Namna Serikali inapaswa kupambana na changamoto ya ukosefu wa ajira nchini

The Festival

Member
Aug 30, 2021
27
98
Ni matumaini yangu kwamba sote tuko poa. Kwa wale ambao wana changoto tunawaombea kwa Mola Mkuu awatatulie shida zao. Moja kwa moja kwenye jambo husika.

Kupata job serikalini sio shughuli ndogo. Mbaya zaidi hilo ndio kimbilio na tumaini kwa vijana wengi. Pitia jukwaa la ajira na tenda utapata ushuhuda. Tatizo la unemployment linatakiwa kutatuliwa strategically. PSRS, TAESA, TAMISEMI, VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA pekee haviwezi maliza hii changamoto.

Hivyo basi ningependa kuandika machache ya namna serikali yetu pamoja na wadau wa maendeleo wanaweza kwa pamoja kupambana ili kutatua adha hii, tumuombe MwenyeziMungu atusaidie Aamin.

01) Kuwepo na programs maalum za kuwaanda vijana kupata maarifa nje ya waliyopata darasani katika masomo yao ya sekondari. Imagine vijana wa form 4 na 6 wanaenda kwa Mujibu au wanabaki street miezi kusubiri matokeo instead of enrolling them at VETA or other institutions ambazo hutoa Vocational education.

Huko vijana wanaeza pata maarifa thabiti kwa mazingira tulonayo. Mfano, mhitimu anamaliza secondary huku lugha anazozijua ni Kiswahili na English. Na hapo kwenye English tunajua kinachoendelea. Hivyo inahitaji kujipambanua kidogo walau vijana wapewe fursa za kujifunza lugha za ziada pamoja na skills nyengine kama computer, hairdressing, automotive repair, catering, fashion design, driving, na kadhalika. Hii itasaidia sana hata kama kijana akipata zero kwenye matokeo anayosubiri basi hatokosa kitu kwenye skills za kutaftia mkate wa siku.

02) Serikali inapaswa ku-encourage na ku-promote entrepreneurship and innovation. Kuwaambia vijana wajiajiri pekee haisaidii bali inatakiwa pia kuwapa motivation ya kujiajiri. Mbali na kupewa skills za kujiajiri, bali pia wanapaswa wapatiwe financial capital kwa njia nyepesi zaidi, msamaha wa kodi kwa startup ventures, utaratibu wa kupata new technology uwe mwepesi kusiwe na a lot of bureaucratic issues, na kuwe na economic policies za kuwalinda hawa wajasiriamali wa ndani.

03) Serikali kama mlezi inapaswa izipe tax relief kampuni zote zinazoajiri wazawa kwa kiwango kikubwa. Hii itatoa motivation kwa kampuni kuajiri wazawa ili zipate relief ya kodi.

04) Huduma muhimu zipelekwe vijijini ambapo kuna fursa nyingi za kilimo, ufugaji, na biashara nyenginezo. Hii itapunguza issue ya immobility of labour. Ukiunga na infrastructure development kurahisisha usafiri basi demand na supply of labour ita balance vzr. Penye uhitaji na fursa, wasaka ajira watafika na kuchapa kazi bila longolongo.

05) Serikali isimamie benefits za wafanyakazi wa sekta binafsi kama ambavyo inafanya kwa watumishi wa uma. Kuna baadhi ya kampuni watu wanafanya kazi bila contracts, hawalipwi stahiki zao kama wanavyopaswa kulipwa, wanateswa na kunyanyasika, wanapata kila madhila lakini hawapati utetezi. Hii inakatisha tamaa vijana kufanya kazi huko na wanaona bora wapambane serikalini penye ajira chache ili walau wapate job security na peace of mind.

Nimefika tamati, kila sifa njema anastahiki MwenyeziMungu.
 
Pole, ..kwani wewe unadhani yote uliyoyaandika Serikali haiyajui?

Ni kwamba SERIKALI ina Kiburi, Dharau na Ujeuri.

Nenda mahakani au bungeni kama unaona tabu sana!!!! #ulipoTupo and we don't care! That's your problems, not theirs
 
Ahsante. Serikali inaundwa na watu na watu hawafanani.

Hapo pa kuiona tabu, mimi sipo huko.

Kujali na kutojali kwa mwanadamu hakumuathiri mwanadamu mwengine ila kile alichoandikiwa na Mola wake.
 
Back
Top Bottom