Nape azomewa makambako

Hajagundua kuwa akiwanyooshea kidole cha kati wananchi vidole vingine vinne kikiwepo na kile kinene zaidi gumba vinaingia kwake? Kweli ana....... Anavivumilia vyote hivyo!.
 
Hapana sasa mnakubuhu kwa uongo,simpendi Nape lakini kwa Makambako kafanya kitu sijaamini kama ni Nape huyuhuyu ninae mchukia. Katoka vijana wanasukuma gari yake kwa furaha leo wawadanganya watu. Mengine sawa lakini si la Makambako

QUOTE=Milindi;4005850]Mkutano WA nape makambako waishia kwa nape kuzomewa na kuoneshwa alama ya chama pinzani.nape uzalendo ulimshinda akafungua kioo na kuonesha ishara ya mkono akiwa na maana kuwa wale wanaozomea wana...
...rwa. jiheshimu[/QUOTE]
 
Tumuamini nani? Kazomewa ama kapokewa na mpokezi mazuri? Msituchaga leteni picha kuthibitisha msemayo

Unamuamini huyu 'chini kwa chini'? Huyu yupo hapo mtaa wa lumumba akisubiri buku yake kama malipo ya siku kwa kuposti *****.
 
Akiwa makambako nape amekutana na zahama hiyo baada ya kukataa kuulizwa maswali na wananchi.baada ya kuona wanamzomea na kuonyesha alama ya v inayotumiwa na cdm naye kawaonyesha alama ya matusi kuwajibu.asema wanaohama ccm ni oil chafu azomewa,asema slogan ya m4c imekosewa ilibidi iwe movement for demokratic change ,aambiwa hiyo ni ya ccm na si cdm.leo wamepata aibu ya mwaka.
Source ni mimi mwenyewe niliyekuwepo kwenye mkutano

yaani gamba hili 'nepi' ndo wa kuwafundisha cdm cha kufanya na cha kuwaza? mbona haji na mipango ya kukiokoa chama chake!!
 
Sishangai maana CCM siku hizi mnaenda ki-reverse mkizomewa ndo mmeshangiliwa. Teh teh te teh sijui na hapa utasema nimecheka ama nimekucheka

Hata mimi sishangai maana kwa ccm maandamano wanayaita mapokezi
 
Sishangai maana CCM siku hizi
mnaenda ki-reverse mkizomewa ndo mmeshangiliwa. Teh teh te teh sijui na
hapa utasema nimecheka ama nimekucheka

Hawana aibu, nikikumbuka siku membe alipozomewa uwanja wa taifa nilikuwepo uwanjani lkn kuna watu walikataa katakata kuwa hakuzomewa!
 
Nape ni stooge tu! Namfananisha na boya linalotumwa msitari wa mbele vitani ili kujaribisha kama kuna adui!
Amepewa kazi ya kuwaaminisha watu kuwa maiti inaweza kufufuka na kuwaletea watu maendeleo...Ccm ni maiti!
 
Naleta picha soon jinsi vijana tena nawafahamu kabisa wa cdm wakisukima gari la Nape, kwa hili ntamtetea Nape
Pia utuambie aliwalipa shilingi ngapi hao waliosukuma gari lake hilo.
 
Naleta picha soon jinsi vijana tena nawafahamu kabisa wa cdm wakisukima gari la Nape, kwa hili ntamtetea Nape

Tafuta picha za songea haraharaka utupie hapa tuuzuge umma kumnusuru katibu mwenezi, anahaibika kaka.
 
Mh! hlo nalo gamba livuliwe,.wasira kazomewa anasema walikua watano tu wamezomea wengne wameshangila yan hawa chama cha mafisi wameshachokwa tuwatoe kwa nguvu
 
Kwa iyo aliwaonyesha wapiga kura dole la kati??
Dah, nnauye jr kama ni kweli kazi unayo.
Ila sishangai sana kwani wewe ni mmoja kati ya waasisi wa kifo cha ccm.


Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

Ndugu zanguni; ogopeni sana kiumbe kinachokaribia kukata roho kuingia mautini na hasa kama matendo yake wakati wa uhai wake yalikuwa ya mashaka. Kiumbe cha aina hiyo kiko tayari kufanya lolote ili kujinusuru lakini ndio hivyo tena siku "yenyewe" ikiwadia imewadia.

Na ndipo ilipofikia CCM; matendo yake kwa taifa letu yamekuwa machafu ajabu; siku zake ilizoandikiwa kuishi ndio hivyo tena zimekwisha mtasikia na kuona kila kimbwanga. CCM walipofikia sasa hivi wako tayari kuropoka kila aina ya upuuzi ili kujinusuru. Suala la ukweli na amani ya nchi kwao sio issue tena; la muhimu watajiokoaje na kifo kinachowakabili!

Narudia tena: AMANI YA TAIFA HILI ITAVURUGWA NA CCM wala sio na kabila, dini, au kanda fulani; kama ikitokea basi vitakuwa ni vichocheo tu vya CCM bali ibilisi halisi ni lichama lenyewe!
 
Nape Oil Chafu ina soko kubwa sana Kenya na Uganda kama unayo leta tukauze tujikomboe na huu waya!
 
Nini Nape kipande kile Mwenyekiti wake alipopolewa mawe sembuse nape...watu wamechoka kudanganywa ebo!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom