Naona kama mabinti waliohitimu vyuo wanakabiliana vizuri na changamoto ya ajira kuliko vijana wa kiume

Wanawake tumeamua kuchakarika na kila shughuli ukitafta hela hamna kuona aibu. Tena tumejiunga na vikundi tunacheza na michezo hatutaki utani maisha yetu wanawake tusipofanya kazi tutakuwa jamvi la wageni.
Hongera ila punguzeni vitambi hata kama hela zenyu
 
Hii ni kitu nimeiona baada ya kufanya utafiti wa kijuu juu. Nimeona mabinti wengi wanachakarika na ujasiriamali.

Ninekutana na wahitimu wa vyuo ambao ni mama ntilie. Wanapiga umachinga mdogomdogo wa nguo za kike, juice, viatu nk. Pia wamekuwa mstari wa mbele kuhudhuria mafunzo ya ujasiriamali kama kutengeneza sabuni nk.

Imekuwa kazi sana kumkuta mhitimu wa kiume akifanya hizi ishu ndogondogo kama kuchoma chips na mishkaki. Nini shida kwa vijana wakiume kuingia kwenye sekta isiyo rasmi baada ya kumaliza chuo?

Rai yangu, Serikali ijitahidi kwa nguvu zote kuweka mazingira ya vijana kuweza kujiajiri.
Kuna kiungo hujakitaja hapo huwakinapata taabu sana kabla ya kufikia hatua hiyo.
 
Back
Top Bottom