CCM imetoa tamko linalodaiwa kuwa ni majibu ya tuhuma zilizotolewa na CHADEMA juu ya mipango ya kumuua Dr.Wilbrod Peter Slaa,Katibu Mkuu wa CHADEMA. Tuhuma hizo zilitolewa mbele ya vyombo vya habari na Wakili Msomi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA,Mabere Nyaucho Marando. Tamko la CCM limetolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM
Nape Nnauye. Nape ametuangusha na amejidhalilisha.
Tamko lote la CCM halijagusa wala kukanusha tuhuma za CHADEMA lililomgusa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara,Philip Mangula, Mlinzi binafsi wa Dr.Slaa na Maafisa wa Usalama wa Taifa.Tuhuma alizozitoa Marando kwa niaba ya CHADEMA ni tuhuma nzito.Ilitegemewa kuwa CCM wangejibu kwa undani tuhuma hizo hadi kuonyesha upande wa pili;hatua kwa hatua.
Tamko la CCM limeshindwa kujibu tuhuma za CHADEMA.Limeishia kumshambulia Dr.Slaa ambaye kwenye tuhuma yeye ni muathirika tu wa mpango ovu uliodaiwa kupangwa. Tuamini kuwa waliotajwa wamehuska kweli? Iko wazi kuwa Tamko limejielekeza kwingine kabisa na kuziacha tuhuma vile vile zilivyotolewa. Watanzania bado wanasubiri majibu ya CCM juu a tuhuma za CHADEMA.
Kwanini vitu serious kama hivi aachiwe
Nape Nnauye mwenye masihara kila mahala na uwezo mdogo wa kupambanua mambo?
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam