"Naongea na Riz1": Nusura daladala ikamatwe Arusha

Filipo

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
9,342
5,536
Katika kile kilichoonekana kama ni muendelezo wa wananchi wa Arusha kuikataa serikali, muda mfupi uliopita dereva wa daladala iliyokuwa imesimamishwa na polisi pamoja na gari nyingine eneo la Aicc hosp, ili kupisha msafara wa makamu wa rais ambaye alikuwa anakwenda kupata lunch kibo palace hotel, alijikuta matatani baada ya kuwekwa chini ya ulinzi kwa muda.

Daladala hiyo ilikuwa inapiga wimbo wa bongo fleva unaosema "naongea na Riz1, ongea na mshua" kwa sauti ya juu sana wakati gari zilipokuwa zimesimamishwa. Alifuatwa na askari waliokuwa karibu na kumhoji sababu za kupiga wimbo huo pale na kwa sauti kubwa. Walimlazimisha azime na aseme aliyemtuma.

Hata hivyo alikubali kuzima na kukana kutumwa. Walimwacha baada ya abiria kumtetea kuwa wimbo unatoka kwenye kituo cha redio.

Duh! Kaaazi kwelikweli!?
 
Anyway, kwanini afungulie kwa sauti ya juu. Atakuwa anawasumbua abiria.
 
Nimeona zile gari za pa chadema zilizokuwa zimeshikiliwa na polisi arusha zimeachiwa saiv maeneo ya field force mbauda,shangaa polisi walisema hawaziachi mpaka chadema watakapolipa uharibifu uliotokea kwenye magar ya polisi.serikal legelege,pia kuna tetesi afande zuberi kaondolewa arusha
 
Katika kile kilichoonekana kama ni muendelezo wa wananchi wa Arusha kuikataa serikali, muda mfupi uliopita dereva wa daladala iliyokuwa imesimamishwa na polisi pamoja na gari nyingine eneo la Aicc hosp, ili kupisha msafara wa makamu wa rais ambaye alikuwa anakwenda kupata lunch kibo palace hotel, alijikuta matatani baada ya kuwekwa chini ya ulinzi kwa muda.

Daladala hiyo ilikuwa inapiga wimbo wa bongo fleva unaosema "naongea na Riz1, ongea na mshua" kwa sauti ya juu sana wakati gari zilipokuwa zimesimamishwa. Alifuatwa na askari waliokuwa karibu na kumhoji sababu za kupiga wimbo huo pale na kwa sauti kubwa. Walimlazimisha azime na aseme aliyemtuma.

Hata hivyo alikubali kuzima na kukana kutumwa. Walimwacha baada ya abiria kumtetea kuwa wimbo unatoka kwenye kituo cha redio.

Duh! Kaaazi kwelikweli!?
Aisee hii imetulia sana,
 
Nashauri tuanzishe kaji-jukwaa kadogo kwa ajili ya kuawtukana kidogo polisi walioshindwa kukamata majambazi na wezi wa mali zetu....
 
kati ya nyimb nnazo zipenda hiyo ni moja wapo, kitu kimetulia ukikisikiliza utagundua jamaa ametupa meseji kali mle ila kwa akili za magamba bado sana
 
Du kiboko ule wimbo umeshiba sana natumain mkuu wa kaya na R1 hawata usahao maishani mwao
 
Polisi wa bongo akili zao zimejaa makonokono, vinyonga, kumbikumbi, kobe na mikia ya kondoo ndio maana hawawezi kufikiria
 
Kwani trafiki kumuambia dereva apunguze sauti ya radio ni kosa. Radio zinachangia ajali za barabarani.
 
Tuwekeeni huo wimbo basi ama hata mashairi.JF ni international jamani.
 
Sasa kunaakiri hapo mtu kusikiliza nyimbo nako kuna masharti,juz wamemshikilia mtu kwa kosa la kuvaa nguo ya chadema iv mbona watu wakivaa nguo za CCM huwa hakuna mtu anaye hoji au ndo kuishiwa hoja watakiona mwaka huu
Aluta continua!!"
 
Hii nimeipenda, naongea na ridhiwan we ridhiwan ongea na mshua aachie ngazi kwani dr.slaa yupo tayari kupokea haki yake na kutimiza kile alichoahidi wapigakura wake
 
Back
Top Bottom