Akikua ataachaNimejaribu kufuatilia mikutano yake, na mmoja hapa jamii forums kanikonyezea niende Facebook nione comments zake kuhusu Jamii forums, nimekuja kugundua kitu kimoja muhimu kuhusu Nape Mnauye.
Kama amepitia university, alipuuzi kozi ya rhetorics ambayo kwa lugha nyepesi wanasema effective speaking, na hata kama alipitia tu shule ya msingi na sekondari, alipuuzi somo la fasihi ya kiswahili au english composition. Ningemshauri back to school apate msasa vinginevyo ataharaibu zaidi.
Kwa cheo chake cha DC na Katibu mwenezi wa CCM Kitaifa katu sikutegemea anaweza kuandika kitu kama hiki hadharani ambako kila kuku hupita kudonoa mtama. Kama hotuba zake hata kule Masasi alikokabidhiwa District Commission kama anatoa lugha kama hizi basi naona CCM wameishiwa watu wanaofaa katika uongozi.
Nisaidieni DC anaweza ongea au andika hadharani kauli zifuatazo alivyofanya Nape?
Samahani huyu ni mtanzaniea na kijana mwenzetu tunahitaji kumsaidia kwani ni kiongozi mmojawapo katika taifa letu na watu wale wale tunaoongea na kufanyakazi pamoja kila siku.
- CHANDIMU AIBUUUU KALIPENI KODI YA MSHAHARA WA BOS WENU
- UKINYANG"ANYWA TAULO CHUTAMA MNACHOFANYA JF AIBU.....nimefurahi mnakuja huku pia>>> HAYA ONENI AIBU YENU
- NADHANI MNATANGAZA UBABE SASA,TOENI NA HIII
- HAKIKA CHANDIMU NA JF WAO WAMECHANGANYIKIWA SANA....hahahaaa MPAKA WANACHONGA PICHA KUHALALISHA UONGO WAO?......DAWA YA DENI KULIPA JAMANI...KALIPIENI KODI YA BOSS WENU
- MTOTO WACHA KUPIGA MAYOE ACHA WATU WAONE WENYEWEEE
Wazee wa CCM msaidieni kijana wenu, kuacha hivi hivi mnaumbua utamaduni wa kitanzania.
Mkuu Candid Scope,
Tatizo siyo lugha, tatizo ni chama kukosa hoja za maana ambazo zitaweza kukirejeshea chama haiba ambayo imepotea mbele ya wananchi/wapiga kura.
Nape Nnauye alianza kwa kishindo sana. Wiki mbili za mwanzo tangu alipoteuliwa kuwa Katibu wa Uenezi na Itikadi, alionekana kuanza kurejesha imani kwa wananchi.
Baada ya kufungwa mdomo amekosa cha kuongea na hivyo imebidi tu aanze kuleta vioja na lugha za kejeri. Hizo lugha za kejeri ndizo zinazidi kuongeza matope na haiba ya CCM inazidi kupotea. Hata wale waliokuwa na imani japo kidogo, ndiyo watazidi kuipoteza kabisaaa.
Kwa sasa Nape Nnauye amejiweka kwenye kona mbaya kwa sababu ya mambo yafuatayo:
1. Aliahidi kwamba mafisadi wataondoka na kuwaachia CCM iliyo safi (hapa aliwalenga Lowassa, Chenge na Rostam). Hoja hiyo imeenda na maji na sasa hivi haiongelewi tena maana amegundua kwamba hilo haliwezekani.
2. Alitamba kwamba mafisadi wataandikiwa barua, na alisema baada ya Pasaka barua wangepelekewa. Mpaka leo hakuna fisadi hata mmoja aliyepewa barua.
3. Nape Nnauye alisema mafisadi wamepewa siku 90 za kujitazama then wajiondoe na wasipoondoka watafukuzwa. Katibu Mkuu (boss wa Nape) akasema hakuna cha siku tisini na wala hilo halimo kwenye majumuisho ya makubaliano ya kikao cha NEC.
Hoja ambayo ilikuwa inampa nguvu Nape ilikuwa imejengwa kwenye msingi wa hoja ya ufisadi, lakini hoja hiyo imepoteza mwelekeo kutokana na hayo matatu juu. Nape amejikuta mahali ambapo kila anachokisema kinaonekana kupingana na maboss wake (Msekwa na Mukama). Swala la barua, Msekwa alisema wao hawafanyi kazi kwa kupitia vyombo vya habari (limeisha kimya kimya). Swala la siku 90, Mukama akasema halimo kwenye tamko la NEC. Swala la mafisadi watatu ambao walikuwa wakilengwa na Nape, Mukama alisema CCM haina list ya mafisadi. But Nape alisema anawajua na kwamba wameambiwa wazi na walitajwa majina kwenye vikao, sasa kwanini Msekwa na Mukama wanaingia mitini?
Nape yuko njia panda na si ajabu anajuta kwanini alitamka hayo maneno wakati wa ile mikutano ya mwanzo ya Operation Vua Magamba. Maneno aliyoyatamka amekuta hayatekelezeki au walio na uwezo wa kuyatekeleza, hawataki au wanaogopa. Sasa inabidi aje na vijembe, vioja na lugha za kejeri, typical Mzee Makamba na Tambwe Hizza.
Mkuu African Stars ipo toka enzi hizo za kina Mbinga na Mtido wao ni Twanaga pepeta wameingi na Kutoka kina Banza,Ally choki,Muumin,Khalid Chokolaa,Badi bakule lakini Twanga ipo palepale na mtindo wao ni uleule na Radha yake ni ile ile twanga Pepeta.Vivo hivyo CCM ya Mwalimu , Mwinyi, Mkapa na hatimaye Kikwete itabaki kuwa CCM ile ile yenye maana ileile CHUKUA CHAKO MAPEMA,watabadilika viongozi lakini Sera za chama zipo kwenye maandishi kila ajae lengo ni kuchukua nchi na kutawala si kuwaletea maendeleo chanya.Jamani,
Huyu bwana mdogo naona amekuja na staili inayoweza kumwingiza kwenye kundi moja la wazee wa taarabu tuliowazoea la mzee Yusufu Makamba na Tambwe Hiza.
Katika siku za hivi karibuni nimeona kasi ya Nnape ya kuropoka na kubwabwaja kama kasuku imeongezeka kiasi cha kutilia shaka uwezo wake katika kukiletea mabadiliko chama chake kilichompatia dhamana ya uongozi.
Sasa ameibuka na kauli yake kwamba Dr. Slaa ni fisadi! Yeye anadhani watanzania ni watoto wanaoweza kudanganywa na kauli nyepesi nyepesi hivyo!!!
Sasa nimeanza kuamini maneno ya watu waliobeza slogan ya kujivua gamba kwamba nyoka akijivua gamba anabaki kuwa nyoka. Na ndivyo ilivyo kwa CCM.
Mwanzoni, nilidhani sasa tutaanza kusikia kauli zenye mashiko kutoka kwa huo uongozi mpya wa ccm ulioingia baada ya kile kilichoitwa kujivua gamba. Nilijua nyimbo za taarabu zitakuwa zimeisha.
Kumbe wapi, kilichobadilika ni wanamuziki tu, hivi ni kweli ccm imeishiwa watu wa maana wanaoweza kuongoza chama professionally?
Mwanzo wa mwisho wa Nape kisiasa unakuja haraka sana
nape hana hoja. Yeye ni mtu mbishi.
Wadau katika gazeti la mtanzania Nape Nauye (aka..Tambwe Hizza) amejibu makombora ya chadema na amesema kwamba Chadema wanatapatapa kwa sababu sasa amepatikana mtu makini wa kujibu hoja zao.
Pia amedai kwamba Chadema walizoea kuionea CCM kwa sababu hakukuwa na mtu makini anayejua kujibu hoja.Ameapa ataendelea kuianika Chadema mpaka pale watanzania watakapotambua ni nani fisadi kati ya CCM na Chadema.
Pia amedai kwamba mshahara wa katibu mkuu wa CCM Wilson Mukama hauzidi milioni 3 kwa sababu CCM haina mafisadi kama chadema.Amesema pia kwamba hakuwahi kuomba kujiunga chadema eti kwa sababu yeye si mchaga.
Kuna vyombo vingine vya habari Nape amedai leo atazidi kuilipua na kuimaliza kabisa Chadema.
Mwanzo wa mwisho wa Nape kisiasa unakuja haraka sana
Jamani,
Huyu bwana mdogo naona amekuja na staili inayoweza kumwingiza kwenye kundi moja la wazee wa taarabu tuliowazoea la mzee Yusufu Makamba na Tambwe Hiza.
Katika siku za hivi karibuni nimeona kasi ya Nnape ya kuropoka na kubwabwaja kama kasuku imeongezeka kiasi cha kutilia shaka uwezo wake katika kukiletea mabadiliko chama chake kilichompatia dhamana ya uongozi.
Sasa ameibuka na kauli yake kwamba Dr. Slaa ni fisadi! Yeye anadhani watanzania ni watoto wanaoweza kudanganywa na kauli nyepesi nyepesi hivyo!!!
Sasa nimeanza kuamini maneno ya watu waliobeza slogan ya kujivua gamba kwamba nyoka akijivua gamba anabaki kuwa nyoka. Na ndivyo ilivyo kwa CCM.
Mwanzoni, nilidhani sasa tutaanza kusikia kauli zenye mashiko kutoka kwa huo uongozi mpya wa ccm ulioingia baada ya kile kilichoitwa kujivua gamba. Nilijua nyimbo za taarabu zitakuwa zimeisha.
Kumbe wapi, kilichobadilika ni wanamuziki tu, hivi ni kweli ccm imeishiwa watu wa maana wanaoweza kuongoza chama professionally?