikia kama amelazwa au anaumwa wakati wowote ule. na Mungu tunamwomba azidi kumzidishia afya njema na maisha marefu.
Tupingane katika yote lakini tusijifanye kama sisi wanadamu tunafahamu kuwa nani ataishi mpaka lini. Mungu humchukua kila mtu kwa wakati alioupanga bila kujali umri, jinsia, dini au itikadi yake ya kisiasa, hufanya hivyo kwa hekima yake ya Kimungu ili kuwafifisha wanadamu kama akina Nape wanaodhani wanautambuzi au wanajua nani anastahili kuishi mpaka lini. Sisi wengine tunazidi kumwomba Mungu wetu mamlaka na ukuu wake uzidi kudhihirika siku zote.